Uganda: Aina Mpya ya Kifafa Yatishia Maisha ya Watoto.

Ugojwa unaofanana na Kifafa unaosababisha akili na mwili kwa ujumla kushindwa kufanya kazi vizuri, unaathiri watoto walio na umri kati ya mwaka 1 hadi miaka 10. Hadi sasa ugojwa huu umeonekana zaidi katika baadhi ya maeneo ya nchi za Sudani ya Kusini,Tanzania na upande wa Kaskazini mwa Uganda.

Ugonjwa huu hadi sasa haujapata tiba na haijafahamika unasababishwa na nini. Siku za hivi karibuni, dalili za ugojwa huu zimeonekana pia kwa baadhi ya watu wazima. Maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa huu zaidi, ni yale ya upande wa kaskazini mwa Uganda. Ugonjwa huu unawafanya watoto kushindwa kufanya shughuli yoyote ya uzalishaji; wasichana hawawezi hata kushika kisu ili kuandaa chakula, na kwa wavulana, hawawezi hata kushika jembe na kuotesha walau mbegu moja ya mmea.

Mwanaume wa miaka 18 anaweza kuonekana kama ni mvulana wa miaka 3, na anapaswa kubebwa na kusaidiwa kutoka nje ya nyumba ili angalau aweze kuota jua. Dalili za kwanza za ugonjwa huu ni kutikisa tikisa kichwa na kushindwa kula na kunywa. Na baadae mtoto anaharibikiwa akili na mwili kushindwa kufanya kazi.

Mwanahabari wa Uganda, Florence Naluyimba, ameshachukua hatua za awali kuchunguza na kuliweka bayana jambo hili. Anasema kuwa, pamoja na kuwa serekali inajaribu kutoa dawa katika vituo vitatu vya afya ili kuwasaidia waathirika, watu wanalazimika kusafiri umbali mrefu kwa miguu au kwa baiskeli ili kuvifikia vituo hivi. Wagonjwa hawawezi kwenda hospitali peke yao, hivyo wanapaswa kubebwa mgongoni au kubebwa kwa baiskeli na kusafiri umbali wa zaidi ya kilometa 30.

Ugonjwa huu mara nyingi unapelekea mtu kukakamaa na wakati mwingine hali hii huwapelekea hata kuangukia kwenye moto, kuangukia vitu vyenye ncha kali au kwenye mabwawa/ kwenye mito hali inayoweza kusababisha kifo au kupata majeraha makubwa. Watoto wengi wameshapoteza viungo vya mwili kama vile vidole katika ajali hizi. Wakati mwingine wagojwa wanaweza kuwa wadhaifu sana kiasi cha kushindwa hata kulia.

Kituo cha kukabiliana na ugojwa huu kimepanga kupulizia dawa kutoka angani ili kuangamiza inzi weusi wanaosadikiwa kuwa ndio chanzo kikubwa cha ugojwa huu. Bado haifahamika sana kama njia hii itaweza kusaidia au la. Wanavijiji nchini Uganda wanalalamika kuwa vipimo vilipelekwa nchini Marekani tangu mwaka 2010 lakini hadi sasa bado hawajapata taarifa za kuridhisha kuhusiana na kinga pamoja na visababishi vya ugojwa huu.

Zifuatazo ni baadhi ya picha na video kutoka kwenye mtandao wa YouTube kuhusiana na ugojwa huu.


Ugojwa wa kuanguka katika hatua zake za awali.
.
Picha kwa idhini ya ugandaradionetwork.com


Mtoto mwenye majeraha usoni baada ya kuanguka kwenye moto wakati alipokakamaa
Picha kwa idhini ya 256news.com

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.