Twita Kutoka Beirut: Siku ya Pili ya Warsha ya Wanablogu wa Uarabuni


Siku ya pili ya Warsha ya Wanablogu wa Kiarabu ilianza na mada inayohusu Mtandao wa Herdict, tovuti inayotumia vyanzo vya watumiaji kukusanya taarifa za uchujaji wa habari kwenye intaneti kutoka kwa watumiaji duniani kote. Mshiriki wa warsha kutoka Qatar Muhammad Basheer alituma picha kutoka kwenye mada hiyo katika ujumbe wa Twita:

Muhammad Basheer atuma ujumbe wa twita kuhusu Herdict

Muhammad Basheer atuma ujumbe wa twita kuhusu Herdict

Baada ya mada ya kwanza, mwanablogu wa Kimisri Manal alijadili ulimnwengu wa wanateknolojia wa Kiarabu, hasa aligusia kuhusu wanateknolojia wa kike nchini Misri. Mlebanoni NightS aligusia haja ya wanawake wengi zaidi kwenye #ab09:

NightS awataka wanawake wengi zaidi wajihusishe na masuala ya kiteknolojia

NightS awataka wanawake wengi zaidi wajihusishe na masuala ya kiteknolojia

Baada ya mada yenye kufahamisha ya Manal, wanablogu walijigawa katika warsha za makundi , wakigusia mada mada mchanganyiko. Warsha moja, iliyoendeshwa na hamzoz, ilimakinikia kublogu kuotkea Iraq. Muhammad Basheer alihudhuria utoaji wa mada hiyo na alituma ujumbe wa Twita:

Muhammad basheer alihudhuria mada ya @hamzooz

Muhammad basheer alihudhuria mada ya @hamzooz

Mwakilishi wa Haki Miliki Huru Donatella Della Ratta pia alihudhuria na kutuma ujumbe wa Twita:

Donatella anaandika kuhusu mada ya @hamzooz

Donatella anaandika kuhusu mada ya @hamzooz

Mshiriki wa ki-Bahraini Amira Al Hussaini alihudhuria mada iliyotolewa na kiongozi wa mradi wa Sauti Zinazokua nchini Yemen. Ni wazi alivutiwa na warsha hiyo:

Amira Al Husseini avutiwa na idadi ya wanablogu wa Yemen

Amira Al Husseini avutiwa na idadi ya wanablogu wa Yemen

Mada kubwa ya mwishio kutolewa siku hiyo kwa mara nyingine tena pengine ilikuwa ya kuvutia zaidi. Anas Tawileh, mwanzilishi wa Meedan, aliwasilisha mada kuhusu mradi wa watumiaji wa kutafsiri Kiingereza-Kiarabu. Mwanablogu wa Iraq Salam Pax alizikamata hisia katika ujumbe huu wa Twita:

Salam Pax alivutiwa na mada ya Meedan

Salam Pax alivutiwa na mada ya Meedan

Tawileh alifungua mada yake kwa taarifa za kweli kadhaa kuhusu Intaneti pamoja na hii moja inayosema kuwa idadi ya masaa yanayotumiwa kwenye Facebook kwa mwaka, yakitafsiriwa katika masaa ya kazi za kujitolea, yangelkiweza kulijenga piramidi la Giza kwa siku 9. Amira Al Hussaini pia alishirikisha dondoo nyingine kutoka kwa Tawileh:

Amira Al Hussaini aandika ukweli unaofurahisha

Amira Al Hussaini aandika ukweli unaofurahisha

Akituma ujumbe wa Twita kuhusu dhana hiyo, mwandishi wa Ki-Moroko wa GV Hisham G. aliandika muhtasari wa Meedan kwa maneno machache:

Hisham G. anaongelea kuhusu dhana ya mtandao unaoweza kutafsirika

Hisham G. anaongelea kuhusu dhana ya 'mtandao unaoweza kutafsirika'

Na mwisho, Meedan yenyewe (ambayo iliandika kuhusu warsha hapa) ilieleza kwenye Twita kuwa watakuwa wanatafsiri twiti kutoka kwenye kongamano (ambazo zinaweza kupatikana kwenye alama #ab09)

Meedan itatafsiri twiti zote kutoka kwenye Warsha

Meedan itatafsiri twiti zote kutoka kwenye Warsha

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.