Namna 10 Ambazo Warusi na Wa-Ukraine Walivyopokea Hotuba ya Putin Kuichukua Crimea

Machi 18, 2014, siku mbili baada ya wa-Crimea kupga kura ya maoni kuamua kujiunga na Shirikisho la Urusi, Rais Vladimir Putin alitoa hotuba [ru]  akitangaza kuwa ameipokea Crimea na mji wa bandari ya Sevastopol kuwa wanachama wapya wa shirikisho hilo. Mpaka wakati tangazo hilo linatolewa, haikuwa wazi ikiwa Urusi itarekebisha mipaka ya nchi hiyo mara moja, au itawaacha wanachama ao wapya kuwa huru kama zilivyo Abkhazia, South Ossetia, au Transnistria.

Pamoja na namna yoyote ambayo mtu anaweza kujisikia kuhusu suala la Crimea, hotuba hiyo ilikuwa ya kihistoria, na ambayo wanablogu waliiipokea kama kawaida ya mijadala ya mtandaoni. Hapa ni baadhi ya mijadala hiyo:

1. 

Putin as Tony Stark. The caption reads "Got Crimea back." Anonymous image found online.

Putin akifananishwa na Tony Stark. Maelezo yanasomeka “Nimeirudisha Crimea.” Picha isiyojulikana aliyeiweka mtandaoni.

Warusi wengi waliipokea kwa furaha. Zaidi ya yote, hata kwa mujibu wa kura za maoni za upinzani  [ru] wengi wanaunga mkono “kutwaliwa kwa mara nyingine” kwa eneo hilo.

2. 

Anonymous image found online.

Picha isiyojulikana imewekwa mtandaoni na nani.

Kwa wengine, hisia zilikuwa mchanganyiko. Ikiwa Putin “ameiiba” Crimea, je bado litakuwa jambo jema? Labda ni mtindo mpya, kama mchezo wa video.

3.

-"Must not sleep, must not sleep" -"Zzzzzz" Anonymous image found online.

-“Hakuna kulala, hakuna kulala”
-“Zzzzzz”
Picha isiyojulikana imewekwa mtandaoni na nani.

Ungeweza kumtegemea Waziri Mkuu Dmitry Medvedev kuweka mambo katika hali ya utulivu na angalau kutoa maelezo. Kulala kwake wakati wa shughuli za hadharani imekuwa kawaida katika miezi ya hivi karibuni ambapo Urusi inatengeneza sera.

4.

Anonymous image found online.

Picha isiyojulikana imewekwa mtandaoni na nani.

“Kuanzia leo ninaachana na bidhaa za kimarekani maishani mwangu. Marafiki, niungeni mkono!” alitwiti Mikhail Dvorkovich, mfanyabiahsra wa Kirusi na kaka wa mshauri wa Medvedev, ikiwa ni majibu kwa tishio la Marekani kuweka vikwazo[Ripoti ya Global Voices] dhidi ya maafisa wa Urusi. Watu wengi walijadili ujasiri wa kutwiti kwa kutumia simu ya iPhone, na, kwa hakika, kwa kutumia huduma iliyoanzishwa marekani ili kuwafikia aliotaka wasikie anachosema.

5.

President Obama dressed in an FSB (Federal Security Bureau) uniform. Anonymous image found online.

Rais Obama akiwa amevalia magwanda ya Idara ya Usalama wa Taifa la Urusi. Picha isiyojulikana imewekwa mtandaoni na nani.

Baadhi ya wanablogu wa ki-Rusi wanaonekana kuviangalia vikwazo dhaifu vya Marekani kama dalili ya kuunga mkono kimyakimya matendo ya Rais Putin. Huenda ndio sababu ya picha yake hii nyeti ya kutengeneza ikimwonyesha akiwa katika magwanda ya Idara ya Usalama wa Taifa la Urusi. “Asante sana comrade Obama!”

6.

Users of the public Facebook group "This is Kiev" are making their displeasure known. Collage from kievtypical.

Watumiaji wa kundi wazi la mtandao wa Facebook liitwalo “Hii ndiyo Kiev, mwana” [“This is Kiev, baby”] wamesikitishwa na hatua hiyo. Mchanganyiko wa picha za kiev [ru].

Kwa upande mwingine, Waukraine wanaonekana kusikitishwa sana na hotuba ya Rais Putin. Mwitikio kama huu unaonekana kuonyesha hisia hizo.

7. 

Nazis

Kushoto: “Hitler atangaza kutwaliwa kwa ustria kuwa sehemu ya Ujerumani” Kulia: “Putin atangaza kutwaliwa kwa Crimea kuwa sehemu ya bunge la Urusi.” “Zijue tofauti 10.” Picha isiyojulikana imewekwa mtandaoni na nani.

Kulinganisha hatua hiyo na ile ya kundi la Nazi imekuwa kawaida ya mijadala ya kishabiki baina ya Warusi na Waukraine kwa miezi kadhaa sasa, na sasa, hali haijabadilika.

8.

Anonymous image found online.

Picha isiyojulikana imewekwa mtandaoni na nani.

 Na hata tendo la hisani lakufananishwa na kundi la Nazi, kama hilo linawezekana.

 9. 

"Crimea, Summer of 2014" Anonymous image found online.

“Crimea, Majira ya joto ya 2014″ Picha isiyojulikana imewekwa mtandaoni na nani.

Picha ya kijana wa Caucasia Kaskazini akicheza kwenye mitaa ya Urusi. “Kama hutakuwa mwangalifu, Crimea,” anasema aliyeipiga picha hiyo, “mtageuka kundi la wachache wanaonyanyasika Urusi!” Haya ndiyo mategemeo ya wote wanaoshutumu hatua hiyo inayolinganishwa na ile ya U-Nazi.
10. 

G8 logo. Russian flag has been replaced with the Ukrainian one, on the lower left. Anonymous image found online.

Nembo ya G8. Bendera ya Ukraine imechukua nafasi ya ile ya Urusi, kushoto chini. Picha isiyojulikana imewekwa mtandaoni na nani.

Baadhi ya Waukraine wamebaki na matumaini kuwa Marekani na Umoja wa Ulaya watachukua hatua madhubuti kumwadhibu Putin na Urusi yake. Na kama Shirikisho la Urusi litatimuliwa kwenye kundi la G8 mwaka huu, nani achukue nafasi hiyo mwingine zaidi ya Ukraine?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.