Amerika Kusini: Waathirika wa ‘biashara’ ya kukuza matiti waingia mtandaoni

[Viunganishi vyote vinakuunganisha na kurasa za lugha ya Ki-Hispania isipokuwa ikisemwa vingine]

Matatizo yanayosababishwa na urekebishwaji matiti wenye makosa yamezua mgogoro mkubwa katika tasnia ya afya ya jamii. Kumekuwa na maswali juu ya tunu za kimaadili dhidi ya kujipatia fedha katika njia hii ya kurekebisha matiti barani Amerika ya Kusini. Kengele ya kwanza ya onyo ilisikika mwanzoni mwa mwaka 2010. Katika kipindi hicho kulikuwa na ongezeko la watu waliokutwa na saratani, ambapo ongezeko hilo lilihusishwa na ‘biashara’ ya utengenezaji matiti ya bandia.

Kadri miezi ilivyopita, wasiwasi nao umeongezeka zaidi kiasi kwamba wanawake wengi wameungana kwenye tovuti za kijamii ili kuweka maoni yao waziwazi. Wanafanya hivyo ili kubadilishana taarifa pamoja na kupanga hatua gani za kisheria wachukue.

Examination of a silicone breast implant. Photo by Wideweb Videographer, copyright Demotix.

Uchunguzi wa “utengenezaji” wa titi kwa kutumia madini ya Silikoni. Picha ya Wideweb Videographer, haki miliki Demotix.

Matukio haya ni mengi barani kote. Hata hivyo, tutataja machache tu, yaani wale wanawake walioguswa na kupaza sauti zao kupitia mtandao wa lugha ya ki-Hispania wa Web 2.0. Bado kuna maswali mengi ambayo hayajapatiwa majibu: Nani anapaswa kulipa fidia? Itakuwaje baada ya virutubisha titi kuondolewa? Uwezekano wa kupatwa na madhara ya kiafya ni mkubwa kiasi gani? Waathirika wana maoni gani? Na pia: Suala hili linatoa picha gani kuhusu Amerika Kusini, kwa nini kuna mahitaji makubwa ya watu kutaka kufanyiwa upasuaji au kutengeneza viungo vya miili yao kwa ujumla, hususani kupandikizwa virutubisha matiti?

Nchini Columbia, kuna matukio mengi, na wanawake wengi wamejipanga kupitia vikundi vya mtandao wa Facebook. Mifano miwili ya vikundi hivi ni Wale walioathirika na virutubisha matiti nchini Columbia na Mwanamke aliyeathirika kwa kukuza matiti nchini Columbia, ambalo pia limetengeneza blogu, ambapo baadhi ya watu wamehoji kuwajibika kwa taasisi za umma zenye dhamana ya afya ya jamii:

 Las prótesis PIP se vendieron en Colombia durante once años legalmente, a pesar de que la autoridad colombiana nunca tuvo documentos que probaran que sus componentes podrían ser utilizados en seres humanos…

Virutubisha titi vilikuwa vinauzwa kwa mujibu wa sheria nchini Columbia kwa muda wa miaka 11, hata kama mamlaka zinazohusika nchini humo hazikuwahi kuwa na ujuzi wa kuthibitisha kwamba viini hivyo vingeweza kutumika na binadamu…

Wengine wametengeneza blogu kusimulia yaliyowapata, kama blogu hii iitwayo “Hapana kwa virutubishi hai.” . Vikundi hivi na blogu zinakusanya shuhuda, maswali na marejeo kuhusiana na virutubishi matiti hivyo, utunzaji wake na namna ya kuvitoa. Pia, wale wanaoshiriki wanaweza kupata taarifa zitakazowawezesha kujua hatua za kisheria wanazoweza kuchukua pamoja na kujadili uwezekano wa kubadilisha virutubishi hivyo vya matiti.

Nchini Chile, kuna waathirika waliobadilishana mawazo kuhusu hali wanazokumbana nazo, akiwemo Daniela Campos, ambaye alitumia chaneli yake ya You Tube kusambaza tahadhari pamoja na kutoa wito kwa ushiriki wa taasisi za umma katika uchunguzi wa hali hiyo na kuwaadhibu wale wanaohusika. Daniela aliwahimiza wafutiliaji wa habari zake kuendeleza madai haya kwenye tovuti za kijamii, na akatengeneza  kikundi cha mtandao wa Facebook kuwataka wake wanaohusika na janga hili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria itakapofikia mahali pa kulazimisha mchakato wa kuviondoa virutubisha matiti hivyo.

http://youtu.be/TZNmgCUPvlM

Hata hivyo, Hernan Corral, kupitia blogu yake ya Derecho y Academia alionyesha matatizo ya kisheria yanayokwamisha suala hili:

¿Podrían invocar las mujeres chilenas afectadas un régimen como éste? Lamentablemente, nuestro ordenamiento jurídico no ha recepcionado aún este tipo de responsabilidad sin culpa. (…) Las afectadas chilenas, invocando el registro del Instituto de Salud Pública como producto médico (y por tanto eventualmente peligroso), podrían demandar al fabricante. Pero si Poly Implants Prothéses no tiene representantes en Chile, les será muy difícil emplazar a la compañía.

Je, mwanamke aliyeathirika wa Chile anaweza kuthibitisha madai (ubovu wa bidhaa) kama haya? Bahati mbaya, mfumo wetu wa sheria haujaweza bado kubeba wajibu huu pasipo makosa (…) Wa-Chile walioathirika, wanaodai kuandikishwa kwa Taasisi ya Umma ya Afya ya Jamii kama vile bidhaa za dawa (na bila shaka za hatari), wanaweza kumshitaki mtengenezaji. Lakini kama watengenezaji hawa wa viini hivi vya kukuuzia matiti hawana wawakilishi nchini Chile, basi itakuwa vigumu sana kwa wao kuishitaki kampuni husika..

Kutoka Miami, Sofía Jiménez alifungua blogu kusimulia yaliyomkuta  baada ya kuwekewa virutubisha matiti. Blogu hiyo inatoa uchambuzi wa kina hatua za kuchukua kabla na baada na pia habari za namna ya kujua ikiwa virutubisho hivyo “vimechipua” kwa kasi:

El hecho de estar tan cerca de testimonios de mujeres sufriendo de todo tipo de síntomas y complicaciones me hizo abrir un poco más los ojos. Y me pregunte a mi misma, ¿son los implantes tan seguros como nos quieren hacer pensar?

Kwa kufuatialia kwa karibu masimulizi ya wanawake wanaotaabika kwa kila namna ya dalili na matatizo, hiyo imenisaidia kufungua macho yangu zaidi kidogo. Na ninashangaa, je, vikuza matiti hivi ni salama kama tunavyojiaminisha?

Lakini nini kiko nyuma ya idadi kubwa ya upasuaji wa matiti unaofanyika Amerika Kusini? Wanablogu wawili wanalitafakari hili kutoka Venezuela. Naky, kupitia blogu yake inayoitwaProDavincianatoa ushuhuda wa wanawake kadha wa kadha ambao wanafanya kazi jirani na ofisi yake:

[Una de ellas] Aún debe la mayor parte del crédito bancario con el que financió sus cirugías (…) tiene 24 años (…) gana poco más de salario mínimo y tiene prótesis PIP de 400 cc. Le da gracias a Dios de haber tenido el dinero para pagar todo eso (…) “No todas llegamos al Miss Venezuela, pero hay que hacerle creer al resto que sí.”

[Y otra más opina:] “La estatura que te dan los tacones es nada frente a la manera que te crece el ánimo cuando un tipo se te queda viendo como si quisiera arrancarte la blusa”

De las nueve en conversa, sólo una sabe el tipo de prótesis que tiene, conserva el certificado y pudo hablar con su cirujano, que le garantizó que todo está bien. El resto hizo algunas llamadas, pero se encuentran en el estadio de la negación. Ninguna está dispuesta a operarse de nuevo (…) Les resulta impertinente pensar que deban renunciar a su sinuosidad sin nada que les compense la ausencia. Karla llegó a sugerir que el mismísimo gobierno debiera pagar las nuevas prótesis y reconocer mediante un permiso especial, la ausencia laboral de las afectadas por tal circunstancia (…)

[Mwanamke mmoja] Bado ana madeni makubwa ya mikopo ya benki iliyogharamia upasuaji wake mara kadhaa (…) ana umri wa miaka 24 (…) analipwa mshahara kiasi kudogo tu, pengine juu kidogo ya kima cha chini cha mshahara, yaani fedha za Venezuela 400. Ni vikuza matiti. Anamshukuru Mungu kwa kuwa na pesa za kulipia yote hayo (…) “Sio sote tunaweza kufanikiwa kuwa Mlimbwende wa Venezuela, lakini inatufanya tuamini kwamba ndiyo, tungeweza.”

[Mwanamke mwingine] “Kimo kirefu unachokipata kwa kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu hakiwezi kufanana na vile unavyojisikia pale mwanaume anapokukodolea macho utafikiri anatamani kuchana blauzi yako.”

Kati ya wanawake tisa waliohojiwa, ni mmoja tu anajua aina ya vikuzaji vilivyowekwa kwenye matiti yake, amehifadhi cheti na aliweza kuzungumza na daktari aliyehusika na upasuaji kumhakikishia kwamba kila kitu kilikuwa sawa. Waliobaki walipiga simu kadhaa pasipo majibu. Hata kuna mmoja wao aliye tayari kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine (…) Wanaona ni kitu kinachoumiza na kisicho faida wanapofikiri kuwa wanatakiwa kuondoa michirizi kati ya matiti yao bila kitu chochote cha kuweza kufidia kuondoka kwayo. Karla anapendekeza kwamba serikali yenyewe ndiyo yapaswa kuwalipia kwa ajili ya virutubisha matiti vipya na kutoa ruhusa maalumu kwa wanawake walioathirika kukosekana kazini kwa sababu ya zoezi hili (…)

Mwisho, huko Aporrea, Antonio Rangel alihoji mtazamo wa jamii kuhusu kwa nini kuna mahitaji ya kubadili viuongo, na kwa nini upasuaji unapata umaarufu:

Es imposible negar que algunas mujeres, víctimas de la poderosa alienación o enajenación mental que las ha hecho creer que ser más sexy o atractiva las conduce directamente al éxito social y económico, convertidas de la noche para la mañana en señuelos sexuales irresistibles, serán dotadas del poder de seleccionar entre la manada de turulatos seguidores a quien ellas consideren que es el mejor “partido” (…) Les resulta impensable que (…) los reinados de belleza, los desfiles de moda, los cosméticos mágicos, son las mismas que se lucran con las prótesis…

Haiwezekani kukanusha kwamba baadhi ya wanawake ni waathirika wakuu wa mikopo na ujinga unaowasababisha kuamini kwamba kuonekana mwenye mvuto wa kimapenzi au kuvutia zaidi basi moja kwa moja kunahusiana na mafanikio ya kijamii na kiuchumi. Wengi wanabadilika ghafla na kuwa watu wasioweza kukataa vishawishi, watumwa wa ngono, wanafikiri kuwa watapata fedha kwa kuchaguliwa kati ya kundi la wafuasi waliochanganyikiwa ambao wao wanawachukulia kama “watu wakukamatwa” sawa sawa (…) Inakuwa vigumu kwao kufikiri kwamba makampuni yale yale yaliyogharamia hamu yao ya kuwa warembo, maonyesho ya ulimbwende, vipodozi vya gharama, ndiyo yayo hayo yanayofaidika na viungo vyao bandia.

Maswali zaidi na mijadala itaendelea kujaza nafasi kwenye mtandao. Mamia ya maelfu ya wanawake bado wanashangaa juu ya masuala ya kina yanayozunguka ukuzaji huo wa matiti na matibabu yake. Madhara ya upasuaji wa kurekebisha sehemu ya mwili na shauku kubwa inayoambatana na matumizi ya sehemu hizo katika ulimwengu wa kitabibu yamekuwa ni kiini cha mijadala mingi. Ingawa vita vya kisheria havijaanza rasmi, mawazo yanajitokeza kuwa changamoto ya nini hasa kinachowasukuma wanawake kujibadili sehemu za miili yao na namna wanawake wanavyoshughulikia misukumo hii inayowekwa kwao.

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.