Cameroon: Ndoto za Umeme kwa Ajili ya Maendeleo ifikapo 2035

Makala haya ni sehemu ya habari zetu maalumu za Mahusiano na Usalama wa kimataifa

Power lines in Cameroon

Mikondo ya umeme ikionekana juu ya majengo nchini Cameroon, 2008. Picha ya Zzilch kwenye mtandao wa Flickr (CC BY-NC-ND 2.0)

Baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine mwezi Novemba 2011, Rais Paul Biya wa Cameroon alitangaza [fr] kwamba ndani ya muda mfupi, nchi yake ingeongoza kwa kuwa “eneo la ujenzi”. Lengo kubwa la awamu yake mpya ya urais kwa nchi ya Kameruni ni kufikia hadhi ya soko linaloibukia ifikapo 2035 kupitia hatua kwa hatua za “mafanikio makubwa” katika maendeleo ya miundo mbinu ya usafiri na nishati [fr]. Kutimia kwa ndoto hii ndani ya muda uliopangwa kumeshindwa kuwashawishi [fr] wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa, kwa sababu tu changamoto zilizopo ni nyingi.
Nishati, na hususani umeme, ni sekta yenye matatazo mengi. Kama ilivyo katika nchi nyingi za Kiafrika, Cameroon inataabika na ugavi duni wa umeme nishati ya umeme.

Mwandishi Leopold Nséké anaeleza katika makala yake iliyochapishwa kwenye jarida la Afrique Expansion Magazine:

Kule kuwa na nyenzo duni, bara la Afrika imefurikwa na nyenzo zilizopitwa na wakati pamoja na utawala duni na butu wa raslimali zilizopo. Ikiwa na takribani asilimia 15 ya idadi ya watu duniani, ni ajabu kabisa kwamba Afrika inatumia asilimia 3 tu ya umeme unaozalishwa duniani.

A village with no electricity

Hakuna umeme kwenye vijiji vya Mafa Kilda, umeme unapita tu kwa nguzo za umeme (ukitokea Ngong kwenda Garoua). Picha ya Philippe Semanaz kwenye mtandao wa Flickr mwaka 2006 (CC BY-SA 2.0)

Kwa mujibu wa makadirio (fr) yasiyorasmi, ni asilimia 20 tu ya idadi ya wa-Cameroon wameunganishwa na umeme. Kwa hakika, pamoja na kuwa na umeme, watu hao hukumbana na kero ya kukatika kwa umeme takribani kila baada ya siku tatu. . Umeme unaendelea kuwa bidhaa ghali kwa raia wengi kuweza kumudu bei yake. Kampuni binafsi ya AES Sonel, kwa mfano, hivi karibuni ilitangaza kupanda kwa bei ya umeme [fr] kwa asilimia 7 kuanzia tarehe 1 Juni, 2012.

Kutokuwepo kwa uhakika wa upatikanaji wa umeme pia kunaleta tishio kwa maendeleo ya viwanda nchini Cameroon, jambo ambalo litakwaza ndoto ya nchi hiyo kuwa nchi yenye uchumi imara ifikapo 2035. Utafiti [fr] uliofanywa na Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Younde ulibainisha kwamba:

Hasara za uzalishaji katika makampuni ya viwanda zilikadiriwa kuwa EU milioni 91.5 kwa mwaka kwa sababu ya matatizo ya ugawi wa umeme. Matokeo haya yalionyesha kwamba kiwango pungufu na kilicho duni cha ugawi wa umeme kimezorotesha maendeleo ya umeme.

Aidha, ugavi wa umeme usioaminika unagusa maisha ya idadi kubwa ya watu nchini humo.Feowl ni mradi mpya unaotaribiwa na jamii unaolenga kukusanya, kusaili na hatimaye kutoa takwimu ambazo kwa sasa hazipatikani juu ya athari za ugavi duni wa umeme huko Douala, eneo linalosifika kwa shughuli za uchumi nchini humo.

Kwa vile Cameroon kimsingi inategemea, uzalishaji wa umeme utokanao na maji , serikali imezindua ujenzi wa bwawa la Lom Pangar lililo mashariki mwa nchi hiyo. Mradi huo -unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na mashirika mengine ya kimataifa- unachukuliwa kuwa na umuhimu wa pekee katika kufikiwa kwa ndoto za nchi hiyo za kuwa na uchumi imara.
Bwawa hilo linalotazamiwa kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme nchi humo litakuwa na ukubwa wa mita za ujazo bilioni 7.250 litakalotunza maji kwa eneo lenye kilomita za mraba 610. Maji yatahifadhiwa kwa matumizi hasa wakati wa ukame katika mabwawa hayo yaliyopo kwenye mto wa Sanaa, hivyo kusaidia kuzalisha umeme zaidi.

Blogu ya Christiane Badgley inaangazia baadhi ya mapungufu ya mradi huo. (Mwanablogu huyo) anawasiwasi kwamba umeme utakaozalishwa unakusudiwa zaidi
kutosheleza mahitaji ya umeme wa viwanda vya nchi hiyo:

…masikini wa mijini na vjijini hawaonekani kuwa wanufaika wa mradi wa Lom Pangar. Badala yake, bwana limebuniwa kudhibiti maji ya mto Sanaga ili kuongeza uzalishaji wa umeme kwenye mashine za kufua umeme zilizopo tayari na zile zinazokusudiwa kujengwa ili kutosheleza mkondo wa umeme wa kusini pamoja na mgodi wa machimbo ya madini ya aluminiam wa Alucm unaotumia umeme zaidi nchini humo. Mgodi huo wa Alucam unaomilikiwa kwa ubia wa serikali ya nchi hiyo na kampuni ya ki-Kanada iitwayo Alcan, unapanga kuongeza uzalishaji wake mara dufu na hivyo unahitaji vyanzo vipya nafuu vya nishati kufikia malengo hayo.

ISN logoMakala haya ni sehemu ya tafsiri ya ki-Hispania, ki-Arabu na ki-Faransa ambazo zilitolewa na Mtandao wa Usalama wa Kimataifa (ISN) kama sehemu ya ushirikiano wa kutafuta sauti za raia wa kawaida katika masuala ya mahusiano na usalama wa mataifa duniani. Tembelea blogu ya ISN ili kuona habari nyingine zinazofanana na hii.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.