Sudani: Je, Umoja Bado Ni Chaguo la Kimkakati

Akiandika kwa Kiarabu, mwanablogu wa Kisudani Ayman Hajj anajadili siasa za nchi yake na kwa nini watu wengi wa Sudani wanapoteza imani katika umoja.

Vitendo vya serikali ya Sudan na vile vya Chama Maarufu cha Sudani ya Kusini anasema mwanablogu huyu, vinaonekana kama vile mchezo wa kuigiza:

لماذا يظل الشعور متزايدا بأن الحكومة السودانية وشريكها في الحكم الحركة الشعبية لايقومان بشئ غير اداء مسرحية باهتة الملامح امام اعين الشعب السوداني.

Kwa nini hisia zinaongezeka kuwa serikali ya Sudani pamoja na mwenzi wake katika utawala, Chama Maarufu, hawafanyi kitu kingine zaidi ya kuigiza mchezo ambao ni wa kizembe, mbele ya macho ya watu wa Sudani?

Uigizaji wa namna hii, anaandika Hajj, unauweka umoja wa Sudani katika sehemu nyeti:

الشئ الذي لم اعد اشك فيه أن الاثنين شبه متفقين علي تقسيم السودان بحدوده الحالية الي دولتين ولايعدو الحديث عن جعل الوحدة خيارا جاذبا مجرد ذر للرماد في العيون فطيلة السنوات الماضية لم يقم احد منهما بعمل يقودنا الي ذلك فقط يتخاصمون ويتصالحون ويقوم البعض منهم بالشتم والسب والبعض الاخر بالتهدئة والمغازلة وتكون المحصلة الاخيرة ان لاشئ يجعلنا نؤمن بأنهما يحاولون ايجاد شئ ما يجعل الوحدة امرا جاذبا.

Jambo ambalo sina mashaka nalo ni kuwa hawa wawili wapo karibu na kukubaliana kuigawa Sudani vipande viwili katika mipaka iliyopo sasa. Kuongelea umoja kama chaguo linalovutia ni jambo la utupu. Katika miaka yote iliyopita, hakuna aliyekubali kufuatilia kitendo chochote ambacho kingepelekea kwenye hilo – umoja. Wamekuwa wakipigana na kupatana. Mooja wao humlaani na kumtukana mwingine na mwingine hujaribu kutuliza mgogoro na kuendelea na taratibu za kutongozana. Matokeo ya mwisho ni kuwa hakuna lolote wanalolifanya ambalo linatufanya tuamini kuwa wanajaribu kuunda kitu fulani ambacho kitaufanya umoja kuwa ni chaguo la kuvutia.

Akinukuu maendeleo ya hivi karibuni, mwanablogu huyu anaandika:

اخيرا الاسبوع الماضي تخرج الحركة الشعبية في مسيرة يتم قمعها بواسطة الحكومة ويعتقل فيها بعض القادة الذين يصرحون علي اجهزة الاعلام بأن الحكومة دكتاتورية وقمعية وينسون انهم شركاء اصيلين فيها، ثم تأني الحكومة لتعلن بأنها اتفقت مع شريكها علي مجموعة من القوانين الداعمة لأتفاقية السلام والخيار الديمقراطي ثم يتصافحون وتطبع الحركة قبلة علي خد شريكها وكأن شئ لم يحدث.

Hatimaye, Chama maarufu wiki iliyopita kiliandaa maandamano ambayo yalikandamizwa na serikali. Baadhi ya viongozi walikamatwa. Walikuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa wakitoa matamko kwenye televisheni wakisema kuwa serikali ni ya utawala wa kiimla wa kikandamizaji, huku wakiwa wamesahau kuwa wao wenyewe ni wenza wa asili wa serikali hii. Halafu serikali inageuka na kutangaza kuwa imekubaliana na wenzi wao juu ya sheria kadhaa zinazounga mkono makubaliano ya amani na chaguo la kidemokrasia. Halafu wanasalimiana kwa mikono na Chama Maarufu kinatia muhuri wa busu kwenye mashavu ya serikali kama vile hakuna kilichotokea.

Na kwa kuhitimisha anasema:

اخيرا بهذه الافاعيل يدفعون المواطن يوما بعد اخر بالكفر بالوحدة التي هي في الحقيقة خيار استراتيجي بنسبة له لما يصورونه له بعدم امكانية التعايش المشترك تحت مسميات الاختلافات العرقية والدينية والاقتصادية.

Na mwisho, ni vitendo hivyo ambavyo vinawalazimisha raia kupoteza imani katika umoja, ambao katika ukweli ni chaguo la kimkakati. Hawaamini tena katika hilo kwa sababu inaonyeshwa kuwa haiwezekani kuishi pamoja huku kukiwa na tofauti za kikabila, kidini na kiuchumi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.