Kampuchea: Vikwazo Vya Intaneti Vyalenga Wasanii

Kadiri idadi ya watumiaji wa intaneti invyokua kwa haraka katika Kusini Mashariki ya Asia kwenye miaka ya hivi karibuni, na ndivyo kuchujwa kwa kwa habari kunavyozidi, kuanzia Uchina mpaka Kampuchea, kana kwamba kunafuata mkondo wa Mto Mekong.

Siyo tu “ukuta mkuu wa moto wa Uchina” unaojulikana na watu wengi, nchi ya kidemokrasia kama vile Thailand pia inazuia idadi kubwa ya tovuti; nchini Vietnam, wizara yake ya Habari na Mawasiliano hivi karibuni ilitoa tamko la kusimamia na kutekeleza taratibu za kublogu nchini humo tangu mwishoni mwa mwaka 2008. Utaratibu na utekelezaji vikiwa vimeshika nafasi, serikali hizo zimeendeleza na kusimika mashine za kuchuja ili kudhibiti jinsi raia wanavyoandika na kuyapata yaliyomo mtandaoni.

Pamoja na nchi ya Kampuchea kuwa na uenezi mdogo zaidi wa intaneti (watumiaji 70,000 hadi kufikia mwaka 2007), wasanii wanatambulika zaidi kwa uwepo wao kwenye mtandao wa intaneti. Ongezeko hili la matumizi ya blogu ili kufikia kadamnasi kubwa kunavutia zaidi ya kujionyesha na kuungwa mkono.

Aliyekuwa mchoraji huru wa picha za vikaragosi wa Jarida la Uchumi la Mashariki ya Mbali tokea mwaka 1997 – 1999, Bun Heang Ung anaishi Australia hivi sasa. Akiiangalia nchi yake kutokea upande mwingine, mchoraji huyo mwenye umri wa miaka 57 alizindua blogu ya Sacrava Toons mnamo mwaka 2004, mwongo mmoja baada ya kuchapisha “Mapinduzi ya Mauaji ; Uhai na Kifo katika Kampuchea ya Pol Pot” kitabu chake cha kwanza cha michoro ya rangi nyeusi na nyeupe ambacho kinaelezea uzoefu wake binafsi wakati wa utawala wa Khmer Rouge. Katika kuupaza ujumbe wake, mchoraji huyu mwenye kipaji huchapa michoro yake ya vitu vinavyomgusa katika mtandao wa intaneti. Katika moja ya jumbe zake za hivi karibuni, alitumia “nina ndoto” kama picha ya nyuma ya mchoro wake wa Barack Obama, rais wa 44 wa Marekani.


Barack Obama kama alivyochorwa na Bun Heang Ung

Hivi karibuni, kwa mujibu wa Wikileaks, blogu ya mchoraji huyu wa vikaragosi vya kisiasa imezuiwa nchini Thailand, ambako Wizara yake ya Habari na Mawasiliano inashika hatamu za kufunga tovuti ambazo zinamtukana mfalme.

Bloga wa Kampuchea Thom Vanak, anayeblogu kwenye Blog By Khmer, anafikisha ujumbe kuhusu suala hili:

Kuhusu sheria inayokataza kumtusi mfalme, japokuwa nafikiri kuwa ni sheria ya kizamani sana na imepitwa na wakati katika wakti huu, hata hivyo, bado ni sheria ya Ki-Thai. Kama nitatia mguu kwenye nchi ya Wa-Thai lazima niheshimu sheria zao. Sawa tu na vile nitakapotembelea nchi nyingine yoyote, nitaheshimu sheria za nchi hiyo.

Wakati blogu ya mchoraji mashuhuri wa vikaragosi inaonekana kwenye orodha ya kuzuiwa (kama ilivyokuwa tarehe 20 desemba 2008) ya Thailand, Wizara ya Masuala ya Wanawake ya Kampuchea, mwezi wa Desemba mwaka jana, ilitishia kuzuia tovuti yenye michoro ya wacheza ngoma ya Apsara walio vifua wazi pamoja na mwanajeshi wa Khmer Rouge. Jaribio la kuifunga reahu.net (au kuichuja kwa kutumia watoaji huduma za mawasiliano aktika jiji la Kampuchea) vilishika mwangwi wa wananaharakati wa haki za binadamu, ambaye alinukuliwa akisema kwamba “Tovuti hiyo lazima ifungwe kwani inamvuto mkubwa kwa vijana wadogo wa Kikampuchea.”

Reahu.net hivi sasa haipatikani kwa watumiaji wa intaneti walioko nchini Kampuchea, ingawa hakuna vizingiti kama hivyo nchini Marekani, ujumbe wa makosa hutokea:

Picha ya tovuti ya reahu.net inavyochujwa na watoa huduma za intaneti nchini Kampuchea.

Mwanablugu mashuhuri asiye na jina wa Kampuchea kwenye ‘Cambodia: Details are Sketchy’ ameandika kuhusu suala hili tata:

“Kama kuna yeyote anayetakiwa kuelewa thamani ya uhuru wa kujieleza, Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Utetezi kule Licadho ndiye anayepaswa kuwa. Inavunja moyo kwamba Vann Sophath anaunga mkono kuchujwa kwa michoro ya Reahu”

Msanii Reahu alituma ujumbe kwenye tovuti yake, ambayo imeongezeka umashuhuri hivi karibuni baada ya kuangaliwa na vyombo vya habari katika miezi michache iliyopita, ili kuwajibu wanaompinga:

Kutokana na malalamiko niliyoyaona, ninajiuliza ni jinsi gani sisi kama Wa-Khmer tunaweza kuishi katika karne ya 21. Tafadhalini kuweni na akili huru, ni lazima muweze kuona zaidi ya kuta nne zinazowazunguka.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.