Palestina: Makala Kuhusu Kifo cha Arafat yaibua maswali

Mnamo tarehe 3 Julai, 2012 kituo cha televisheni cha Al Jazeera ilionesha makala ambayo yalihusu uchunguzi wa kifo cha kutatanisha cha Rais wa Palestina Yasser Arafat. Alifariki dunia Mjini Paris mnamo tarehe 11 Novemba, 2004 na makala hayo yaliashiria kwamba hakufariki kwa njia ya kawaida ila aliwekewa sumu ya poloni.

Wakati na hata baada ya kuonyeshwa kwa makala hayo,  wa-Paletistina wengi wanaotumia twita walitwiti kutoa maoni na miitikio yao kuhusu ushahidi uliotolewa. Wengi wao hawakushangaa kuhusu madai ya kwamba Arafat aliwekewa sumu, jambo ambalo  kwa muda limedaiwa na watu wengi. Hata hivyo, madai ya kwamba sumu ya poloni ilitumiwa, huo ulikuwa ushahidi mpya wa kina.‏

Yasser Arafat katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi wa dunia mjini Davos, Januari 2001. Picha ya Remy Steinegger (CC BY-SA 2.0)

Mtumiaji twita, ‘Maoni kutoka Gaza’ alitwiti:

@ThisIsGaZa:الجزيرة تكشف حقائق جديدة عن وفاة عرفات عثر تحقيق للجزيرة استمر تسعة أشهر على مستويات عالية من مادة البولونيوم السام
في مقتنيات للرئيس عرفات
Al Jazeera imefunua ukweli mpya kuhusu kifo cha Arafat baada ya  uchunguzi wa miezi tisa, iligundua kiwango cha juu cha sumu ya poloni katika vifaa alivyokuwa akivitumia marehemu Rais Arafat

Na mimi mwenyewe nikatoa maoni:

@olanan: هلأ الكل يتساءل عن الجديد الذي قدمه وثائقي الجزيرة ‘والشعب كله كان عارف انو مات مسموم’. الجديد هو الادلة المادية.. بالأول كان اشاعات فقط!
Kila mtu anashangaa ni habari gani mpya zilizotolewa katika makala hayo yaliyoandaliwa na Al Jazeera, wakati taifa nzima lilifahamu kuwa aliwekewa sumu. Kilicho kipya ni kwamba ushahidi umeotolewa, na awali zilikuwa ni tetezi tu.
Wapalestinia wengi waliuliza iweje makala hayo yatangazwe sasa, na wengine wakaoanisha habari hizo kuwa hila.

Mtumiaji wa mtandao wa twita Majd alijibu:

@majds: قمة الوقاحة: ان يتواطؤا ل 8 سنوات باخفاء حقيقة اغتيال الشهيد ياسر عرفات، وبعدها عندما يأتي من يكشف الحقائق بمهنية، يقولون له: توقيتك مشبوه!!
Ni jambo la kusikitisha inapotokea kuwa wale walioshirikiana kuficha ukweli kwa miaka minane kuhusu ukweli  wa kifo cha Yasser Arafat, kisha eti baadaye kujitokeza kueleza ukweli. ‘Kulizungumzia suala hili sasa hivi kunatia wasiwasi!’

Kaburi kubwa la Yasser Arafat. Picha ya Mary-Katherine Ream (CC BY-NC 2.0).

Nour Abed hakuficha maoni yake hasi kuhusu Al Jazeera na wanahabari kwa jumla, lakini aliisifu idhaa hiyo kwa makala hayo:

@NourGaza: كلنا يعلم أن قناة الجزيرة كغيرها مجرد إعلام موجه له أسبابه وأهدافه وراء كل طرح جديد, ولكن هذا لا ينفي أنها كشفت معلومات جديدة عن موت ‎‫#عرفات‬!
Wote tunafahamu kuwa Al Jazeera kama vituo vingine vya habari inayo agenda yake, ina sababu na malengo kwa kila wanachofanya, lakini  huwezi kukanusha kwamba wamefichua ripoti mpya kuhusu kifo cha Arafat.

Diana Alzeer alitarajia kupata majibu zaidi:

‏@ManaraRam:  Swali lingine ambalo nataka nijibiwe ni  “N'nani aliyemuua Arafat?”

Ismaeil Mohaisen alitwiti kuhusu baadhi ya tuhuma dhidi ya Mamlaka ya Palestina:

@IsmaeilFadel: لا زلنا بإنتظار تعليق من السلطة..! خصوصاً وأن الوثائقى أشار ببعض أصابع حتى ولو بشكل غير مُباشر! هناك أشخاص متورطين، لا شك فى ذلك! ‎‪#Arafat
Bado tunangoja maoni kutoka Mamlaka ya Palestnia.  Haswa  kwa sababu makala hayo yalionyesha kuhusika kwa watu fulani. Hakuna shaka kuhusu hayo!‬

Kwa namna hiyo hiyo, Rami Khrais alitwiti:

‏@Abuelrim: أهم ضربة للسلطة الفلسطينية بخلاف طلب سهى استخراج جثة زوجها للتحقق من التسمّم، هو إشارة التقرير أن أي تحقيق لم يجر منذ وفاته.
Pigo kubwa kwa mamlaka ya Palestina -pamoja na maombi  ya Suha Arafat kutaka kuchunguzwa kwa sumu kwa mabaki ya mumewe -je, ripoti hiyo yaashiria kwamba hakuna upekuzi rasmi uliofanywa baada ya kifo chake?

Makala hayo yalikamilika kwa Mjane wa Yasser Arafat, Suha Arafat kuomba mamlaka ya Palestinia ifukue mabaki ya marehemu ndio uchunguzi uendelelee. Rais Mahmoud Abbas alitoa taarifa iliyosema kwamba mamlaka  ya Palestina haikuona sababu ya kufukua mabaki yake.  Kwa sasa tunasubiri tuone kitakachotendeka  baadaye.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.