Udhibiti Nchini Singapore

Katika kipindi cha mwezi hivi, mamlaka za Singapore zimesababisha kelele kubwa baada ya kupiga marufuku filamu ya aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa na kumkamata mtunzi Mwingereza wa kitabu kilichoandiaka kuhusu adhabu ya kifo nchini humo.

Picha hii imechukuliwa kutoka kwa The Online Citizen

Mnamo Julai 12 mwaka 2010, Mamlaka ya Maendeleo ya Vyombo vya Habari ilitangaza uamuzi wake wa kuipiga marufuku filamu (kuanzia Julai 14, 2010) inayomuonyesha Dr Lim Hock Siew akizungumza hadharani juu ya uzoefu wake wa kuwa kizuizini chini ya Sheria ya Usalama wa Ndani. Filamu ilitengenezwa chini ya uongozi wa Martyn See. Bw. See alitakiwa kuondoa filamu hiyo kwenye YouTube. Unaweza kusoma maelezo ya filamu hiyo hapa.

Mwanablogu wa Singapore, Lucky Tan ametaka ukweli kusemwa wazi:

Kimsingi kinachosemwa na MICA ni kwamba wameipiga marufuku filamu hiyo kwa kuwa wanataka ukweli pekee ndio usemwe lakini filamu hii imejaa mambo mengi ya uongo, ulaghai na kupindishwa. Dr Lim Hock Siew alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa miaka 20 bila kifikishwa mahakamani. Katika kipindi hicho serikali ya PAP ilikuwa na wakati wa kutosha kuonesha ushahidi na kusema ukweli ili kwamba wote tuweze kushuhudia kazi nzuri iliyofanywa na ISD katika kutukinga na maovu. Bado tunangoja.

Picha hii imechukuliwa kwa Jacob Geroge

Mnamo Julai 18, mwandishi Muingereza Alan Shadrake alikamatwa na polisi wa Singapore akiwa hotelini kwa tuhuma za “jinai ya kuharibu sifa” siku moja baada ya kitabu chake cha, “Once a Jolly Hangman”: Haki Kwenye Gati Nchini Singapore, ambacho kilikosoa mfumo wa mahakama wa Singapore kilipozinduliwa. Kitabu hicho kiliondolewa kwenye maduka makubwa ya vitabu nchini Singapore.

Alishikiliwa kwa siku mbili ambapo Shirika la Haki za Binadamu la Kimataifa Amnesty International na Wanahabari Wasiokuwa na Mipaka walitaka aachiwe.

Blogu ya masuala ya kijamii-na-ya-kisiasa ya Singapore, The Online Citizen ilijiuliza kwa nini Bw. Shadrake alituhumiwa kwa tuhuma hizo za jinai ya kuharibu sifa:

Kitabu cha Alan Shadrake “Once a Jolly Hangman” ni simulizi inayokosesha raha. Kitabu hiki kinaweza kuwa kiliwakosesha raha baadhi ya watawala kiasi cha kuwalazimu kumkamata Mr Shadrake kwa kutumia sheria mabayo inatumika kwa nadra sana ya jinai ya kuharibu sifa.

Blogu ya kiSingapore, Chemical Generation Singapore, iliandika:

Kwa kumatwa kwa Shadrake, suala zima limekuwa siyo la kuhusu adhabu ya kifo, na badala yake limehusu zaidi juu ya wapi msaada kutoka nje ya nchi unapokoma kuingilia kati. Kuwadhibiti wanasiasa wa ndani wanaopokea pesa toka nje ya nchi hilo sina tatizo nalo. Lakini hili la kumdhibiti mgeni wakati wa uzinduzi wa kitabu chake ni sawa na uchokozi wa kitoo kabisa kwa Oliver Fricker, pengine umezidi kipimo katika kitabu changu. Labda tu kama kuna zaidi ya yale tunayoyaona

Mwanaharakati wa kisiasa, Chee Siok Chin ameishutumu serikali kuu ya nchi hiyo kwa kuwa na ‘siri chafu ‘:

Sasa, ni utawala gani wa kiimla utakaotaka siri zake zianikwe hadharani na kijitabu?
Vile vile hata kwa hotuba Dr. Lim Hock Siew iliyowekwa na Martyn See kwenye Youtube. Bila shaka Martyn ilimbidi kukubaliana na matakwa ya MDA ambayo iliamtaka kuiondoa hotuba hiyo. Hata baada ya yote, Dr. Lim alizungumzia kuhusu kitendo cha ukiukwaji wa sheria kilichofanywa na ISD cha kumuweka kizuizini kwa miaka 19.
Tena, ni serikari gani kandamizi ambayo itataka ukweli usemwe juu ya jinsi ilivyo kiasi cha kuzuia urushwaji wa video ambayo mtu yoyote anaweza kuipata?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.