Maelfu ya Wavenezuela wanaoishi ng'ambo wameandaa maandamano kuwaunga mkono wenzao wanaoandamana mitaani katika nchi yao ya Bara la Amerika ya Kusini. Picha ya mikusanyiko hiyo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Kwenye ukurasa wa Facebook uitwao SOS Venezuela [es] picha nyingi zinakusanywa, ambazo pia zinachapishwa kwa alama habari ya #iamyourvoicevenezuela #SOSVenezuela na #PrayForVenezuela kwenye mtandao wa Twita na Instagram.
Mi primo @guidorinconc me envió esta foto de venezolanos y extranjeros manifestando hoy en Malta. #SOSVenezuelapic.twitter.com/Fji1a1WzMC
— Rita (@RitaFinol) February 17, 2014
Mpwa wangu amenitumia picha hii ya Wavenezuela na wageni wanaoandamana leo mjini Malta.
Baadhi ya Wavenezuela ng'ambo walitumia fursa ya maandamano hayo kupeleka nyaraka kwa mashirika ya kimataifa au mabunge ya nchi hizo wanakoishi. Hivi ndivyo walivyofanya raia walioandamana mjini The Hague.
Venezolanos en La Haya, Holanda. Presentamos documento a Parlamento. Denunciamos violaciones a DDHH en #Venezuela pic.twitter.com/7j3OLpLUC4
— Tomás A. Chang Pico (@TomasChang) February 18, 2014
Wavenezuela jijini The Hague, Uholanzi. Tulipeleka nyaraka kwenye Bunge. Tulilaani vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu nchini Venezuela
Gaby Silva aliweka video kwneye mtandao wa Instagram [es] inayoonyesha maandamano yaliyofanywa na kikundi cha Wavenezuela jijini Madrid. Video hiyo inawaonyesha wananchi hao wakitoa mwito wa haki, amani na majadiliano.
Gazeti la TalCual [es] lilisambaza picha ya waandamanaji kwneye viwanja vya Times Square jijini New York.
PROTESTAN EN NUEVA YORK. Cientos de venezolanos protestaron en Times Square. http://t.co/ukrjIAueK3 pic.twitter.com/uwmkICODa0
— TalCualDigital.com (@DiarioTalCual) February 18, 2014
MAANDAMANO JIJINI NEW YORK. Mamia ya Wavenezuela waliandamana kwenye viwanja vya Times Square.
Kulikuwa na maandamano pia nchini Australia:
Venezolanos en Sídney se solidarizan con las marchas de estudiantes http://t.co/NF4OaoGKh9 pic.twitter.com/PzFwR4D4vT
— La Voz (@EldiarioLaVoz) February 18, 2014
Wavenezuela jijini Sydney walionyesha mshikamano wao kuunga mkono maandamano ya wanafunzi
Wakati huo huo, nchini Venezuela kiongozi wa upinzani Leopoldo López alitekeleza ahadi yake kwa kujisalimisha mwenyewe kwa mamlaka za serikali na Rais Nicolás Maduro alitangaza kwamba atakabiliwa na mashitaka ya uchochezi na “kutokuelewa Katiba”.
1 maoni