Misri: Basboussa kwa Urais!

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu tunazowaletea kuhusu Mapinduzi ya Misri ya Mwaka 2011.

” “Mtangazaji habari wa zamani wa televisheni ya Misri na mwanaharakati Bothaina Kamel alitangaza kwenye ukurasa wake wa twita usiku wa Ijumaa [ar] saa za Cairo kwamba ana mipango ya kugombea urais kwenye duru inayofuata ya uchaguzi, na kumfanya awe mwanamke wa kwanza kutangaza nia ya kutaka kuingia kwenye ofisi kuu nchini Misri”, Manar Ammar

Hivi ndivyo Manar Ammar alivyoripoti habari za Bothaina Kamel kugombea kwenye uchaguzi wa Urais wa Misri. Kamel (@basboussa1) amepokea miitikio mchanganyiko kutoka kwa watumiaji wa twita.

Mtumiaji wa Twita @FaresADLhakuweza kuamini habari hiyo, kwa hiyo akamwandikia Kamel akishangaa kama habari hizo zilikuwa zimethibitishwa ama zilikuwa ni uvumi tu:

@FaresADL: @basboussa1 ni kweli kabisa unagombea uraisi?

Fatma Eman, ambaye ni mtetezi wa usawa wa mwanamke aliandika kuhusu habari hizo:

@fatmaemam: Bothina Kamel mgombea mwanamke wa kwanza na wa pekee nchini #Egypt , mfuatilie hapa @basboussa1 , katika mshikamano #womenrights #jan25
Photo taken from the Facebook account of Bothaina Kamel; participating in a demonstration during the World Day Against Corruption.

Picha iliyochukuliwa kwenye ukurasa wa facebook wa Bothaina Kamel; akishiriki maandamano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vita Dhidi ya Rushwa duniani

Lara (@FarawlaLawra) aliiona habari hiyo kuwa nzuri, bila kujali ikiwa ameshawishika kumpigia kura ama la:

@FarawlaLawra: @basboussa1 ninajisikia fahari na furaha unagombea –ni hatua moja mbele kuifungua jamii kuelekea kwenye haki sawa (hata kama ninaweza nisikupigie kura wewe)

Mahmoud Salem, anayefahamika pia kama @Sandmonkey, pia aliandika kumuunga mkono:

@Sandmonkey: @basboussa1 ana ma3aky ya rayessah 3ala fekra. mpaka hapo kura yangu umepata

Katika video hii iliyopandishwa kwenye YouTube na mtumiaji tarehe 3 Aprili, 2011, Kamel anatangaza mipango yake ya kugombea Urais [ar].

Watu kadhaa walitoa maoni juu ya video hiyo hapo juu kupingana na nia yake ya kugombea Urais.

MyHamosa: انا ارفض ان تحكمنا امراة
MyHamosa: Sikubaliani sisi kutawaliwa na mwanamke
Algeriangirls123: اعتقد انها لن تحصل حى على التأييد لمن اجل دخول الأنتخابات
Algeriangirls123: Sidhani kama hata ataambulia kura za chini kabisa zinazotakiwa ili kuingia kwenye uchaguzi!

Radwa El-Shami alihoji sababu zilizo nyuma ya idadi kubwa ya wagombea wanaoutaka Urais nchini Misri:

Idadi inaongezeka na nimeanza kujiuliza kwa makini dhamira na nia za kila mtu anayetaka kupanda kwenye kiti cha enzi cha Misri. Inaonekana zaidi kana kwamba siwezi kuitumikia nchi yangu bila kushika nafsi za juu za utawala, bila ya kuwa rais. Ninakiri kwamba ninahoji pia wale wenye uchu wa madaraka na sifa binafsi.
Ninahoji kwa nini Bw. Shafiq anagombea urais (wakati kiasi cha wa-Misri milioni 10 kati ya milioni 45 wenye sifa na haki ya kupiga kura walimkataa kama waziri mkuu!); kwa nini Dk. Amr Khaled anafikiria kugombea urais (bado haijathibitishwa); Jema gani Sheikh Hassan anafikiria kuwa itaifanyia Misri kama rais (kuna uvumi kuwa naye anawania urais); kwa nini Bw. Martada Mansour anajidhania kuwa anaweza kuwa rais (je atatutawala kwa vitisho na kupayuka?); kwa nini Bi. Bothaina Kamel anataka kuwa rais (ni harakati za usawa wa mwanawake?); kwa nini wapo watu wanamshawishi Bw. Naguib Sawiris kuwa sehemu ya harakati za uraisi (habari kutoka hapa na pale, lakini yeye mwenyewe alisema Baradei ni mtu anayempenda); na ninauliza pia ni upi msimamo wa Dk. AlBaradei baada ya umma kukubali mabadiliko yenye kilema ya katiba ambapo yeye aligoma kuwa rais?

Halafu Radwa aliendelea:

Sijui kama mimi ni mtu pekee ninayeikatia tamaa hali hii na kuiona kama kituko, na hii ndiyo sababu ninaandika. Ninapazia sauti kuguswa kwangu kwa sababu ninahitaji uhakikisho. Ninaomba maoni yenye weledi na ujuzi; Ninatafuta mtu atakayeongea kwa mantiki.

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu tunazowaletea kuhusu Mapinduzi ya Misri ya Mwaka 2011..

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.