Somalia: Kuufahamisha mtandao wa waandishi na wanablogu wa Kisomali

Kituo cha habari cha Somalia ni jukwaa la waandishi na wanablogu wa Kisomali wanaoishi ndani na nje ya Somalia. Kituo kinasambaza machapicho ya habari na kuchapisha blogu zilizoandikwa na waandishi wa habari.

Kituo cha Habari cha Somalia ni jukwaa linalojitegemea kwa ajili ya waandishi wa Kisomali ndani na nje ya nchi hiyo. (Kituo hicho) kimeanzishwa kukuza wasifu wa waandishi werevu, na wachapa kazi waliyoyatoa maisha yao kuwatumiakia watu dunia nzima.
Somalia imekuwa ikichukuliwa kama nchi iliyoshindwa, nchi inayohusishwa na vifo, mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yasiyoisha, vita, ugaidi na uharamia wa kisasa. Lakini moja wapo ya habari za mafanikio kwa miaka mingi imekuwa ni kukua kwa uhuru wa habari na maoni. Hata hivyo, kuupa kipaumbele na kuutangaza ukweli huja kwa gharama kubwa.

Kituo hicho huchapisha blogu za waandishi hawa. Pia, kituo kinatawanya habari na taarifa za waandishi wa habari. Kituo pia kinaratibu waandishi wa Kisomali na wale wasio Wasomali. Kinawapa waandishi wasio Wasomali wanaoweza kuwa wanasafiri kwenda Somalia ushauri na mawasiliano ya awali. Kituo pia kinafanya kazi na mashirika makubwa ya kimataifa ya habari kwa ushirikiano, kuzalisha na kujazia habari na taarifa kuhusu Somalia na eneo lote la Pembe ya Afrika.

Solana Larsen anaandika kuhusu asili ya Mradi wa Kituo cha Habari cha Somalia:

Kama haujahisi bado, mimi si Msomali.

Katika shule ya Uandishi wa Habari jijini London mwaka 2002 nilikuwa na mwanafunzi mwenzangu aitwaye Harun Hassan ambaye nilizoea kumuuliza maswali mengi kuhusu maisha yake ya Mogadishu na Siasa za Somalia. Baada ya kuhitimu, tulibaki kuwa marafiki na nilimfahamisha kuhusu uwezekano wa yeye kuandikia mtandao wa openDemocracy.net ambapo nilikuwa mhariri kwa miaka michache. Baadaye, nikawa mhariri mtendaji wa Global Voices Online, ambapo mara chache tulikuwa na habari kuhusiana na wanablogu wa kiSomali.

Harun alizoea kuniambia kuhusu mawazo aliyokuwanayo kwa ajili ya Mradi wa Habari uliojumuisha jamii ya Kisomali mjini London. Alianzisha gazeti la Kisomali, na wakati fulani alinifuata nimsaidie kutengeneza tovuti kwa ajili ya kitu alichokiita Kituo cha Habari cha Somalia.

Habari za jamii ya KiSomali kwenye vyombo vya habari nchini Uingereza zilikuwa hasi na zisizo sahihi, Harun alifikiria kuwa namna pekee ya kusahihisha hilo,ilikuwa ni kuwarahisishia waandishi wa Uingereza kuwapata waandishi wa Kisomali na watafiti wa kuongea nao.

Tulitengeneza tovuti na blogu, lakini baadae kidogo tukakabiliwa na kazi nyingine na mradi ukadumaa.

Wavuti unayoipitia sasa, ni jaribio letu lapili la kutengeneza nyenzo ya mtandao kwa ajili ya waandishi wa Kisomali na wengine kuitumia ili kusaidia kuboresha uwelewa wa kidunia wa Wasomali na Somalia yenyewe.

Hapa chini ni baadhi ya makala za blogu za hivi karibuni kabisa kutoka kwenye Kituo cha Habari cha Somalia:

Katika makala yenye kichwa cha habari, Uzinifu wa Kukumbuka, Fathia Absie anaandika kuhusu kushitakiwa kwa Joshua Asisam mlinzi wa amani katika Somalia, kwa kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa Kisomali:

Mahakama ya Kijeshi ya Kampala ilimhukumu Joshua Asisa kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela. Bw. Asisa ambaye ni mwanachama wa walinzi wa amani wa AMASOM nchini Somalia alipatiaka na hatia ya kujuhusisha na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa Kisomali aitwaye Nimco Omar na kumpa ujauzito baada ya kumuoa kwa kumdanganya kuwa alikuwa Mwislamu.
Habari hii ilitokea mwaka uliopita huko Mogadisho lakini hakuna aliyesikia mpaka mwanamke huyu mdogo alipokwenda Kampala na kumshitaki Bw. Asisa mahakamani kwa kumdanganya. Mohamed Abubakar Ahmed ambaye ni mwandishi aliyeiibua habari hiyo aliniambia kuwa aliipata habari hiyo baada ya kuwa imeripotiwa na magazeti ya Uganda. Baada ya hapo, Bw. Ahmed alijaribu kuonana na viongozi wa jamii ya Kisomali waishio Kampala na akaweza kukutana na msichana huyo. Aliniambia kuwa Bi. Omar alimwambia kuhusu habari hiyo na jinsi alivyokutana na Bw. Asisa ambaye ni daktari. Alikuwa akifanya kazi kwenye hospitali binafsi kwa ajili ya jeshi la Uganda mjini Mogadisho.

kwa nia ya kutawanya neno..,” anaandika Idil Osman:

Mafunzo ya kijeshi yanayofanyika katika makambi ya wakimbizi wa Kisomali huko Dadaab, Kaskazini mashariki ya Kenya yamechochea kelele zinazochanganya wengi ndani na nje ya eneo. Hata hivyo ninashangazwa sana na msimamo wa serikali ya Kenya. Nilifanya ripoti ya uchunguzi katika suala hili mapema kazini ambapo waziri wa ulinzi wa Kenya alidai kwa msimamo kwamba Kenya haikutoa ruhusa kwa mafunzo haya kufanyika.
Wakati huo huo mashahidi na wanaharakati wa haki za binadamu wanarekodi na kuweka kumbukumbu za ushahidi wa vijana hawa wanaowekwa katika magari ya kijeshi ya Kenya na kusafirishwa kwa magari kwenda kwenye vyuo vya mafunzo ya Kijeshi vya Kenya.
Wengi wa vijana hawa wanachukuliwa kwa kudanganywa na kuahidiwa mshahara mzuri pamoja na kazi inayoaminika kwenye miradi ya kijeshi ya Umoja wa Mataifa/Umoja wa Ulaya/Umoja wa Afrika..
Kiukweli wanafunzwa kwenda na kupigana kwenye vita ile ile waliyoikimbia na kuwafanya wawe wakimbizi. Wengi wa wakimbizi hawa vijana wanaarifiwa kuwa chini ya umri unaotakikana na wamechukuliwa bila ridhaa ya wazazi wao.
Imevunja haki zao za kimataifa za binadamu kama wakimbizi kwa mujibu wa tangazo la kwenye vyombo vya habari lilitolewa hivi karibuni na Shirika la Human Rights Watch, kwa sababu wakimbizi wanatakiwa kuwekwa kwenye mazingira ya kiraia.

Solana anajadili suala la ‘chanzo kisichotaka kufahamika’ katika taarifa za vyombo vya habari vya Kimagharibi kwenye makala yake aliyoipa jina la “Wakati vyanzo vya mahali vinapochagua kutokuwa na jina

nimechukua toleo la hivi karibuni la jarida la National Geographic Magazine kwa habari yao inayohusu ‘Somalia iliyovunjika’. Picha za Mogadishu zilizopigw ana Pascal Maitre ni nzuri, ingawa zinaonyesha uharibifu mkubwa. Na mwandishi, Robert Draper anatoa muhtasari wa haki na wenye mguso kuhusu historia tata. Pia anaziweka wazi changamoto za upashaji habari wa kigeni.

Katika hali inayoacha maswali, mwandishi wa Kisomali Harun Hassan anatajwa kwa jina kwenye maelezo ya picha inayomwonyesha mlinzi wa barabarani mjini Mogadishu, lakini kwa kiwango ninachoona haionekani kwenye habari yenyewe. Kwa nini kuna ugumu wa kuweka wazi chanzo? Kama Draper alihangaika kuwasiliana na kuvihoji vyanzo vya Habari vya Somalia, kwa nini asiwaeleze wasomaji wake habari hiyo?

Je, huu ndio uzoefu wa wandishi wa Kisomali wanaowasaidia waandishi wa Kimagharibi kuhabarisha? Ninatumainii wanachama wa Kituo cha Habri cha Somalia watasaida kutupa mwanga wa jinsi inavyokuwa kwenye sehemu hiyo ya timu inayotengeneza ripoti.

Unaweza kuona orodha ya wanachama waliopo wa Kituo hicho hapa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.