Indonesia: Sony yamkabili Sony

Mwezi uliopita, Sony Arianto Kurniawan au Sony AK kutoka Mega Kuningan, Jakarta nchini Indonesia alitishiwa kushitakiwa kwa kukiuka sheria za matumiza ya nembo na shirika la Sony la Japan kama hatafunga tovuti yake binafsi yenye jina www.sony-ak.com.

Tushukuru kuwa, Sony mtu alikuwa akisaidiwa na jumuiya ya mtandaoni na shirika la Sony hatimaye liliona kuwa ni ujinga kufungua kesi. Shirika la Sony likaamua kuondoa mashtaka na limeshaomba msamaha kwa mwanablogu huyo.

Tovuti hiyo binafsi ya Sony AK ilianzishwa mwaka 2003 na imekwisha zawadiwa kama tovuti bora zaidi ya kuelimisha kwa mwaka 2003, 2004 na 2006 na Gazeti la PC la Indonesia.

Multibrand ililijuza shirika la Sony kwamba tovuti ya Sony AK hutoa bure taarifa kwa jamii na haiuzi kitu chochote.

Kwa maoni yangu binafsi, Shirika la Sony lilitoa madai hayo kwa kujiamini mno, kwa sababu kinga inayotolewa wakati wa usajili wa nembo huwa inahusu aina fulani tu ya bidhaa iliyo chini ya nembo husika.

Katika hili, Shirika la Sony ni mzalishaji bidhaa za elektroniki, wakati tovuti ya: www.sony-ak.com ni tovuti binafsi tu ya aina yake inayotoa maarifa bure kabisa.

talking points imesaidia kuongeza umaarufu wa tovuti hii ya Sony AK kwa miaka sita iliyopita.

Mashtaka hayo yamewaudhi waIndonesia mtandaoni hasa wale ambao wakuwa wakiblogu na waliokuwa katika tekinoloia ya habari kwa miaka kadhaa. Tovuti ya Sony AK imekuwa ikijulikana kuwa ni kituo cha kushirikishana elimu kwa wadau wa teknologia ya habari nchini Indonesia na imekuwa ikifanya hivyo kwa takribani miaka 6.

Jambo hili limeibua mjadala mzito katika uwanja wa kublogu wa Indonesia na watumiaji facebook wanaoiali Sony AK – ‘Sony — usinyang’anye jina la rafiki yangu’ – kwa haraka imevuta maelfu ya watu.

Tovuti ya Sony AK

Tovuti ya Sony AK

Blogu ya Whispurr inasema kuwa kuna waIndonesia wengi wanaoitwa Sony

Na kwa taarifa yako, kuna maelfu ya watu hapa Indonesia wanaoitwa Sony. Ninao marafiki wanaoitwa Sony, mchezaji nyota wa Badminton wa indonesia ni SONY DWI KUNCORO, na mwingine ni mwigizaji maarufu wa Indonesia SONY TULUNG.

Sasa kwanini SHIRIKA LA SONY lisiwashitaki hao na maelfu ya akina mama wanaowaita watoto wao SONY.

Na finally woken anajiuliza je kampuni Apple itamshitaki mwanadada mwigizaji Gwyneth Paltrow kwa kumwita bintie Apple

Nadhani kampuni ya Apple imshitaki Gwyneth Paltrow kwa kumpa bintie jina Apple na kwa kuwa binti huyo anaweza baadae kufungua Blogu nakuuita Apple pia…

Hakika hii ni zaidi ya ujinga.

Colson anaelezea hili kama pambano kati ya Daudi and Goliati

Wakumhurumia zaidi hapa ni Daudi (AK) katika vita yake dhidi ya Goliati (shirika). Kumshitaki raia mwema kwasababu tu anatumia jina ambalo kwa umbali ni sawa tu na lile litumikalo na kampuni kubwa ya kimataifa, kwa kweli ni kituko

Nafikiri bado Goliath yuko sahihi hapa – kwasababu mfumo wa sheria kwa kiasi kikubwa upo kwa matakwa ya Goliati. Na kwa sababu ya nguvu ya kisheria Goliati ana uwezo wa kupanga matokeo mara nyingi zaidi kuliko Daudi kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha alionao.

Kabla ya kuondolewa kwa kesi mahakamani , wana blogu walikuwa wanapanga kuanzisha mgomo wa kutonunua bidhaa za shirika la Sony. Yari NK anafurahia uamuzi wa shirika hilo wa kuifuta kesi.

Ni busara kwa shirika la Sony kufuta shutma, kwa sababu haina maana kwa namna yeyote ile kumtaka mtu kuacha kutumia jina la blogu yake binafsi isiyokuwa ya kibiashara

Kwa kitendo chake cha kufuta kesi, Sony haitakumbwa na athari hasi ambazo zingetokana na muonekano wake kwa jamii ya waindonesia, ambao ungeweza kufikia kwenye mgomo wa kutonunua bidhaa zakekwa wale wanoipenda blogu ya Sony AK kwasababu wanajua kuwa Sony AK alikuwa na malengo mazuri tu alipoanzisha blogu yake na si kwa lengo la kuliingilia shirika la Sony…

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.