Afrika Kusini: Ubaguzi wa Julius Malema

Wakati tabia za Rais Jacob Zuma zimekuwa zikizua mijadala mikali na yenye uhai katika ulimwengu wa blogu wa Afrika Kusini, hivi sasa ni mwanasiasa mwenye utata ambaye pia ni rais wa Umoja wa Vijana wa ANC, Julius Malema ambaye anatengeneza vichwa vya habari. Hivi karibuni, aliwaongoza wanafunzi katika kuimba wimbo wa zamani wa kupinga ubaguzi wa rangi unaoitwa Ua kaburu. Anakabiliwa na mashtaka ya jinai kwa wimbo huo.

Hebu tuangalie maoni kutoka kwa wanablogu wa Afrika Kusini.

Blogoff!!! Anaandika makala yenye kichwa “Pigeni risasi Makaburu, ni wabakaji!!!!”:

Julius Malema

Ni mtu mpumbavu, na wanafikiri kuwa mtoto wa ki-Pedi atakuwa rais wetu atakeyefuata. Nimo njiani kuhamia nchi nyingine ikiwa atakuwa amiri jeshi. Watu wanafikiri kuwa Zuma anatufanya tuonekane kama manyani; naam Julius atafanya vibaya zaidi ya mheshimiwa JZ… akiwa usingizini!!!

Aliimba wimbo wa zamani wa mapambano “Piga risasi Makaburu, ni wabakaji”! Ati nini! Ninupenda ukweli kuwa anaamini katika demokrasi, lakini anasambaza kauli za chuki!

Bw. Jackson Mthembu, msemaji wa ANC, ni dhahiri anamtetea, anasema kuwa halikuwa kosa lake na kwamba alinukuliwa, au lolote lile, nje ya muktadha. Naam ninafikiri Julius ni mpuuzi na asiyefahamu lolote na ni mbaguzi wa rangi, lakini tafadhali usininukuu nje ya muktadha. Hivyo sivyo ninavyomaanisha, hello!!

Rea kutoka katika blogu ya “My Life and World” anajadili uropokaji wa Malema katika makala yenye kichwa kinachosema, na labda niongezee sawa kabisa, “Weka mkasi chini Malema, kabla mtu hajakuchapa sawasawa!!!!

Wote tunafahamu kinachotokea pale unapokimbia na mkasi, sawa? Naam hivyo ndivyo hasa Malema anavyofanya hivi sasa, anakimbia kimbia kama vile mtoto mbaya asiye na fadhila ambaye hataki kumsikiliza mama yake. Wakati atakapoanguka na kujichoma jichoni marafiki zake watoto wote watamtelekeza na kukimbia wakimuacha anavuja damu kama nguruwe aliyenasa. Hawezi kumsikiliza mtu yoyote anayemwambia nini cha kufanya.

Hauwezi kuamini kuwa sisi ndio wenyeji wa Kombe la Dunia la Mpira wa Miguu la Fifa, kwa jinsi anavyotenda. Kama anafikiri kuwa wageni kutoka ng’ambo watakuja hapa na kuijanza nchi hii wakati inaonekana kana kwamba machafuko ndio jambo la kawaida hapa, basi yumo njiani kuamshwa kwa jambo baya.

Lakini matokeo ya miropoko ya Malema, ANC na Rais wa Afrika Kusini walikuwa wepesi kumtetea mmoja wa viongozi wao wakuu.

Blogu ya Common Dialogue inaandika “ ANC itaongea na Malema kuhusu kauli zake za kibaguzi? Hili ndilo lingekuwa la kwanza!”:

ANC inasema kuwa itakabiliana na rais wa Umoja wa Vijana Julius Malema kuhusu moja ya kauli zake za kiubaguzi wa rangi wakati wa maandamano ya wanafunzi. Kwa bahati kubwa! (jambo hilo linaweza kutokea)
Msemaji wa chama Ishmael Mnisi alisema: “Tunawasiliana na Umoja wa Vijana kila mara, tutaendelea kuongea nao… hata katika wakati huu tutaendelea kuwasiliana nao,” alisema.
Malema, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, aliwaongoza wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Johannersburg katika wimbo unaosema: “Piga risasi Makaburu [wakulima], ni wabakaji.”
Hivi sasa sote tunafahamu kuwa Malema amekuwa akiwatukana watu pamoja na wanachama wakongwe wa ANC na vyama wabia kadiri anavyopenda. Hakuna kilichomtokea.

Waafrika Kusini Weupe wachache asmbao ni wahafidhina wamejiunga na pambano la kwenye ulimwengu wa blogu na wanauonyesha unafiki. Wessel's Place ameweka yale yanayomkera kwenye blogu yake:

Wakati Julius malema alipokuwa akiimba “Piga risasi Makaburu” kwenye maandamano ya vijana wa ANC, wakulima walikuwa wanauwawa kwenye jimbo la Limpopo.

Na hakuna kiongozi yeyote mweusi wa siasa aliyesema lolote.

Naona hili ni jambo la kusikitisha. Ninaona kuna vipimo visivyo sawa kwa wote katika nchi hii. Kama mtu mweupe yeyote angetamka “Piga risasi Wazulu” au “Piga risasi Waxhosa”, wangepata sababu ya kuwa na hofu kwa maisha yao. Kwa hakika, wakati mtu mmoja alipoamua kuunyooshea kidole msafara wa rais, mtu yule alikamatwa na kunyanyaswa na wenye mamlaka.

Ninataka kuamini katika nchi hii. Ninataka kuamini katika uwezo wake. Ninataka kuamini kuwa watoto wangu wanaweza kukua bila ya kuomba msamaha kwa kuwa weupe.

Akiblogu kwenye blogu ya My Digital Life, The Source ameweka malalamiko marefu aliyoyapa kichwa cha “Wimbo wa Ua Kafir?”…

Kwa hiyo ANC inamtetea Julius malema kwa kuimba wimbo wenye maneno, “Pigeni risasi makaburu, ni wabakaji”.

Msemaji wa ANC Jackson Mthembu aliiambia Sapa kwa simu Alhamisi asubuhi kuwa atamtetea Malema na kwamba wimbo huo angaliwe katika mazingira ulipoimbwa (soma makala nzima).

Anaendelea kusema:

“Swala hili, kwa kweli, watu wengine wanaweza kuwa sahihi kwamba kuna nyimbo ambazo hazipaswi kuimbwa. Hebu waliweke (suala hili) kwenye ajenda na wawashawishi ANC kwamba tusiziimbe nyimbo hizo na watueleze kwa nini.

“Lakini pia waziangalie nyimbo zilizoimbwa na nguvu za ukandamizaji.”

Hebu tuliangalie tamko hili

Nguvu za ukandamizaji zinaweza kumaanisha serikali ya weupe katika zama za ubaguzi wa rangi na kwa hiyo zinaweza kumaanisha weupe wote.

Sasa nilikuwa katika shule ya lugha ya Afrikaans na pia nilikuwa kwenye kikundi cha Voortrekkers. Na kwa wale wasiofahamu, Voortrekkers ni sawa na chama cha maskauti, lakini wao wanasherehekea urithi wa taifa la Makaburu (Afrikaner) ambao walisafiri kutokea sehemu za pwani kuelekea ndani kwenye sehemu inayojulikana hivi sasa kama Freestate, Gauteng, Mpumalanga na Limpopo.

Alex Matthews katika blogu ya Thought Leader anauliza, “Kama kuua Makaburu ni sawa, vipi kuhusu weusi, wanawake na mashoga?”:

Msemaji wa ANC Jackson Mthembu ametetea toleo lisilo maarufu la wimbo huo wa “Ueni Makaburu, Ni wabakaji”, kama uilvyoimbwa na Julius Malema akidai (kwa mujibu wa makala ya Sapa) kwamba “ mmaneno yaw imbo huo yanukuliwa nje ya muktadha”.

“Wimbo huu uliimbwa kwa miaka mingi kabla Malema hajazaliwa. Julius hata hafahamu ni nani aliyeuandika wimbo huo. Aliupata jutoka kwetu [ANC]. Wapeni lawama ANC, msimlaumu Julius. Lakini wakati unapoilaumu ANC, basi wekeni mambo katika muktadha husika,” Sapa ilimnukuu Mthembu akisema.

Kwa mantiki ya Mthembu, inakubalika kabisa kuchochea watu waue watu wengine, ikiwa tu kuna “mazingira au hali inayoruhusu”. Je hiyo inamaanisha nini? Naam, kwa kuwa “Ueni watu weusi” ulikuwa wimbo wa zamani wa kibaguzi, wabaguzi wenye chuki wanaweza kuuimba kutokea juu ya mapaa ya nyumba. Kwa kuwa wimbo wa “Ueni wanawake” ulikuwa ni wimbo wa watu wanaopenda kuonea na kudharau wanawake, kwa hiyo wanaume weny kudharau wanawake wanaweza kutengeneza Macarena yaw imbo huo kwenye vilabu vya wanaume pekee. Kwa kuwa “Ueni mashoga” ulikuwa ni kibao kikubwa kwa wabaguzi wakati walipokuwa wanawachoma moto wasagaji, wanaweza kpayuka wimbo huo wakati wakiwatosa mashoga kwenye madaraja kwenda kwenye mashimo ya majitaka.

Matokeo yake, Malema ameomba msamaha, ambao tovuti ya ClassicMalema.co.za imeuchapisha katika makala ya “Malema asema Samahani”:

Ni jambo la nadra kwa mshenzi huyu kuomba msamaha kutokana na kauli zake. Nafikiri ANC walimshukia kwa nguvu zote. Je barabara ya Ju Ju inafikia mwisho wake?

Azad Essa katika tovuti ya Thought Leader amepandisha makala moja nzuri sana ya kejeli na utani inayoongelea mikataba ya ajabu ajabu ambayo Julius Malema amejikusanyia katika nafasi yake nzuri serikalini. “Nipatie Kilo mbili za Malema laini, tafadhali!”:

Wakati nchi imo kwenye hali ya kuchanganyikiwa na bei kupanda kwa ghafla pale “Malema laini” ilipofika kwa wauza magazeti, wanachama wa ngazi za juu wa ANC walikutana kwenye mkutano wa dharura siku ya Jumatatu ili wasuluhishe mgogoro mpya zaidi ndani ya chama.

Wakati taarifa kuwa za zabuni za serikali zinaongeza mishahara midogo ya maofisa wa serikali, familia zao na familia za familia zao, zinaokekana kuwa zimeongeza mauzo ya magazeti katika wikiendi, uongozi wa ANC ulitoa matamko rasmi katika jitihada zake za kung’oa rushwa.

Katika mabadiliko ya msimamo ya ghafla ANC ilitoa tamko mapema leo asubuhi linalosema kuwa ni haki ya kada mwandamizi kutojihusisha na mikataba ya serikali.

Na je, Google inafikiria nini juu ya Julius Malema?:

Kawa huu ndi mkataba. Fungua www.Google.com na andika “Julius Malema is” suburi sekunde moja au mbili ili uone mapendekezo ambayo Google inayatoa.

Inachekesha

Bila ya shaka, Zuma na Malema wataendelea kuwa mada moto katika ulimwengu wa blogu wa Afrika Kusini kwa muda mrefu ujao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.