Pakistani: Vitendo vya Unyanyasaji Watoto Vyaongezeka

Kuna ongezeko linalokera la vitendo vya unyanyasaji watoto nchini Pakistani. Kwa mujibu wa afisa wa Shirika la UNICEF anayefanya kazi nchini humo, Shamshad Qureshi, sababu zinazotajwa ni pamoja na kukosekana kwa udhibiti wa kutosha wa sheria inayohusika, upuuzaji unaofanywa na wazazi na ukosefu wa uelewa miongoni mwa watoto na jamii kwa ujumla. Alieleza pia kwamba sababu kubwa ya kuwepo kwa vitendo vya kuwaingilia kimwili na kuwanajisi watoto nchini humo inatokana na uwezekano wa watu kuwa karibu na watoto kutokana na upuuzwaji unaofanywa na wazazi.

Faheem Haider kupitia blogu ya Bangladesh Foreign Policy anajadili kuhusu vitendo vya unyanyasaji watoto na watoto wanaotumikishwa katika nchi za Pakistani na Bangladeshi. Wala haumi maneno yake anapotuonyesha upande mwingine wa pili wa vitendo hivi:

“Baada ya kushindwa kuhudumia familia inayokua, katika kutapatapa, baadhi ya wazazi huwatoa watoto wao ili waende kufanya kazi za ndani katika familia zenye uwezo, yaani wanafanya kazi za ndani au zile za uyaya (yaani walea watoto ndio jambo la maana ambalo kwalo watoto hawa huajiriwa kuwa katika kaya hizo). Hatimaye watoto hawa hugeuka kuwa jalala la kila kitu na mara nyingi hutendewa kama moja ya mali binafsi zilizo pale nyumbani. Wazazi halisi hawapo, mara nyingi wapo mamia ya maili huko, wakiwa hawana habari kwamba watoto wao wanapitia mambo mengi sana magumu kutokana na tabia na mienendo ya waajiri wao wasio na shukrani.

Watoto hawa wanakuwa wamenyang'anywa haki yao. Wao ni kama bidhaa zinazotokana na umaskini usiotulia na zawadi zilizofungwa upya za mazingira ambayo hayadhibitiki. Hawana fursa; matokeo yanakuwa hayana alama wala miisho isiyoeleweka ambayo pengine inakuwa ikiwasubiri na bado wao hawana habari nayo. Kwa watoto hawa haki ni kama mwalimu asiyesikiliza.”

Siyo tu kwamba Fatima Bhutto ni mrithi mwenye ushawishi katika ulimwengu wa siasa bali pia ni mtetezi wa utu. Katika makala yake kwenye blogu inayoitwa The Daily Beast wala haachi neno pasipo kulisema na hivyo kutengeneza taswira halisi ya vitendo vya unyanyasaji watoto:

“Mauaji ya kinyama yaliyofanywa dhidi ya mfanyakazi wa ndani mwenye umri wa miaka 12, anayesaidikiwa kuuwawa na mwajiri wake mwenye nafasi kubwa, yameuacha umma wa nchi hii mdomo wazi. Lakini kwa sababu ya kuwa na serikali inayonuka ufisadi mpaka heshima ya kuua kulikofanywa na mwanamke tajiri, daima wale wenye uwezo katika nchi hii huwa hawaguswi.

Shazia Masih, msichana mwenye umri wa miaka 12 na mwenye umbo dogo kuliko umri wake, alizikwa juma lililopita katika mazishi ya Kikristo yaliyofanyika katika Kanisa Kuu la Lahore. Binti huyu alikuwa ameajiriwa na mtu tajiri na mwenye uwezo mkubwa aliyewahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria, na binti huyu alichokuwa akilipwa ni dola 8 tu kwa mwezi huku baadhi ya majukumu yake yakiwa ni kusafisha choo, magari yaliyokuwa ayakiegeshwa hapo katika nyumba iliyo pembezoni kidogo mwa mji, pamoja na kuondoa taka zote katika nyumba hiyo ya ghorofa.”

Video hii ya YouTube inamwonyesha mwalimu mmoja katika shule ya serikali aliyemfanyia vitendo vya unyanyasaji mwanafunzi mmoja kama adhabu, lakini hakuna mtu aliyemchukulia hatua yoyote.

Msemo ‘Unyanyasaji watoto’ hutumika kueleza vitendo vya aina mbalimbali vilivyo jinai na vinavyofanywa dhidi ya watoto. Vitendo hivyo hudhihirisha maumivu ya kimwili na yale ya kiakili. Mtu mzima anapojaribu kumtumia mtoto kama mdoli wake wa ngono, hiyo ni unyanyasaji watoto. Pale mtu mzima anapojaribu kumtumikisha mtoto kwa fedha kiduchu, huo ni unyanyasaji watoto. Pale mtoto anapogeuzwa kuwa bidhaa na kuuzwa kwa mabadilishano ya fedha au makubaliano mengine, huo ni unyanyasaji watoto. Pale mtu mzima anapomfanya mtoto afanye kazi kupita kiasi pasipo kujali hali yake ya kiafya na kanuni za afya, huo ni unyanyasaji watoto.

Pakistani ni moja ya nchi ambazo hazifanyi juhudi kwa kiwango kinachotakiwa katika kulinda watoto dhidi ya maovu mengi ambayo wanaweza kufanyiwa katika mazingira mbalimbali ya utafutaji.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.