Lesotho: Uchaguzi wa amani ambao hukuusikia

Lesotho ilifanya uchaguzi wa wabunge kwa amani siku ya Jumapili. Chama kinachotawala nchini humo, Democratic Congress cha Waziri Mkuu Pakalitha Mosisili kilishinda kwa asilimia kubwa ya kura lakini kikishindwa kuvuka nusu ya kura. Vyama vya upinzani vya nchini humo vimeungana kwa makusudi ya kuunda serikali.

Kwa nini vyombo vikuu vya habari vya kimagharibi havikwambii kuhusu uchaguzi huo wa amani wa Lesotho? JohnsonJJ anasema hilo halipaswi kukushangaza. Anaeleza namna wambukuzi wa kimagharibi wanavyoamua kipi chastahili kubeba uzito habari barani Afrika:

Haishangazi kwamba suala hili halijapata uzito wa kutosha. Kwa hakika, nchi hii huwa haisikiki vya kutosha isipokuwa kama inakumbwa na mambo yanayohusiana na ngono na ufukara yanayokazia namna Lesotho ilivyo na hali inayotisha, holehahe na inavyosumbuliwa na UKIMWI.


Mpiga kura nchini Lesotho akonyesha kumwunga mkono Waziri Mkuu Phakalitha Mosisili. Picha kwa hisani ya Simon Allison&dailymaverick.co.za

Lesotho, JohnsonJJ anaendelea kujenga hoja, haina hadhi yoyote kwa maana ya kutambuliwa nchini Marekani:

Vyombo vya habari vinavyoanzishwa vinatufahamu vyema. Vinajua kwamba habari nyepesi nyepesi zinasoko kubwa nchini Marekani. Hatuna tofauti kubwa. Ndio maana tulivutwa sana na mawazo, kwa mfano, kwamba mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalikuwa ni matokeo ya “chuki za asili za kikabila” badala ya mukhtadha wa siasa za kijiografia. Ni kwa sababu hiyo hiyo tulijifunza kwamba nchi iliyoshindwa ya Somalia ilishindwa kwa sababu ya vikundi vya magaidi wenye hasira wasiowaza kingine zaidi ya kuwaua wa-Marekani. Na ndivyo unavyojifunza kwamba watoto wote wa ki-Afrika wana matumbo ya utapiamlo huku nyuso zao zikizungukwa na mainzi siku zote. Ndivyo tunavyojifunza kutoka kwa Nicholas Kristof (mtu mzito kuelewa kupata kutokea) kwamba wanawake wengi wa ki-Afrika wanateseka na “ukeketaji wa wanawake” na kwamba vitendo hivyo vinahatarisha maisha ya wanawake barani kote.

Ni kwamba Lesotho ni ndogo sana na kwa kweli hana hadhi yoyote ya kupata uzito wa kihabari, na kwa hali yoyote ile, nchi ndogo yenye jamii ya kistaarabu inayokua? Kamwe haitopewa uzito nchini Marekani. Kama kuhusiana kwetu kusiko na mantiki na vyombo vya habari ni utambulisho, basi hata hatujajihusisha kihalisia na vyombo vyetu.

Zachary Rosen anaonyesha kwamba hata Lesotho inapogonga vichwa vya habari, makala hizo mara nyingi huhusu UKIMWI na ufukara:

Jumla ya yote, makala chache zimejaribu kuondoka kutoka habari za juu juu na kujikita kwenye masuala mazito ya hali ya kisiasa ya nchi hiyo na mana ya matokeo haya ya uchaguzi.

Ni kweli pia kuwa hata vyombo vya habari vya Afrika Kusini vilipuuza uchaguzi wa Lesotho. Lesotho imezungukwa pande zote na Afrika Kusini.

@fanamokoena: Inasikitisha kwamba vyombo vya habari vya Afrika Kusini vinatupa habari za mara kwa mara kuhusu uchaguzi wa Ufaransa lakini vinashindwa kufanya hivyo kwa nchi jirani ya Lesotho. Huku ni kutokuwajibika.

@BelindaaPheto: Inahuzunisha kuona vyombo vyote vya habari vya Afrika Kusini havionyeshi kufuatilia vya kutosha ama havifuatilii kabisa uchaguzi wa Lesotho.

@simonallison: Ni ajabu lakini ndio ukweli wenyewe: Nilikuwa mwandishi pekee wa magazeti na tovuti za habari za Afrika Kusini kuandika habari za uchaguzi wa Lesotho. Wengine wote walizipata habari hizi kwa njia ya simu. Ujinga.

@sheofnations: @simonallison Kupuuzwa huko kunaleta maana kukifanywa na vyombo vya habari vya kimataifa, lakini ni tatizo sana inapotokea kuwa habari kuhusu bara hili zinachunjwa kupitia vyombo vya habari vya kimataifa.

@simonallison:@sheofnations kweli, karibu kila tunachosoma kuhusu Afrika kutokea Afrika Kusini kimenyofolewa na wahariri wa kizungu na kimarekani kutoka kwa hadhira yao…

Lesothoni nchi iliyozungwa na ardhi pande zote ikiwa imezungukwa na nchi ya Afrika Kusini. Ni nchi ya kifalme inayoendeshwa kidemokrasia. Waziri Mkuu ni mkuu wa serikali wakati mfalme ni mkuu wa heshima. Jina Lesotho limetokana na nchi ambayo watu wake wanazungumza lugha ya ki-Sesotho.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.