Attahiru Jega: Kiongozi wa Tume ya Uchaguzi ya Naijeria au Mtekaji?

Huku zikiwa zimebaki saa chache tu kufikia Uchaguzi Mkuu wa 2011 (kabla uchaguzi haujaahirishwa), yupo mtu mmoja aliyebeba ufunguo wa kuendelezwa ama kusitishwa kwa mapinduzi ya kijamii kupitia sanduku la kuranchini Naijeria. Uchaguzi wa Bunge unafanyika tarehe 2 na ule wa Rais unafanyika tarehe 9 Aprili 2011.

HABARI MPYA 04/03: Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza kwamba chaguzi zote zimesogezwa mbele kwa juma moja, kwa sababu ya kuchelewa kufika kwa vifaa vya kupigia kura.

Attahiru Jega, profesa wa Sayansi ya Siasa na mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa kiasi kikubwa ndiye atakayeamua juu ya kuhalalishwa kwa zoezi la upigaji kura ndani ya majuma matatu.

Attahiru Jega, a professor of Political Science and head of the Independent National Electoral Commission.

Attahiru Jega, profesa wa Sayansi ya Siasa na mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi (INEC) ilikuwa na tatizo la kuaminika wakati mtangulizi wa Jega, Maurice Iwu, alipokuwa akishikilia kiti hicho. Katika maneno ya Patrick Utomi (ambaye mpaka hivi karibuni alikuwa mgombea Urais wa chama cha Social Democratic Mega Party (SDMP):

Kama ambavyo imesambazwa sana katika maandishi na kukubalika uchaguzi wa mwaka 2007 ulikuwa ni mchezo wa kuigiza. Lakini si kule kuwa mchezo wa kuigiza pekee ndiko kulikonisumbua. Ilikuwa ni kiwango cha uovu katika mchakato na mtazamo uliosambaa kwamba ili upate nafasi katika siasa ilikubidi kuuza roho yako, dhamira na utu wako. Nilishawishika kuwa kunaweza kuwepo njia nafuu, njia tafauti.

Hainishangazi hata hivyo kuwa:

…mtu anayeongoza chombo cha uchaguzi lazima aonekane kuwa hana hatia yoyote, mwenye uaminifu ambao upo wazi na vile vile asiye na upendeleo. Haitoshi tu kuashiria sifa zilizotajwa hapo juu, ni muhimu sana kwamba hisia zilingane na uhalisia.

Kuyaishi matarajio, Jega alihakikisha kwamba habadiliki kutoka kuwa refa kuwa mchezaji asiyependelea katika uchaguzi. Get2Central anaandika kwamba:

Saa arobaini na nane kuelekea kwenye uchaguzi mkuu katika nchi ukianzia na upigaji kura wa kuchagua wabunge, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi, INEC, Prof. Attahiru Jega, alitangaza jana kwamba hakuwa kwenye shinikizo la kuchezea (kuchakachua) mchakato wa uchaguzi ili kumpa yeyote faida isiyo halali na kwamba hata shinikizo hilo linatokea sehemu yoyote, hatalazimika kukubaliana nazo.

Bosi huyo wa tume anasisitiza kuwa:

…Huku kukiwa na nyenzo za usalama, (ambazo) kama sanduku la kupigia kura litachanwa ama kubadilishwa, tume itajua. Pia, kama makaratasi yatabadilishwa au kuchukuliwa kwenda kwenye maeneo yasiyolengwa, Tume, INEC itajua. Katika mkondo huo huo, kama karatasi za matokeo zitachanwa na kubadilishwa kiujanja-ujanja, tume itajua.

Kwa namna kama hiyo, Jega amewatupia mzigo wanasiasa na wanasheria.

Kwa Tume, INEC, ninaweza kusema kwa uhakika na kwa kujiamini kwamba tuko tayari kwa ajili ya uchaguzi, swali badala yake linapaswa kuwa, je wanasheria na wanasiasa wako tayari? Tumeweka mfumo unaotakikana tayari si tu kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa haki na unaoheshimika, lakini pia kuhakikisha kuwa uwanja wa mchezo ni sawa kwa wagombea wote. Ninafanya kila ninaloweza kuhakikisha kwamba makosa ya nyuma hayarudiwi…Kwa hivyo, swali si ikiwa tume, INEC, iko tayari, lakini ni ikiwa wadau wengine wako tayari. Mashaka yetu kwa wakati huu yapo kwa wanasiasa na wanasheria

Haya si maneno matupu, yanayotoka kwa mtu mwenye historia ndefu na inayoogofya:

…kama Rais wa zamani wa Chama cha Wanataaluma wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (Naijeria), mwanaharakati wa jamii anayeheshimika na mtetezi wa haki za binadamu.

Posti hii kwenye twita inajumuisha matarajio ya wa-Naijeria wengi inayomhusu bosi huyo wa tume, INEC, na uchaguzi wa mwaka 2011 nchini Naijeria:

Sitadanganya. Mwenyekiti wa tume, INEC, Attahiru Jega ananikuna. Ninatarajia atafanya kama alivyoahidi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.