Moroko: Wafanyakazi wa Shirika la Misaada La Kikristu Wafukuzwa

Wakiwaaga  baadhi ya watoto yatima (picha kutoka katika tovuti rasmi ya Kijiji cha Matumaini)

Wakiawaaga baadhi ya watoto yatima (picha kutoka katika tovuti rasmi ya Kijiji cha Matumaini)


Wiki iliyopita, wafanyakazi 20 wa Kijiji cha Matumaini, makazi madogo ya yatima katika mji mdogo wa Moroko vijijini, waliondolewa (walifukuzwa) nchini bila onyo, kwa madai ya kuhubiri dini. Kijiji hichi kimekuwepo kwa miaka kumi iliyopita, na ina wafanyakazi wengi zaidi wa Kikristu kutoka nchi za Magharibi.

Wafanyakazi hao wanadai kuwa siku zote wamekuwa wawazi kwa malaka za moroko kuhusu Ukristu wao, na hapajatokea tatizo lolote. Kwa wengi wa watoto hao, makazi hayo ya yatima ndiyo nyumba pekee ambayo wanaijua.

Tovuti rasmi ya Kijiji cha Matumaini kina tamko, ambalo limekubalika na wafanyakazi wote ambao walitakiwa kuondoka nchini humo, ambalo linasomeka:

Siku ya Jumatatu tarehe 8 Machi, wafanyakazi wote 16 kutoka nje ya nchi, wakiwemo wazazi 10, na watoto 13 waliozaliwa nchini humo, waliambiwa kuwa wataondolewa kutoka katika eneo na nchi hiyo. Sababu iliyotolewa ni kuwa wazazi hao walikuwa wanahubiri dini, bila ya ufafanuzi ni nani, na katika wakati gani, wapi na vipi madai yanayodaiwa yalitukia. Hakuna madai yanayohusu ustawi na uangalizi wa watoto ambayo yametolewa kama jambo la kutia hofu na mamlaka za Moroko katika historia ya miaka 10 ya VOH.

Mamlaka za Moroko hazijatoa ushahidi wowote wa madai na wametoa masaa machache tu kwa wazazi hao kufunga virago vyao na kuwaeleza watoto wao kuwa pengine hawataonana nao tena.

Vyombo vichache vya habari vimeidaka habari hiyo (Shirika la Habari la Moroko [FR] ni mojawapo), lakini wanablogu kadhaa wenye uhusiano binafsi na Kijiji hicho wameanza kusambaza habari kuhusu mkasa huo, wengine wakiwa na matumaini ya kuwarejesha wafanyakazi hao nchini Moroko. Mwanablogu Elizabeth Shelby, mfanyakazi Mkristu ambaye aliwahi kufanya kazi kwa kujitolea katika makazi hayo ya yatima huko siku za nyuma, ameitisha maombi kutoka kwenye jamii yake, lakini pia anatumaini kupata maelezo kutoka kwa serikali juu ya kwa nini kuetokea mabadiliko ya ghafla katika mioyo yao. Anaandika:

Ni zaidi ya masaa 24 tangu wafanyakazi 20 (wengi wao wakiwa ni wazazi) katika Kijiji cha Matumaini walipohamishwa kutoka kwa watoto wao, bila ya kutarajiwa na maofisa wa Moroko. Walipewa dakika thelathini kupakia vitu vyao na kuondoka nchini, bila ya uhakika wa kuwaona tena watoto wao wa Kimoroko. Kijiji cha Matumaini kimekuwa na maridhiano na kimefanya kazi na serikali kwa miaka 10, na kimekuwa na matatizo machache. Kuanzia tarehe 4 Januari, Moroko imekuwa na Waziri mpya wa Sheria, Mohammad Naciri, ambaye anahisi ni lazima atumie nguvu zake ili afunge Kijiji cha Matumaini kwa sababu anaamini “Wakristu wanawashawishi watu wabadili dini.”

Shelby pia anaongoza kampeni kwenye Twita, kwa kutumia alama ya #MoroccoOrphans na ameanzisha kikundi cha Facebook.

Mwanablogu wa The Moroccan Dispatches ameandika makala ya kina inayovinjari pande kadhaa za uamuzi huo wa serikali, na pia uendeshaji wa makazi hayo ya yatima. Kwa kuzingatia yote, mwanablogu huyo anaandika:

Kama ilivyoelezwa, ni vigumu kuelewa ni kipi kinachoruhusiwa na kipi kisicho nchini moroko kwani sheria za kwenye vitabu huwa hazimaanishi chochote (kimsingi). Kwa hiyo pengine, Mamlaka za moroko zilifumba jicho kwa miongo michache iliyopita kama vile wanavyofanya kwa pombe, hashish, biashara ya umalaya na uendeshaji wa kasi. Au pengine kiji cha matumaini kilifanya baadhi ya vitendo hivyo. Sijui.

Mwanablogu wa Kimarekani aliye nchini Moroko anaandika kukiunga mkono kijiji hicho:

[Wafanyakazi wa Kijiji] kwa kweli walifikiri kuwa wanafuata utaratibu, lakini walihojiwa na kufukuzwa nchini bila ya muda wa kufungasha na kusema kwa heri kwa watoto. Yatima wana maisha magumu katika nchi za Kiislamu, ambako, hata wakiasiliwa, hawana haki sawa na watoto wa kuzaliwa katika familia, na hata Waislamu wa moroko waliokuwa wanafanya kazi na watoto walifukuzwa kutoka kwenye sehemu hiyo, kwa hiyo hakuna sura yoyote inayofamika inayowaangalia watoto hao hivi sasa. Tafadhalini fanyeni maombi kwa watoto hao, kwa wale waliofukuzwa nchini, na kwa wale ambao wanaweza kufukuzwa. Ni hari ngumu, hasa kwa sababu Moroko imekuwa ikichukliwa kama taifa la wastani ambalo linahimiza uhusiano wa amani kati ya watu wa imani tofauti. Wawekeni watu wa nchi hii inayopendeza kwenye maombi yenu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.