Kenya: Uanahabari wa kiraia wa Mtandao wa Habari wa Kibera

Vijana wa Kibera, Kenya, kitongoji ambacho kinajulikana kwa baadhi kama eneo kubwa la hovyo zaidi ya yote barani Afrika, wamedhamiria kuonesha sura nyingine ya mahali wanapoishi. Huku wakiwa na kamera mkononi, wanavinjari mitaa wakitafuta habari ili kuionesha dunia jinsi Kibera inavyojiona yenyewe.

Mradi huo ulianza mwezi Aprili 2010, ukiongozwa na Map Kibera pamoja na Kibera Community Development Agenda (KCODA). Walianza na wanahabari vijana wawili tu na hivi sasa timu hiyo ina vijana wanaofikia 14 ambao wanarekodi video hizo, wanahariri na kuzipakia kwenye mtandao wa intaneti: siyo tu kwenye tovuti yao Kibera News Network bali pia kwenye Voice of Kibera, tovuti ambayo inaorodhesha video zao kwenye ramani na pia habari nyingine zinazotumwa na watu kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu za mkononi na hata kwa njia nyingine nyingine.

Kibera News Network in Kenya

Mtandao wa habari wa Kibera nchini Kenya

Maudhui yapo ya namna nyingi: kuanzia masuala ya usalama wa ajira, mpaka taarifa za moto au ajali za gari moshi, na hata matukio ya kitamaduni na shughuli za siasa. Video hii inayofuata, fkwa mfano, inaonesha jinsi vijana wa kiume walivyoikubali ajira hii isiyo ya kawaida, kwa Kibera: wanamiliki na kufanya kazi katika duka ra urembo, wanatoa huduma kama vile za utunzaji wa mikono na kucha pamoja na ususi:

Katika video hii nyingine tunamtembelea Kevin Irungu, kijana wa kiume ambaye anapata kipato chake kutokana na sanaa:

Mifano yote hiyo inaonesha jinsi ubunifu na uchapa kazi unavyoweza kulipa. Hata hivyo, kwa wengine huko Kibera kujipatia kipato ni pambano lisilo na mwisho kama inavyooneshwa na hawa wafuaji ambao wanafanya kazi kwa bidii na wakati mwengine huwa hata hawalipwi:

Huko Kibera, afya ni suala muhimu sana: mitaro wazi ya majitaka na wingi wa watu vinamaanisha kwamba magonjwa ya kuambukiza yanaweza kusambaa haraka. Na ukweli kwamba watu wengi hawana rasilimali za kiuchumi kuweza kununua dawa, kiurahisi ugonjwa unaweza kugeuka na kuwa mlipuko wa ugonjwa.

Unaweza kutizama zaidi video kwenye tovuti ya Mtandao wa Habari wa Kibera au katika idhaa yao ya YouTube.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.