Sokari anaandika kuhusu tangazo la biashara la Kombe la Dunia la kibaguzi lililotengenezwa na wakodishaji wa magari wa Kijerumani SIXT: “Tangazo hilo hapo juu lilitumwa kwangu na rafiki kutoka Ujerumani ambaye alifafanua hivi: Linacheza kauli mbiu kadhaa zenye mtazamo wa kiUlaya, mtazamo unaodharau Uafrika kuhusiana na mchezo wa mpira unaokuja kati ya Ghana/Ujerumani.”
Habari mpya Kuhusu Germany
3 Julai 2010
14 Aprili 2010
Piga kura kuchagua “Blogu Bora Zaidi”
Upigaji kura mtandaoni umeanza kwa ajili ya Tuzo ya Blogu Bora Zaidi inayotolewa na Deutsche Welle (Shirika la Habari la Ujerumani), moja kati ya mashindano ya blogu yenye hadhi kubwa kimataifa na blogu zilizotajwa kushiriki ni za lugha kumi na moja tofauti. Unaweza kuipigia kura blogu uipendayo hadi April 14, 2010.
28 Machi 2010
Siku ya Ada Lovelace: Kuwapongeza Wanawake Wanajishughulisha Kupigania Teknolojia na Uwazi Ulimwenguni

Katika kusherehekea Siku ya Ada Lovelace tunawaletea makala fupifupi kuhusu wanawake kadhaa walio sehemu mbalimbali duniani ambao hutumia teknolojia ili kuzifanya serikali ziwe wazi na zinazowajibika zaidi.
13 Disemba 2009
Austria: Jinsi Nyenzo Za Habari Za Kijamii “Zinavyoviwashia Moto Vyuo Vikuu”
Je, ulijua kwamba katika wakati huu vyuo vikuu vingi kote Ulaya vinakaliwa na wanafunzi? Vuguvugu hili lote limeratibiwa kwa kutumia nyenzo za uanahabari wa kijamii katika mtandao.
16 Novemba 2009
Misri: Haki ya Kijerumani kwa Marwa El Sherbini
Muuaji wa Marwa El-Sherbini, mwanamke wa Kimisri ambaye alichomwa visu mpaka kufa na muhamiaji mwenye asili ya Urusi na Ujerumani, Alex Wiens, ndani ya mahakama huko Ujerumani, amehukumiwa kifungo cha maisha, bila uwezekano wa kuachiwa mapema. Haki hatimaye imetolewa na muuaji anaadhibiwa, wanasema wanablogu wa Misri.
11 Novemba 2009
Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini
Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.
15 Oktoba 2008
Macho ya Kimataifa kwenye Uchaguzi wa Marekani
Kadiri uchaguzi wa Marekani unavyokaribia, ndivyo kadiri macho ya kimataifa yanavyozidi kuelekezwa katika sera za nje za taifa hilo na wagombea wake wakuu. Kazimiradi kama vile ile ya Collective Journalism inayofanywa na Current TV (Uandishi wa Habari wa Umma wa Current TV) na Global Voices' Voices Without Votes (Mradi wa Global Voices - Sauti Zisizo na Kura) zimechukua jukumu la kukusanya taarifa na kuzipa mtazamo wa kimataifa katika masuala ya ndani ya sehemu fulani tu ulimwenguni.




























Kiungo cha RSS kwa Germany 







mambo vipi wanablog muko powa wote.kama mumenisoma nijibuni.
Asante. Nimepita hapa natafuta japan na china wamemalizaje ugomvi wao kuhusu visiwa,pia chanzo cha ugomvi...