Namibia: Nafasi ya Vyombo Vipya vya Habari kwa Uchaguzi wa 2009

Uchaguzi wa rais na bunge la taifa la Namibia ulifanyika tarehe 27 na 28 Novemba 2009. Vyama vya kisiasa kumi na vinne vilishiriki uchaguzi. Chama tawala, SWAPO kinatarajiwa kushinda uchaguzi. Chama cha upinzani (RDP) ni mpinzani mkubwa wa Chama cha SWAPO.

Vyama vya siasa na mashirika yasiyo ya kiserikali yalitumia nyenzo kadhaa za habari za kijamii kupiga kampeni, kufuatilia na kuripoti Uchaguzi wa Namibia 2009.

Asasi ya Taifa ya Haki za Binadamu (NSHR) walitumia nyenzo ya Ushahidi kufuatilia uchaguzi. Ushahidi ni nyenzo ambayo ilitengenezwa baada ya Uchaguzi uliokosa maelewano wa Kenya mwaka 2007. Ushahidi ilikusanya taarifa za ushuhuda wa kuona za mapigano na kuziweka kwenye ramani.

NSHR walitumia Ushahidi kukusanya taarifa kuhusu udanganyifu, ushawishi usio haki, vitisho, matumizi ya nguvu na kadhalika. Taarifa zilitumwa kwa njia tatu: Ujumbe mfupi wa simu (SMS), barua pepe na kujaza fomu kwenye tovuti.

Matumizi ya nguvu kabla ya uchaguzi yaliripotiwa kwenye Ushahidi:

Jioni ya Ijumaa iliyopita kati ya saa 2 na saa 3 usiku kwenye Mtaa wa Eveline huko Goreangab sehemu ya Windhoek, mapigano yalianza kati ya wanachama 15 wa SWAPO na wanachama 7 wa RDP baada ya wale wa chama tawala huku wakimba “Sisi ni Askari wa Nujoma ” walipobandua bango la chama cha RDP kwenye nguzo ya umeme ya Manispaa. Wanachama wa Polisi wa Wanaheda waliwahi haraka kuingilia na hakuna tukio jingine lilitokea jioni hiyo.


Mradi wa Chaguzi za Afrika
hutumia nyenzo mpya za habari kufuatilia na kuripoti chaguzi katika nchi za Kiafrika. Mradi ulianzisha ukurasa wa Namibia, blogu na ukurasa wa Twita ili kuweka kumbukumbu ya habari za uchaguzi na matokeo.

Kutoka kwenye ukurasa wa Twita wa Chaguzi za Afrika
:

Hii ni siku ya 3 ya zoezi la uhakiki. Tume ya Uchaguzi imepokea asilimia 40 na asilimia 30 yamehakikishwa #namibiaelection2009
kama masaa 12 yaliyopita kutoka mtandaoni.
Ilitumwa tena kwa njia ya twita na mtu 1

Matokeo ya Uchaguzi kwenye blogu:

Hapa chini ni matokeo yaliyothibitishwa ya Uchaguzi wa Namibia 2009 (kwa rais na Wabunge) kutoka kwenye majimbo tofauti:

Matokeo yaliyothibitika kwa Tsumeb, huko Oshikoto:
Beukes
9
Garoeb
352
Goagose
9
Hamutenya
1131
….

Election Watch ni mradi wa Taasisi ya utafiti wa Sera za Umma. Election Watch inayo blogu ya matokeo ya moja kwa moja ya uchaguzi.

Madai ya kasoro
:

Chama cha RDP na vyama vingine vya upinzani viliitisha mkutano na waandishi wa habari mchana wa Jumamosi vikidai uwepo wa mlolongo wa kasoro zikijumuisha wino usifutika ambao haukufanya kazi, karatasi za kupigia kura ambazo hazikuwa na muhuri rasmi, na daftari la wapiga kura linalobadilika kila wakati (ambalo lina toleo jipya lenye tarakimu tofauti ya idadi ya wapigakura walioandikishwa).

Taasisi ya Utafiti wa Sera za Umma (IPPR) vilevile ilitumia mitandao ya kijamii kama Facebook kuwaruhusu watu kutoka duniani kote kueleza maoni na mawaoz yao kuhusu uchaguzi wa Namibia.

Chama tawala, SWAPO kina idhaa kwenye You Tube, blogu na huduma ya SMS, ambayo itawawezesha wanachama kuwasiliana na chama. Namba ya SMS ni 79276.

Chama cha Upinzani cha DTA cha Namibia kina idhaa kwenye You Tube na ukurasa wa Facebook.

Chama kikuu cha Upinzani RDP, pia kiko kwenye YouTube.

Vyombo vya habari vya kijamii havijawa maarufu nchini Namibia kama ilivyo kwenye nchi nyingine za Kiafrika kama Afrika Kusini, Kenya, Malawi, Naijeria na Tanzania. Tutayakazia macho yetu Namibia kuoana mustakabali wa vyombo vya habari vya kijamii katika nchi hiyo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.