Iraki: Ni Siku ya Uchaguzi Kwenye Twita

Maalum #iraq10 picha kutoka kituo cha kupiga kura #Baghdad: www.mict-international.org/1a.jpg

Maalum #iraq10 picha kutoka kituo cha kupiga kura #Baghdad: www.mict-international.org/1a.jpg


Ni siku ya uchaguzi nchini Iraki na ulimwengu wa Twita umekuwa uking’ong’a na habari mpya mpya tangu mapema asubuhi.

Ili kufanya jumbe za twita ziende na wakati, huduma maalum imeundwa katika @uchaguziwairaki ambako “waandishi 30 kutoka kote nchini Iraki wanatuma jumbe za twita kuripoti juu ya matukio ya uchaguzi kuanzia saa 4 asubuhi kama wanavyoshuhudia matukio hayo yanavyotokea.”

@uchaguziwairaki inawataka wasomaji:

Wafuatilie habari zetu za #uchaguziwairaki siku ya Jumapili, moja kwa moja hapa kwenye Twita. Waandishi 40 wa ki-Iraki watakuwa #wana-twita habari mpya za uchaguzi kama zinavyojiri.

Tangazo lingine linasema:

Tuko hai – tafsiri zipo njiani! Tufuatilie kwa ajili ya twita za moja kwa moja kuhusu #uchaguziwairaki kutokea ndani ya #Iraki. Jiunge na mjadala #iraq10

Habari mpya mpya kutoka kwa wasimamizi walioko nchini ni za aina sawa na zile za chaguzi nyingine duniani, isipokuwa Iraki ni kesi ya aina yake. Mabomu yalilipuka siku nzima na mapambano yaliripotiwa kati ya makundi mbalimbali yanayopingana.

Kaika @uchaguziwairaki, waandishi waliojaribu kutumia Twita walifanya kazi nzuri ya kutupasha habari kwa kutumia nyenzo za mitandao ya kijamii.

Katika habari moja mpya, Laith anaripoti:

Laith: Baghdad: Makumi ya familia kutoka eneo la AlKaradah walizuiliwa kupiga kura kwa sababu majina yao hayapo kwenye daftari ya wapiga kura.

Kutoka Sulaimaniya, Jamal anaandika:

#SULAIMANIYA, Jamal: Vituo vya kupiga kura vimefungwa. Vyombo vya habari haviruhusiwi kuingia na kufuatilia mahesabu ya kura. #iraq10

Kwingine katika ulimwengu wa Twita, @iawia1 anaeleza:

Leo hii Iraki inafanya uchaguzi wa kidemokrasia zaidi katika kanda hii. Natumaini 9demokrasia hiyo) itadumu& na kuwa mfano katika Mashariki ya Kati #iranelection #iraqelection #iraq

Mmarekani @jeffmeyerson ana matumaini:

Sherehekeni na wa-Iraki wanaopenda uhuru kwani leo wanaonyesha msimamo wao wa demokrasia. #Iraq

Naye Miguel Marquez, mwandishi wa habari wa ABC, anatoa muhtasari wa siku kwa kusema:

#Iraq elex: 38 wauwawa, 73 wajeruhiwa. Karibu milipuko 40. Na bado wa-Iraki walijitokeza kupiga kura. Inaonekana kuwa jumla ya kura itakuwa juu zaidi nje ya BGD

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.