Levant: Wanablogu wa Mashariki ya Kati Wanajipasha Moto kwa Ajili ya Kombe la Dunia 2010

Kombe la Dunia litaanza katika kama wiki tatu hivi na wanablogu katika mashariki ya kati tayari wameshaanza kutumia vibodi na kamera zao kujaribu kunasa shauku inayoizingira dunia mara moja kila miaka minne.

Timu za Taifa za Syria na Lebanoni hazijawahi kufuzu kuingia katika fainali za kombe la Dunia, hata hivyo hilo haliwazuii watu kutokuwa mashabiki wakali na kuonyesha upenzi wao kwa timu wanazozipenda katika kila njia inayowezekana. Wakati mwanablogu wa KiLebanoni Rami wablogu ya +961 aliridhika na mambo fulani ya homa hii ya mpira wa miguu, hajavutiwa na baadhi ya yale wananchi wenzake wanayoyafanya. Anasema:

Watu wanakusanya vijibendera kwa ajili ya magari na viambaza vyao, inaweza kuonekana kama vile ni ujinga lakini ni jambo poa kwani litawafanya watu wepukane na mijadala ya siasa.

Bado, ni jambo la kusikitisha pale unaponunua bendera ambayo ni zaidi ya mita 1 kwa upana au urefu! Nina uhakika ungeweza kutumia pesa hizo kwa matumizi mazuri zaidi!

Picha kwa hisani ya blogu ya +961

Kutoka Syria, Nasdaq Nasdaq kwa upande mwingine alikuwa amezama katika kuchambua sababu tofauti za watu kuwa nyuma ya timu fulani, anapendekeza dini kuwa mojawapo ya sababu [ar]:

تطالعنا الأخبار كل فترة حول إسلام احد اللاعبين بالتالي زيادة شهرته في العالم الإسلامي وتوجه الناس  لتشجيعه وتشجيع فريقه وحمل صوره و و و فقط لأنه أصبح مسلماً و لذا تشجعه .
Kila mara tunasikia kuwa kuna mchezaji amekuwa Muislamu na hivyo kumfanya awe nyota katika dunia ya Waislamu, ambako watu huanza kumshangilia yeye na timu yake kwa amkundi na kubeba picha zake, n.k. kutokana tu na kwamba amekuwa Muislamu na kutokana na jambo hilo tu.

Anaendela kutoa maoni juu ya “nguvu au uwezo” wa vijana wa Syria ambao hawawezi kumudu kulipia idhaa za televisheni za bei ghali ambao husimbua misimbo ya idhaa hizo na kuangalia mapambano bure badala yake:

طبعا لا احد يشك بقدرة الشباب السوري على تجاوز كل المعيقات التي تظهر أمامه – عدا المعيقات الرسمية –  للوصول إلى أهدافه ، منذ أن كانت مجموعة محطات ART بأوج قوتها قام بعض الشباب باختراق شيفرة الترميز  للبطاقات، ومع دخول الجزيرة الرياضية وغيرها تحركت مواهب الشباب وأصبح لدينا جيش من خبراء فك التشفير  الذين لم يدرسوا في الجامعات ولم يقرأوا كتب في هذا المجال ، وربما تغلبوا على مهندسين في كسر الشيفرات الصعبة ومشاهدة قنوات رياضية مشفرة ومجانا .
Bila ya shaka hakuna mwenye mashaka juu ya uwezo wa vijana wa Syria katika kushinda vikwazo vyote ambavyo viko kwenye njia yao, ukiachilia mbali vile vya kiserikali, ili kutimiza malengo yao. Tangu idhaa za IRT ziliposhika kasi baadhi ya jamaa waliweza kuvunja misimbo ya kadi zao na wakati idhaa ya michezo ya Aljazeera ilipozinduliwa tulikuwa na jeshi la wataalamu wa kusimbua ambao hawakusomea kwenye vyuo vikuu au kujifunza kwenye vitabu, nap engine wana uwezo mkubwa zaidi ya wahandisi katika kusimbua misimbo na kuangalia idhaa za michezo za kulipia bila kulipa.

Lolitto anatoa maoni kwa kusema kuwa anaishangilia timu ya Italia na jibu likaja haraka kutoka kwa Nasdaq:

Wewe ni msichana kwa hiyo ni jambo la kawaida kwamba unaishangilia Italia. Wakati nyanya yangu alipokuwa kijana, naye pia aliishabikia timu ya Italia na walikuwa ni vijana wanaovutia zaidi kuliko hawa wa sasa kwa mujibu wa bibi.

Na blogu ya Independence '05 , kutoka Lebanoni, inachapisha picha zaidi za “kiwanda cha bendera” ambacho kinashamiri kutokana na kombe la dunia:

Bendera zinauzwa mjini Beirut – kwa hisani ya Independence '05

Kwa hisani ya Independence '05

Na kama walivyo wengine, anasisitizia kidogo juu ya sababu za kujieleza kulikopita kiasi kwa shauku ya kombe la dunia, lakini anafikia hitimisho sawa sawa na lile:

Matokeo? Ni FURAHA, FURAHA, FURAHA.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.