Georgia: Hebu Tuongelee Tendo la Ngono…


Pengine mada iliyotawala katika vyombo vya uanahabari wa kijamii vya Georgia haikuwa siasa, uchaguzi, matatizo, matetemeko ya ardhi au majanga. Badala yake, mada iliyojadiliwa sana ilikuwa inahusu kipindi kipya cha televisheni, Ghame Shorenastan. Kinachoonyeshwa kwenye Imedi TV, jina la kipindi hicho linatafsirika kama Usiku pamoja na Shorena na kinaongelea mada zinazohusu tendo la ngono.

Kwa kuwa ni wa kwanza kufanya hivyo, na msichana wa zamani wa Ki-Georgia wa Playboy, Shorena Begashvili, kipindi hicho kilipokea marejeo mengi katika wavuti, yote yale yaliyo hasi nay ale yaliyokuwa chanya. Mwanablogu NightGravity bila ya shaka alivutiwa.

გაქაჩავს. დარწმუნებული ვარ ბევრმა ცნობილმა თუ არა ცობილმა უყურა,ბევრმა კონსერვატმა და ა.შ.

kipindi hiki kitafanya kazi. Nina hakika watu wengi maarufu, wasio maarufu sana na wahafidhina pia walikiangalia.

Kila mtu alikubali kuwa Georgia inahitaji programu ya televisheni kuhusu ngono na mengi ya maoni hasi, kama ukosoaji huu uliofanywa na Lukrenc, yalikuwa yanahusu zaidi masuala ya kiufundi.

გადაცემას უდაოდ საინტერესო და სექსუალური წამყვანი ყავს–შორენა ბეგაშვილი,გადაცემის საინტერესოობაზე კი რა მოგახსენოთ მეგონა ტოპ 10 სიმღერას ვუსმენდი

Kipindi hiki, kina mtangazaji ambaye bila ubishi anavutia – Shorena Begashvili – lakini kipindi chenyewe hakivutii sana – nilidhani kuwa ninatazama “Kumi Bora za Video za Muziki”.

Mwanablogu mashuhuri wa Georgia Tomushka aliweka makala kdhaa kuhusu kipindi hicho na kuchambua kila onyesho. Pia alikosoa upande wa kiufundi.

Hakikuwa na mada kuu, na kilionekana kama programu ya MTV. Katika dakika 45 kulikuwa na dakika 20 za matangazo na dakika 20 za video za nyimbo za MTV:D dakika 5 za mwisho zilikuwa “Haloo, kwa heri, ngono si kitu kibaya, tendo la ngono ni zuri” :D

Lishtota aliitisha kura ya kwenye mtandao akiuliza “Ni lini kipindi cha “Usiku pamoja na Shorena” kitafutwa?”

[1. Mwezi mmoja au mapema zaidi (40%); 2. Miezi kadhaa (28%); hakitafutwa (31%)]

Mwanablogu mwingine, Giorgi Benashvili alishangazwa na kwamba watu hawakupinga vikali dhidi ya kipindi, hasa kwa vile waandishi na watengenezaji walitarajia kasheshe.

“Leo hii, katika mwaka wa 2009, kufundisha matendo ya ngono kupitia televisheni hakuna umuhimu tena – hili ni hitimisho ambalo limefikiwa kutokana na ukimya ambao ulikikaribisha kipindi na ambao haukutarajiwa nami au na waandishi wake. Kama kipindi hicho kingetengenezwa mwaka 2001, ninaweza kufikiria athari zake, tofauti na zile tulizoziona hivi sasa.”

Kwa kweli, kukosekana kwa maoni mabaya kunapelekea wengi kuamini kuwa jamii, au kwa uchache ile iliyo kwenye mtandao, ilikuwa tayari kwa ajili ya kipindi kama kile. Makala nyingi kwenye blogu na majukwaa zinalalamika kuwa kipindi kile hakikuwa kinaelimisha vilvyo, kama ambavyo moja ya maoni linavyolalamika.

გოგო კარგია უდაოდ. ყველაფერი ისე იყო როგორც ჩვენს ცხოვრებაში, გამომწვევი ფასადით შეფუთული ფრიგიდულობა. სექსი დარჩა ოცნებად :D :D

Kwa hakika msichana ni mzuri. Kila kitu [kipindi – D.] kilikuwa kama maisha yetu – ubaridi mgando uliofungwa kwenye karatasi ya kuvutia. Ngono ilibakia kama ndoto :D :D

Pengine kipindi kile kilitumaini kufanya mapinduzi katika ngono, lakini kilishindwa kwa sababu Georgia imekwishaweza kuhepa kutoka kwenye ile kasumba ya “hakuna ngono katika Muungano wa Jamhuri za Kisovieti (USSR).” Mada hii si mwiko tena na pengine mapinduzi ya ngono yamekwishatokea, hata kama ni ya hariri.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.