Habari kuhusu Zambia

Siasa za Afya ya Rais Nchini Zambia

  5 Novemba 2014

Ajong Mbapndah wa Pan African Vision anazungumza na Gershom Ndhlovu kuhusu siasa zinazozunguka ugonjwa na kifo cha Rais wa Zambia Michael Sata: Rais Michael Sata siku za hivi karibuni amefariki dunia jijini London na inaonekana afya yake na huduma za tiba alizopatiwa ziligobikwa na usiri, kwa nini wananchi wa Zambia...

Baraza la Mawaziri Nchini Zambia Lichunguze Afya ya Rais

  16 Agosti 2014

Kwa mtazamo wa tetesi zilizoenea sana kuhusu afya ya rais wa Zambia, Michael Sata, Gershom Ndhlovu ana hoja kwamba katiba inalipa Baraza la Mawaziri mamlaka ya kuchunguza afya yake: Mara ya mwisho rais wa Zambia Michael Sata kuonekana hadharani ilikuwa takribani Juni 20 ambapo alikuwa mwenyeji wa ujumbe wa serikali...

Je, Madaraka ni Matamu Kiasi cha Watawala wa Afrika Kushindwa Kuyaachia?

  30 Mei 2014

Gershom Ndhlovu anaangalia sababu za kwa nini watawala wa Afrika hawataki kuachia madaraka: Kumekuwepo na tetesi, dondoo na hata uvumi kuhusu afya au basi udhaifu wa afya ya Rais wa Zambia Michael Chilufya Sata, aliye madarakani tangu Septemba 2011. Tetesi hizi zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba serikali...

Ni kazi Ngumu Kuwa Kiongozi wa upinzani Nchini Zambia

  14 Mei 2014

Gershom Ndhlovu anaelezea ni kwa nini ni vigumu kuwa kiongozi wa upinzani nchini Zambia: kwa kweli ni kazi ngumu kuwa kiongozi wa upinzani nchini Zambia. Unakabiliana na polisi kila siku, hatari ya kutupiwa gesi ya machozi au hata kufungwa kwa ajili ya kufanya kazi ambayo lazima uifanye – Kukutana na...

Zambia: Filamu yaYouTube Kuhusu Athari za Machimbo ya Madini

  15 Oktoba 2012

Filamu ya Uchunguzi yenye jina "Zambia: Shaba Nzuri, Shaba Mbaya" inayohusu machimbo ya shaba nchini Zambia na athari zake kwa jamii imewekwa kwenye mtandao wa YouTube na mpaka sasa imevuta watazamaji zaidi ya 6,000. Baada ya kuitazama filamu hiyo, mtumiaji mmoja wa mtandao wa YouTube aliandika, "Jililie eeh nchi yangu nzuriKwa nini tubaki masikini katikati ya utajiri huu wa madini yanayochimbwa kwa gharama ya afya za wenyeji?"