Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011.
Picha zilizotafutwa na kuwekwa kwenye twita zinaweza kuleta mambo ya kushangaza.
Tafuta herufi hizi “宮城” (Miyagi) na picha chache zitatokea kutoka kwenye wilaya hiyo, moja ya maeneno yaliyoharibiwa sana nchini Japani baada ya tsunami. Nenda chini, na picha moja inaonekana, yenye rangi ya kahawia na bluu mpaka utakapoibofya…
…kuonyesha nchi iliyoharibiwa. Hii ndiyo sehemu ya iliyobaki yaKesennuma, mji mdogo, wakati fulani uliwahi kuwa na makumi ya maelfu ya wakazi.
Soma maelezo ya picha, na habari inatokea ya mtu aliyewahi kuishi katika mji. Mtu huyu aliituma picha kwa rafikiCherie, anayeishi Sydney, aliyeituma picha hiyo kwa barua pepe kwa njia ya mtandao wa intaneti. Ujumbe unasomeka:
なんとか家族みな無事でいます。家は半分なくなりました
家の前の風景で家も駅も商店街も何にも無くなりました…
宮城県気仙沼市の被害をネットで配信したいのですが、私には出来ません 助けが必要です。出来るだけ色んな国へ知らせたいと思います。このメールも電波が入る所まで車でやっときて打ってます。これから生き残った人達が生きるために少しでも援助お願いします
Cherie anaongeza maneno machache mwisho wa maelezo yake:
Ninawapenda, tafadhali msipoteze matumaini. Tunaweza kuonana tena, tunawaombea.