Guinea: Jaribio la Kumuua Kiongozi wa Kijeshi Dadis Camara

Dadis Camara, ofisa wa jeshi wa Guinea aliyetwaa madaraka mwezi Disemba mwaka jana katika mapinduzi ya kijeshi, alipigwa risasi na mmoja wa wasaidizi wake jana na amesafirishwa kwenda Morocco.

Dadis Camara, ofisa wa jeshi wa Guinea aliyetwaa madaraka mwezi Disemba mwaka jana katika mapinduzi ya kijeshi, alipigwa risasi na mmoja wa wasaidizi wake jana na amesafirishwa kwenda Morocco.


Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Kapteni Dadis Camara, kiongozi wa kikundi cha jeshi kilitwaa madaraka nchini Guinea mwezi Disemba 2008, alipigwa risasi na kujeruhiwa na mmoja wa wasaidizi wake jana mjini Conakry. Kiongozi wa serikali isiyo rasmi wa Guinea, aliyetengwa na jumuiya ya kimataifa tangu kuuwawa na kubakwa kwa waandamanaji wa upinzani kulikofanywa na maaskari tarehe 28 Septemba, alisafirishwa kwa ndege kwanda nchini Morocco, ambako aliwasili katika majira ya saa 9 Alasiri GMT.

Meja Kélétigui Camara, Katibu Mkuu wa ofisi ya Rais, alisema katika mahojiano ya simu [Fr] na tovuti ya guineanews.org kuwa watu wawili amboo hafahamu majina yao, waliuwawa. Wanachama wengine wa kundi hilo la mapinduzi ya kijeshi pia walisafirishwa kwenda Morocco.

Kwenye eneo husika mjini Conakry, hali inaonekana kuwa ya ukimya, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali pamoja simu zilizopigwa kwa magazeti na serikali na mwandishi huyu. Hata hivyo, hakuna anayefahamu ukubwa wa majeraha ya kiongozi huyo wa mapinduzi ya kijeshi. Mtu mmoja kutoka katika shirika la kimataifa aliniambia kuwa Camara anaweza kuwa alijeruhiwa kichwani au shingoni.

Maoni ya mwanzo kufuatia habari hii kwenye tovuti ya RFI yameonyesha mitazamo mbalimbali. Msomaji mmoja aliyeandika bila kutaja jina aliandika:

C'est incroyable,inacceptable et injustifiable qu'un sous officier tire sur son supérieur. Ce sous officier doit tenir les conséquences de son action. Je comprends pourquoi le capitaine Moussa Dadis Camara dit que cette armée est incontrôlable…

Haiwezi kuaminika, haikubaliki, na haiwezi kuhalalishwa kwa ofisa wa cheo cha chini kupiga risasi mkubwa wake. Afisa huyu mdogo ni lazima akabiliane na matokeo ya vitendo vyake. Ninaelewa kwa nini Kapteni Moussa Dadis Camara amesema kuwa jeshi halidhibitiki…

Hata hivyo, wasomaji wengi, wanaomhusisha Camara uwajibikaji kwa mauaji ya kinyama ya waandamanaji wa upinzani ya tarehe Septemba 28, wanaonekana kuwa wanaamini jaribio la kumuua ni la haki.

Anonymous:

Dadis est entrain de vivre le resultat de sa trahison au peuple de Guinee. Du courage au peuple de Guinee surtout aux Forces vives.

Dadis ni mfano hai wa wa matokeo ya kuwasaliti watu wa Guinea. Ujasiri kwa watu wa Guinea na hasa wafanyakazi.

Joseph:

en fait,ce qui se passe actuellement en Guinnée est tellement triste, du fait que la vie perd son sens aussi sacré. si hier,on a massacré des civils (le 28 septembre),et aujourd'hui c'est le tour peut être du chef de la junte Guinéenne. c'est désolant comme spectacle…

Etant congolais (RDC), j'essaie de voir cette situation comme celle qu'on a vécu en 2001,espéront que le peuple Guinéen va se lever comme un seul homme pour mettre fin à cette situation de crise aussi ignoble et stupide pendant que le monde a besoin de l'apport de la Guinée au concert des nations.
courage…

Kinachotokea nchini Guinea ni cha kusikitisha; maisha yamepoteza utukufu wake. Kama jana, raia waliuwawa (28 Septemba), na leo, ni zamu ya mkuu wa kundi la mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea. Ni onyesho la kusikitisha lilioje…

Kwa kuwa mimi ni Mkongo (DRC), ninajaribu kuiangalia hali hii kama vile ile ya 2001, na kutumaini kuwa watu wa Guinea watanyanyuka kama mtu mmoja na kukomesha mgogoro huu wa kijinga na wenye kutia aibu. Dunia inaihitaji ushiriki wa Guinea katika jumuiya ya kimataifa.
Jipeni moyo…

anonymous:

Jusqu'à la preuve du contraire, il est seul et unique responsable des tueries au stade 28 septembre, au nom du pouvoir et s'il reçu quelques bales dans le crane au nom du mème pouvoir par son propre bras droit ou de fer, allor il merite prouvé le douleur des femmes blessées et violées par ses troupes.

Mpaka hapo tutakapota ushahidi unaopinga, ni yeye n ani yeye peke yakeanayewajibika kwa mauaji kwenye uwanja wa taifa tarehe 28 Septemba, katika jina la nguvu. Na kama akipata risasi chache kichwani katika jina la nguvu hiyo hiyo kutoka kwa mtu aliye mkono wake wa kuume, basi anastahili kusikia uchungu wa akina mama aliojeruhiwa na kubakwa na majeshi yake.

anonymous:

S'il est arrivé un malheur à Dadis aujourd'hui, je dirais que c'est une vengeance de la part de la population guinéenne. La guinée veut un president qui pourraît le représenter partout ailleurs mais pas un president qui vit couper du reste du monde, qui règne avec tyrannie.

Kama dhahama imemuangikia Dadis leo, ninaweza kusema ni kisasi cha watu wa Guinea. Guinea inataka rais ambaye atawawakilisha kila mahali, sio rais ambaye anawatenga na dunia, ambaye anatawala kwa mabavu.
Suzanne Lehn na Jennifer Brea wamechangia kwenye habari hii

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.