Kenya: Habari za Mlipuko Jijini Nairobi Zatawala Mijadala ya Twita

Mlipuko unaodhaniwa kuwa ni bomu umesababisha madhara katika moja ya barabara kuu za Nairobi, Moi avenue, katika mji mkuu huo wa Kenya mchana wa Jumatatu. Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba mlipuko huo ulitokana na hitilafu ya umeme kwenye eneo hilo. Kamishna wa polisi wa nchi hiyo amekanusha tetesi kwamba mlipuko huo umetokana na shambulio la bomu linalohusishwa na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab.

Kenya imekumbwa na mfululizo wa mabomu tangu majeshi ya nchi hiyo yaingie Somalia kupambana na kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab kwa kile kiichoitwa “Operesheni Linda Nchi”.

Kwenye mtandao wa twita, watumiaji wamekuwa wakijadili tukio hilo na kubadilishana taarifa kupitia alama ya #NairobiBlast na #MoiAvenueBlast.

Eneo la mlipuko jijini Nairobi. Picha imewekwa kwenye mtandao wa twitpic na @JoeWMuchiri

Tafadhali kaa mbali:

@__RamzZy__: Kama wewe si mwandishi wa habari, kama huna shughuli inayokulazimu kuwa karibu na eneo la tukio, kaa mbali. Waache polisi na timu za uokoaji kufanya kazi zao. #MoiAvenueBlast

@cobbo3: Ni hatari kwa watu kukusanyika kwenye mtaa wa Moi na Kimathi baada ya mlipuko huo. Ikiwa mlipuko huo ni shambulio la kigaidi, mara nyingi bomu la pili laweza kulipuka kuangamiza maelfu

Wajibu wa vyombo vya habari:

@jaydab: @mckenziecnn, tunasubiri kuona na kusikia mtakachosema kuhusu mlipuko huu. Tujuzeni hali ilivyo na sio kutia chumvi.

@CyrusNjoroge: Vyombo vya habari vya kiraia vilipotua mjini, sote tumekuwa “wataalam”. Wala hatujisumbui kusubiri kusikia ukweli wa mambo.#Nairobiblast

@saddiqueshaban: Ninatarajia kwa dhati baraza la habari @MediaCouncilK linafuatilia kwa makini yanayofanywa na vyombo vya habari kipindi hiki wanaporipoti tukio hili #nairobiblast. Uwajibikaji ni kitu cha lazima

@Kevin2Tek: Alama inayotumika kujadili tukio la mlipuko huo, #NairobiBlast, sasa inatawala gumzo la mtandao wa twita duniani kote. Tafadhali kuwa makini na kile unachotuma kwenye mtandao huo, usisambaze hofu au kujadili uongo!

Nini kimesababisha mlipuko?:

@iAMneshynsky: watu wasikimbilie kufanya mahitimisho na kuhisi ni shambulio la al shabaab…chochote kinawezekana katika tukio hilo #NairobiBlast

@careywinnie: Mungu wangu, ninadhani maafiki zangu wapenzi wa filamu wako salama na wote wanaoishi maeneo hayo!!#NairobiBlast #moiavenue wtf happened?

@jowac50: RT #NairobiBlast RT #NairobiBlast Mkuu wa Polisi Mathew Iteere anasema mlipuko ulisababishwa na hitilafu ya umeme –kwa mujibu wa taarifa mbalimbali

@Fionaakumu: Maneno “mabomu” na “milipuko” yanaihitaji kuangaliwa upya. Tangu lini maneno haya yakawa na maana inayofanana? #MoiAvenueBlast

Kuokuwajibika kwa serikali:

@tonybkaranja: Tunahitaji sana mpango wa kudhibiti majanga ambao hautakuwa tu kwenye makaratasi #nairobiblast

@MisterAlbie: Kwa mara nyingine tabia yetu ya kutokuwa na ufahamu sahihi na maandalizi dhidi ya matukio kama haya yanatugharimu #Firehydrants #MoiAvenueBlast

@TeamKonshens1: Inaonyesha namna mwitikio wa vikosi vya Dharura ulivyo duni! Inaonekana kama filamu kwenye runinga! #NairobiBlast

@iCabway: #MoiAvenueBlast tukio hili linatukumbusha ulazima wa kuwa na mfumo unaoaminika wa maji yakuzimia moto katika kizazi hiki chenye matatizo. Miji ya ki-Afrika haina habari na umuhimu wa kuchukua tahadhari.

Wizi katikati ya Janga::

@iAMneshynsky:Wezi wanafanya kile wanachoweza kwenye mtaa wa Moi Avenue #NairobiBlast

@rmunene: Wa-Kenya wanasomba viatu na nguo kutoka kwenye maduka ya eneo la tukio. #nairobiBlast #KTNLiveStream

Udhaifu wa kiutendaji wa Polisi:

@ArybaStacks: Sijui kwa nini polisi bado wanaruhusu watu kwenda eneo la tukio…itakuwaje kama kuna mlipuko mwingine?#MoiAvenueBlast

@Mwanikih: Polisi wanafanya hali hii ambayo tayari ni mbaya kuwa mbaya zaidi kwa kutumia nguvu kuwatawanya watu. Sasa hivi watu wanapiga kelele “Mlikuwa wapi?” #NairobiBlast

Jeshi la Polisi la Kenya limesema kwamba watu wapatao 27 wamejeruhiwa na mlipuko huo na wanaendelea na matibabu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.