Mbinu za Kugundua Dawa Bandia katika Nchi Zinazoendelea

Kulingana na Shirika la Afya Duniani(World Helath Organization-WHO), dawa bandia zinapatikana kote duniani. Huwa zina michanganyiko ya viungo vyenye sumu na vingine visivyosaidia.Watu 700,000 hufa kila mwaka kwa kutumia dawa bandia za malaria na saratani pekee.  Shririka hilo la Afya linaendeleza kusema katika ripoti yake kuwa, mapato kutoka kwa dawa hizi kila mwaka hukaribia  dola bilioni 200.

Mbinu tofauti zinatafutwa za kusaidia kukumbana na janga hili katika nchi hizi zinazoendelea.

Ubunifu wa kiteknolojia

Ashifi Gogo wa Ghana, ni mjasiriamali ambaye amezindua ubunifu wa kutumia simu za mkononi. Ubunifu huu unahusisha kuweka maandiko yanayokwaruzika katika dawa, maandiko haya yana nambari ya utambuzi, ambayo mtu anatuma kwa kupitia huduma ya ujumbe mfupi ili kuhakikisha kuwa dawa hiyo ni halali.

Katika mazungumzo yake katika TEDx Boston, Gogo anaeleza namna ubunifu wake unavyotumika kwa kuunganisha simu, jamii, serikali na kampuni zinazohusika na dawa.

Baada ya suala la Duo-Cotexcin Kenya, Holley-Cotec kampuni ambayo inatengeneza dawa hizi, walizindua  teknolojia ambayo haiwezi kuchezewa.James Nyikal, mkurugenzi wa huduma za afya, Kenya  anaeleza :

Pakiti mpya za dawa hii, zitakuwa na mhuri wa utambuzi na alama nyingine ili kuonyesha kuwa dawa hizi ni halali.

"Is this drug real or counterfeit? SMS text with Pharma Secure to find out." Image by Wayan Vota on Flickr (CC BY-NC-SA 2.0)
“Dawa hii ni bandia au halali? Tuma ujumbe mfupi kwa Pharma Secure ili uweze kujua.” Picha kwa hisani ya Wayan Vota kupitia kwa Flickr (CC BY-NC-SA 2.0)

Rajendrani Mukhopadhyay anatueleza mbinu za sasa za kusaidia kufahamu dawa bandia. Atueleza hekaya za kusisimua:

Uchunguzi wa kwanza ni kukagua pakiti. Makaguzi wanakagua kwa makini pakiti hizo, ili wapate hakikisho kuwa kuna nia ya kudanganya mteja.’ Kwa wakati mwingine utakuta kuwa tembe hizo, hata kama hazina viungo vinavyofanya kazi, huwa ni makosa ambayo hayakutarajiwa katika kampuni. Pakiti zingine, katika dawa hizi huwa ni za kuchekesha sana. Kuna moja, ambayo ilikuwa iharibike kabla siku yake ya kutengenezwa, na papo hapo tukajua kuwa hiyo haikuwa dawa halali.

Pia anataja matatizo ya kufanya uchunguzi kwa mandhari yasiyofaa:

Changamoto katika nchi hizi ni kuwa lazima wakaguzi watumie njia ambazo zina ubunifu mkubwa, uangalizi wa kiteknolojia, usio na gharama kubwa lakini ambao ni madhubuti. Michael Green wa shirika la Marekani la kudhibiti na kuzuia magonjwa, anasema kuwa dawa hizi bandia kutoka Uchina, huwa zina madini ya chaki (calcium carbonate). Kwa sababu dawa halali huwa haina madini hayo, basi inakuwa rahisi  kwao kutambua dawa hizi bandia kwa kuongeza siku kwenye vipande vidogo vya dawa.

 

Tatizo linaloendelea

La muhimu hata kuliko athari za ki-fedha, dawa hizi zinaleta shida kubwa katika suala la afya kote duniani. Ukiachilia mbali suala la kuhatarisha maisha ya wagonjwa, dawa hizi zinateka imani ya watu kwa madaktari na mifumo ya afya.

Chati hii, kutoka kwa taasisi ya usalama wa madawa inaonyesha sehemu ambazo kulikuwa na visa vya dawa hizi. Suala hili liaendelea kuwa nzito kwa nchi hizi zinazojiendeleza kwa sababu ya kuongezeka kwa dawa hizi na miundombinu inayotakikana.

 

Total counterfeit drug incidents by year. Graph by PSI (available in public domain).
Visa vya dawa bandia. Grafu ya PSI (wazi kwa wote). 

PSI wanadokeza kuwa:

Sio lazima, sehemu zenye visa vingi kuwa hazina wakaguzi. Badala yake, nchi katika maeneo haya zinatafuta njia za kupunguza dawa hizi kwa kutumia kanuni na ukaguzi kwa kupitia wakala wa kuangalia madawa.

Hata tukizingatia ubunifu huu tuliozungumzia hapo awali, kugundua dawa hizi ni jambo gumu, ambalo linahitaji teknolojia za kisasa na uwezo wa kuhakikisha kuwa maagizo ya kitaifa yanafuatwa.

Kwa mfano, dawa nyingi za kukinga malaria zilipatikana katika nchi hizi, [fr] mwaka huu lakini baada ya wagonjwa kuzitumia. Mwaka wa 2012, uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuwa  theluthi ya dawa za Malaria  Asia ya Kusini Mashariki na Sahara ndogo ya Afrika zilikuwa na dosari katika uangalizi wa viungo au pakiti au zilikuwa za uongo.  Mwaka wa 2007, idara ya afya Kenya iliwatahadharisha wananchi kuhusu dawa za malaria za Duo-Cotecxin ambazo zilikuwa zinauzwa sana Nairobi na jinsi ya kuzitambua.

Lawrence Evans, ni mtafiti aliyefanya utafiti wa ubora wa dawa hizi za kuzuia malaria, Guyana na Suriname anasema:

Zaidi ya madawa ambayo hayajapigwa marufuku na Shirika la AFya Duniani ya kukinga malaria, urahisi wa kutengeneza dawa hizi pia ni hatari kubwa kwa maisha ya wagonjwa.

Prisca akiwa Madagascar anaeleza [fr] sababu zinazowafanya watu kukataa kununua dawa katika maduka ya dawa na badala yake kuzinunua kwenye maduka ya kawaida:

 des personnes n'hésitent plus à revendre des produits pharmaceutiques sans ordonnance. Selon Fara, propriétaire d'un commerce prospère ” Les médicaments que nous vendons sont les mêmes qu'en pharmacie, puisque je les achète chez un grossiste agréé. Mais comme je n'ai pas autant de charges qu'une pharmacie, ils sont deux fois moins chers “. Le problème des consommateurs est donc le prix.

Maduka mengi siku hizi zinauza dawa bila ushauri wa daktari. Fara, mwenye duka moja kama hili anasema: “Dawa ninazouza ni sawa na zile katika maduka ya dawa kwa kuwa nazinunua kutoka kwa msambazaji mwenye kibali. Bei yangu ya kuuziwa ni ndogo kuliko ya duka la dawa hivyo basi, naweza kuuza dawa kwa bei nafuu. Kwa wanunuzi, hapa kivutio kwa wateja wa dawa ni bei”

Hata kama ni muhimu kugundua mzunguko wa dawa hizi bandia ili kuzuia kuenezwa, nchi nyingi zinaonelea kuwa suala hili haliwezi kupatiwa uzito kama ubunifu kwa sekta nyingine na pia kupigana na magonjwa. Henry Neondo, anaandika katika Habari za Kisayansi za Afrika lazima Kenya ipigane na malaria kwa njia mwafaka zaidi na pia kutafuta kinga.

Kenya ni miongoni mwa nchi tisa za Afrika zilizochaguliwa kunufaika na mfuko wa mabilioni ya kutafuta kinga ya malaria.” Dawa na kinga mpya za malaria zinahitajika kwa dharura barani Afrika, ambako malaria haitibiki kwa kutumia zile dawa za kawaida. Hata kama dawa na kinga mpya zinaendelea kuzinduliwa, kuna haja ya kujenga uwezo wa Afrika wa kufanya majaribio ya hospitalini ya dawa hizi katika karne ijayo,” alisema profesa Binka, mkurugenzi wa Indepth Network.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.