Zimbambwe: Hasira wakati Mzee Mugabe Anapowania Uchaguzi wa 2012

Mtawala wa muda mrefu wa Zimbambwe, Robert Mugabe, 87, alipitishwa mwishoni mwa wiki iliyopita na chama chake cha ZANU –PF, kuwa mgombea wao kwa uchaguzi wa rais unaotegemewa kufanyika mwaka ujao.

Mugabe amekuwa madarakani tangu mwaka 1980. Amegoma kuitikia miito kutoka ndani na nje ya nchi yake iliyomtaka ang’atuke. Wa-Zimbabwe wengi walitarajia kuwa huenda kuzorota kwa afya yake pamoja na umri wake mkubwa kungemlazimu kuachia madaraka. Mkutano mkuu wa ZANU-PF uliyeyusha matarajio hayo yote. Kama uchaguzi utafanyika mwakani, Mugabe atakuwa na umri wa miaka 88 na atakuwa Mwafrika wa pili mzee zaidi kugombea katika uchaguzi wa rais, wa kwanza alikuwa Kamuzu Hastings Banda wa Malawi aliyekuwa na umri wa miaka 98 wakati aliposimama kugombea kwenye uchaguzi wa mwaka 1994 nchini Malawi.

Twita na Facebook, nyenzo mbili mbadala za mtandaoni ambazo zimekuwa majukwaa muhimu yanayopendwa na wa-Zimbabwe, zilikuwa mahali pa kuonyesha hasira na kutokuamini kilichotokea.

Mtumiaji wa Facebook Wise Chokuda aliandika:

Robert Mugabe atakuwa mzee wa pili wa Kiafrika kusimama kugombea urais. Picha imetolewa na serikali ya Marekani.

Rais Komredi Robert Mugabe hatastaafu katika siku za hivi karibuni kufuatia majimbo yote kumteua kuwa mgombea wao katika uchaguzi wa mwaka ujao. Haya yalitangazwa wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa 12 wa ZANU PF mjini Bulawayo jana.

Masamha Tulisticated aliweka kwenye ukurasa wake wa facebook:

hakuna mipango ya Rais wa Zimbabwe kustaafu. Mashamba zaidi ya wazungu yatatolewa kwa ajili ya uhamiaji vijijini. #Zanu PF congress.

Kwenye Twita, @BrendahNyakudya alituma ujumbe unaomnukuu Mugabe:

Nina bahati sana kwamba Mungu amenipa miaka mingi kuliko mtu mwingine yeyote ya kuwa nanyi (wa-Zambabwe). Sitawaangusha,” aliongeza (Mugabe). #FML

@BrendahNyakudya aliendelea kusema:

Mugabe anasema itakuwa ni kosa kung’atuka” *Brendah anajimwagia majivu kichwani, anavaa nguo ya gunia akiomboleza usiku kucha katika milango ya jiji*

@masamhat: Robert Mugabe anasema hana mpango wowote wa kustaafu. Anamshukuru Mungu kwa kumpa maisha marefu kwa sababu anaweza sasa kutawala zaidi ##Zanu PF congress in Byo [Bulawayo]

@mashanubian: “Si ajabu! Mkutano mkuu wa ZANU PF umemteua #Mugabe kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi utakaofanyika mwaka 2012 au mapema 2013 #zimbabwe

@clivembayimbayi alituma ujumbe huu wenye hasira:

Jamani niambieni, ni lini huyu mpumbavu ataachia madaraka, Ninamaanisha Mugabe kuichia Zimbabwe, jamani hebu tufanye kitu

@nqabamatshazi aliongeza utani kidogo akidokeza kitu tofauti kidogo katika nchi ambayo raia wake wamejifunza kulilaani giza kwa sababu ya umeme kukatika mara kwa mara:

Wakazi wa katikati ya Jiji la Bulawayo wanafurahia maisha sasa hivi. Tangu mkutano wa ZANU PF umeanza [Desemba], hawajakumbana na kero ya kukatika kwa umeme.

Baadae, siku moja baada ya mkutano wa ZANU PF kumalizika, @nqabamatshazi alifuatilia zaidi hali ya umeme jijini ilivyo mjini Bulawayo:

Baada ya mapumziko yasiyo ya kawaida, sasa kero ya kukatika-katika umeme imerudi tena jijini Bulawayo utafikiri ni kulipiza… nina hakika watu wanatamani ule mkutano wa ZANU PF ungeendelea.

Wakati huo huo, @IamClaro alifanya marejeo kwenye tangazo lenye utata la Nando ambalo dunia nzima wanalicheka:

Ha ha ha ahaaa NANDO (Hoteli) wamebadili tangazo lililokuwa linasomeka “last DICTATOR standing” (DIKTETA wa mwisho aliyebaki) na kuwa “LAST STICKTATOR standing”! :-Kumlinda Mugabe asiuawe”

Tangazo hilo lililosababisha utata linamwonyesha Robert Mugabe akila peke yake wakati wa sikukuu ya Noel katika jumba kubwa wakati huo huo akikumbukia “nyakati za raha” alizowahi kuwa nazo na madikteta wa zamani, kama vile kucheza mchezo wa kurushiana maji na Muammar Gaddafi kwa kutumia mpira, akitengeneza midoli ya malaika kwenye mchanga akiwa na Saddam Hussein, akiimba muziki wa Karaoke akiwa na Mao Sedong, akimsukuma P.W Botha kwenye bembea, na akiendesha pipa na Idi Amin.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.