Misri: Mauaji ya Kinyama ya Naga Hammady

Heshimu Dini, na Sarah Carr

Heshimu Dini, na Sarah Carr


Wakristu wa madhehebu ya Koptiki husherehekea Krismasi tarehe 7 Januari. Wakati wa mkesha wa sherehe hizo nchini Misri, waumini hueelekea makanisani na kusherehekea tukio hilo takatifu. Lakini mwaka huu tukio lisilotarajiwa lilitokea huko Naga Hammady, Misri ya Juu, ambapo mhalifu asiyejulikana alianza kupiga risasi hovyo hovyo kwenye umati watu baada ya watu hao kumaliza maombi wakiwa wanaelekea majumbani kwao.

Zeinobia aliandika makala mpya kuhusu mauaji hayo ya kinyama katika blogu yake akisema:

Nimesikitishwa sana na pia nimekasirika kwa kile kilichotokea Naj Hammadi jana. Inaniuma zaidi ya Wamisri Wakristu kwani kilichotokea ni dhidi ya Wamisri wote.

Rambirambi zangu ziwafikie familia za wale wote waliouwawa na kujeruhiwa katika shambulio hili linalochefua.

Mwanablogu mwingine, Coptic File, aliandika kuhusu tukio hilo:

تم إطلاق النار بشكل عشوائى من رَشاش آلى موَجه من داخل سيار (فيات – خضراء اللون)، مما أسفر عن استشهاد ثمانية أقباط وإصابة آخرين، وجميعهم ممن حَضروا قُداس عيد الميلاد بالكنيسة

Bunduki iliyorusha risasi ilitumika kutokea ndani ya gari (Fiat ya kijani), ili kuua hovyo hovyo watu wanane na kujeruhi wengine wengi. Wote walitoka kwenye watu walihudhuria maombi yaliyofanyika ndani ya kanisa wakati wa mkesha wa Krismasi.

Katika blogu ya Misr Digital, Wael Abbas pia aliweka video ya mauaji ya Naga Hammady kwenye blogu yake.

Wizara ya Mambo ya Ndani inasema kuwa shambulio hili lina uhusiano na tukio la zamani ambapo msichana wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 12 alibakwa na mwanaume wa Kikristu katika mji huo huo. Lakini Zeinobia haoni ni kwa jinsi gain tukio hilo linaweza kukubalika kama kisingizio cha mauaji. Pia anailaumu Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mkasa chote:

Na kwa heshima yangu yote huu ni ujinga wa ajabu, kupigana na uhalifu kwa makundi ya uhalifu. Nailaumu Wizara ya Mambo ya Ndani katika hili, kama kuna heshima ya kweli na hofu ya sheria pasingetokea kitu kama hiki.

Nawara, kadhalika, anashiriki hisia kama hizo. Kuhusu Taarifa ya Wizara ya mambo ya Ndani kwa vyombo vya babari juu mauaji, anasema:

اعجب بيان للداخلية قريته في حياتي، عمري ما شفت بيان للداخلية بيلقي اللوم على الضحية وبيحرض على العقاب الجماعي

Taarifa ya ajabu kupita yoyote niliwahi kuisoma katika maisha yangu yote, sijawahi kuona taarifa kwa vyombo vya habari inayowalaumu waathirika na kuhamasisha adhabu kwa umma mkubwa.

Nawara pia alivilaumu vyombo vya habari vya Misri:

الاعلام المصري الراكد مش جايب سيرة الموضوع كأن اللي اتقتلوا امبارح دولم خرفان

Vyombo vya habari vilivyolala vya Misri vinalipuuzia tukio hili, kama vile wale waliouwawa jana ni kondoo.

Mwanablogu The Cat of The Desert anailaumu jamii nzima na watu wenye siasa kali kwa yote yaliyotokea.

موت 7 مسيحيين كلهم شباب فى عمر الزهور واطفال غير الجرحى
سرقوا فرحتهم بالعيد وقتلوهم برصاص الإرهاب والغدر .. وقاعدين لحد يولولوا على شهيدة المرجيحة اللى اطلقوا عليها شهيدة الحجاب
مستنيين ايه ؟؟ بعد الانحطاط وقلة الادب على المختلف عقائديا مستنين سمعتكو تبقى ايه فى الخارج ؟؟
الله ينتقم من كل من افتى بتكفير الآخرين وعلى رأسهم القرضاوى والحيوانى وحسان

Wakristu saba vijana waliuwawa, na wengine wengi walijeruhiwa. Waliwapokonya maadhimisho na furaha yao ya Krismasi, na kuwaua kwa risasi zao. Na bado wanalia juu ya shahidi wa sea-saw, na wakamuita kama shahidi wa Hijab.
Mnasubiri nini baada ya ujinga wote huu, na kupumbaa? Mnatarajia wengine watufikirie vipi baada ya yote haya?
Shenzi wote wale wanaotaka kuwaita wengine makafiri, na zaidi ya akina Al Quaradawy, El Huwainy, pamoja na Hassaaan.

Kisha akatuma video ya Abu Is-haq El Huwainy inayowaonya watu juu ya njama za Wakristu na za kishetani zinazofanywa dhidi ya misri!

Mwanablogu wa Kimisri Te3ma, kwa upande mwingine, anaamini kuwa kuna watu wa nje walio nyuma ya matukio kama haya:

وأنا على يقين تام بأن الفتنة خارجية وليست داخلية

Nina uhakika kabisa kuwa watu walio nyuma ya mauaji haya ya kinyama wametoka nje, na hawatoki hapa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.