Venezuela: Kukutana na kazi za msanii Jesus Soto

Kazi za msanii wa Kivenezuela Jesús Soto (1923 – 2005) ni kati ya kazi maarufu zaidi zinazoonyesha sura ya sanaa ya kisasa ya Amerika ya Kati (Latin), anafahamika zaidi kwa kazi za kutumia mikono yake mwenyewe. Soto alizaliwa huko Ciudad Bolivar, Venezuela, ambako alianza kufanya kazi kama mchoraji wa mabango ya sinema. Alipata elimu yake katika miji ya Caracas na Maracaibo, lakini ilikuwa ni huko Paris ambako kazi yake ilipata mwelekeo wenye nguvu zaidi. Kazi zake maarufu ni zile “zinazoingiliana” ambazo ni vinyago vyenye muonekano wa mistari ya miraba, mirija miembamba inayoning’inia, yenye rangi zinazong’aa zilizotengenezwa na plastiki na ambayo watu huweza kupita katikati yake.

Picha ya mtoto kwenye maonyesho ya Soto iliyopigwa na Ale na imetumiwa chini ya  leseni ya Cretive Commons

Picha ya mtoto kwenye maonyesho ya Soto iliyopigwa na Ale na imetumiwa chini ya leseni ya Cretive Commons

Kwa mujibu wa wataalamu wa sanaa, sanaa ya Sato haijitengi na mtazamaji, ambaye ni mshiriki hai wa kazi ya msanii. Mauzauza na hisia vinakamilishwa na mtazamo wa akili kama matokeo ya kuona, kugusa na kuwa sehemu ya kazi yenyewe. Wanablogu wa Venezuela na jamii ya mtandaoni kwa ujumla, wanasherehekea sanaa yake kwa kupitia makala, mapitio, na video zilizochukuliwa kwenye makumbusho na ndani ya kazi zenyewe, wakati wakieleza maana ya kazi za Sato katika utamaduni wao, sura ya nchi na maisha yao ya kila siku.

Katika blogu yake, Literanova[es], Eduardo Casanova anaingia ndani zaidi kidogo kuhusu maisha ya Sato na kutupa mwanga wa histroia ya mji alikozaliwa:

Jesús Rafael Soto nació en Venezuela, en 1923, en una población cargada de historia: Ciudad Bolívar, donde se instituyó la prensa escrita y se fraguó la creación de la llamada Gran Colombia (…) Era una población aislada, sin museos ni actividades del arte. El mismo ha dicho que aprendió solo el arte de la pintura. Deja su ciudad natal y viaja a Maracaibo, en el occidente del país, para encargarse de la dirección de una escuela de artes plásticas. En 1950 se va a París y allí comienza su carrera de artista creador de nuevas formas.

Jesus Soto alizaliwa mwaka 1923 katika mji wenye historia kubwa; Ciudad Bolivar, ambako vyombo vya habari vilitoa taarifa rasmi kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi na ndipo wazo la kuundwa kwa kwa Colombia Kuu lilipoanzishwa. Ilikuwa ni eneo la watu waliotengwa, wasio na makumbusho ya kihistoria wala shughuli za kisanii. Alizoea kusema kwamba alijifunza namna ya kuchora yeye mwenyewe. Aliondoka kwenye mji huo alikozaliwa na kwenda Maracaibo, magharibi ya nchi kuwa Mkurugenzi wa shule ya sanaa. Mwaka 1950, Soto alienda Paris na huko ndiko alikoanza ubunifu wa mtindo mpya (wa sanaa).
Picha ya tufe la Soto katika Cracas ya Gillermo Ramos Flamerich chini ya leseni huru ya GNU.

Picha ya tufe la Soto katika Cracas ya Gillermo Ramos Flamerich chini ya leseni huru ya GNU.

Chaneli ya YouTube ya VenezuelaTuya inatoa mfano wa uzoefu wa kutembea kwenye mchoro wa maonyesho kwenye Makumbusho ya Jesús Soto, mjini Ciudad Bolívar:

Blogu ya Talento Venezolano [es] pia inatoa nafasi maalumu kwa ajili ya kuzungumzia yanayohusu wasaniii na ubunifu wao maarufu:

En 1967 creó la primera obra de la serie Penetrables, la cual consiste en instalaciones de tubos de plástico a través de los cuales el espectador se siente en un espacio mágico. Ambas obras que pudieron admirarse en el Museo de Arte Moderno, en el Grand Palais y el Centro Pompidou de París.

Mwaka 1967 (Soto) alitengeneza moja ya kazi zake za kwanza “zinazoingiliana” ambazo ni mirija ya plastiki ambapo mtazamaji anaweza kujisikia kwenye eneo la kimazingaombwe. Kazi zote zilizonyeshwa kwenye Makumbusho ya sanaa ya Kisasa, huko Paris kwenye Grand Palais na Kituo cha Pompidou.

You Tube vilevile imekuwa njia ya watu kuonyesha mawasiliano na hisia zao wakati wanashiriki kazi za Soto kwa vitendo. Hasa watoto, wamekuwa na muelekeo maalum wa uzoefu ndani ya kazi za msanii, ambao umeonyeshwa na kushirikishwa kwenye viideo hizi:

Mtumiaji wa YouTube elizaul1:

Na mtumiaji wa YouTube skaracas:

Kwenye tovuti ya msanii kuna kurasa za picha na habari zaidi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.