Tetemeko kubwa kuwahi kutokea nchini Japani

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011.

Photo from March 11 earthquake in Japan shared by @mitsu_1024

Picha kutoka Machi 11 iliyotumwa na @mitsu_1024 (kupitia wikitree.co.kr)

Siku ya Ijumaa, Machi 11, 2011 saa 8:46:23 mchana saa za Japani, tetemeko lenye vipimo vya tetemeko 8.9 liliikumba Japani, lilikiwa kubwa kuwahi kuripotiwa katika historia ya Japani.

Zifuatazo ni nyenzo zilizo kwenye mtandao ambazo watu wanazitumia ili kuwasiliana na wenzao:

Alama za twita zinazotumiwa na watumiaji wa twita nchini Japani ni #sendai na #jishin. #prayforjapan inatumiwa kutuma maombi kwa lugha ya kiingereza katika mtandao wa Twita.

Watu wengi katika Twita wanajaribu kutulia na kutumiana ushauri, hasa kuhusiana na uzoefu uliotokana na tetemeko Kuu la Hanshin ama lile la Chuetsu.

@asahi_chousa:

【拡散希望】電気屋さんからの忠告!です。 ただ今地震で停電している地帯の方はブレーカーを全て落として下さい。通電されたら小さなブレーカーを一つづつ入れて下さい。漏電ブレーカーが落ちるようでしたら、無理に入れず、電気事業者等に連絡をとって下さい。漏電による火災を防ぎましょう。

Tafadhali RT! (Tuma tena ujumbe huu wa Twita!)Ushauri kutoka kwa mafundi wa umeme: Tafadhali zima kifaa cha kukatia mkondo wa umeme kama uko kwenye eneo lililokatiwa umeme. Umeme unaporudi, washa moja baada ya nyingine kwa kutumia vifaa vidogo vya kukatia mkondo wa umeme. Kama mkondo mdogo utaendelea, usiulazimishe, jaribu kuwasiliana na duka lolote la vifaa vya umeme kwa msaada zaidi. Jaribu kujihadhari na moto unaosababishwa na kuvuja kwa umeme.

@take23asn:

@take23asn 【タンスの下敷きになった人を助ける方法】タンスが頑丈なのは全面と上部、側面だけ。背の面は薄い板でできている。その薄い板を蹴破り、そこからすべての引き出しを抜き取る。そうすれば簡単にタンスを解体できる。

@take23asn “Namna gani unaweza kuwasaidia watu waliokandamizwa ndani ya makabati: Kuta za makabati ambazo ni ngumu kwa mbele, juu na kiupande upande. Nyuma imetengenezwa na ubao mwembamba. Piga kwa nguvu kwa kutumia mguu na vunja ubao mwembamba ili uweze kuvuta nje droo zote na kulitawanya kabati kirahisi.

@Grpa_Horiuch:

【 緊急 】 手話が必要な方に教えて上げてください。「目で聴くテレビ」でNHKのニュースに手話をつけて放送中。このURLから「緊急災害放送」をクリックしてください。 http://t.co/KQPhc1r #jishin #NHK

[Haraka sana] Tafadhali inua mkono wako kwa wale mnaohitaji mfasiri wa lugha za ishara. Bofya kiungo kifuatacho http://t.co/KQPhc1r na pitia habari za NHK “Matangazo ya Luninga ya Sikiliza kwa macho yako.”

@hibijun:

FMわぃわぃは多言語で地震・災害情報を放送中。インターネットでも聴けます。http://bit.ly/eaV16I%20 在日外国人の皆さんに伝えてください。 #saigai#eqjp #earthquake

Chaneli ya lugha mbalimbali ya FM wai-wai (simulradio) wanatangaza taarifa kuhusu tetemeko la ardhi na janga. Unaweza kusikiliza kupitia mtandao wa intaneti hapa http://bit.ly/eaV16I%20 Tafadhali fikisha ujumbe kwa wageni waishiio Japani

@kuilne

iPhoneの電池を少しでも長持ちさせる方法。
1.wifiを切る
2.位置情報サービスを切る
3.通知サービスを切る
4.Bluetoothを切る
5.画面の明るさを一番暗くする
6.余計なアプリを切る

Okoa betri ya iPhone 1) ondoa wifi 2) ondoa GPS 3) ondoa kitoa taarifa 4) Ondoa mfumo wa Bluetooth 5) Punguza mwangaza 6) Zima mipangilio ya zaida.

@Tranquil_Dragon wa Sendai, wa wilaya ya Miyagi alituma picha hii:

@wanchan11 aliweka picha ya mafuriko ya bandari ya Sendai:

Baadhi ya video kutoka Tokyo:

Shukrani nyingi kwa Timu ya GV Japan kwa kuwa pamoja wakati wa tetemeko waliohusika na maandalizi ya makala hii.

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.