Habari kuhusu Afrika Kusini
Mbeki Rais wa Mstaafu wa Afrika Kusini Bado Anaamini ‘Mambo ya Ajabu’ Kuhusu UKIMWI/VVU
Mbeki amekosolewa kwa kuandika barua inayokanusha kwamba hajawahi kusema kuwa 'VVU havisababishi UKIMWI'. "Nilichosema ni kwamba 'virusi hivyo havisababishi upungufu wa kinga'."
Afrika Kusini Yakumbuka Mashindano ya Kombe la Dunia 2010 Yalivyokuwa
Mnamo Juni 11, 2010, Afrika Kusini ilikuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya michezo duniani. Ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika barani Afrika.
Kuhusu Uamuzi wa Mahakama wa Haki ya Kusaidiwa Kufa Nchini Afrika Kusini
Profesa Pierre de Vos anaingia rasmi kwenye mjadala mkali kuhusu uwezekano wa kumsaidia mtu kufa nchini Afrika Kusini baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuamua kwamba mtu anayekufa ana haki ya kusaidiwa kufa na daktari ili aweze kuyahitimisha maisha yake: Ni muhimu kuona kwamba hukumu hii haimlazimishi mtu kuyakatisha maisha...
Lugha za Pili Zinazoongozwa Kuzungumzwa Zaidi Afrika
Don Osborne anajadili habari iliyowekwa kwenye tovuti ya Chuo Kikuu cha Olivet Nazarene ikionesha ramani ya “Lugha za pili kuzungumzwa zaidi duniani.” Anaeleza matatizo makuu kutokana na habari hiyo: Suala la kwanza ni kudhani kwamba “lugha inayozungumzwa zaidi kwenye nchi yoyote huwa wazi; mara nyingi, ni lugha ya taifa husika.”...
Maisha ya Wakenya Yana Thamani, Wanafunzi wa Kiafrika Wasema Kwenye Ibada ya Kuwaombea Wahanga wa Garissa Jijini Beijing
Kikundi cha wanafunzi wa Kiafrika jijini Beijing waliandaa ibada ya kuwakumbuka wahanga 147 wa shambulio la Garissa pamoja na china kutokuwa na uvumilivu kwa watu wanaoomboleza hadharani
Afrika Kusini Imejitenga na Waafrika Wengine?
Mashambulizi ya hivi karibuni huko Afrika Kusini yanahusisha wahamiaji kupigwa, kuuawa, kuchomwa moto, wizi madukani pamoja na wizi wa mali zao. Watu watano wameshauawa, miongoni mwao akiwamo mvulana wa miaka 14 aliyeuawa siku ya jumatatu.
Mapendekezo Yanapokelewa kwa Ajili ya Mwezi wa Historia Nyeupe 2015
Likiwa limeandaliwa na blogu ya Africa is a Country [Afrika ni Nchi], tukio la Mwezi wa Historia Nyeupe linajongea mwezi ujao: Mwezi Machi mwaka jana ndio ulikuwa mwezi wa uzinduzi wa zoezi hilo kwenye blogu hii, na bila kupuliza sana mavuvuzela yetu kw akujisifu, ule kwa hakika ulikuwa ni mwezi...
Wachoraji 10 wa Kiafrika wa Vitabu vya Watoto Unaopaswa Kuwajua
Jennifer Sefa-Boakye anasaili orodha ya washindani 10 bora zaidi wa tuzo ya Golden Baobab kwa Wachoraji wa Kiafrika: Mwaka jana shirika la Afrika lenye makazi yake nchini Ghana, Golden Baobab, liliwatambulisha wachoraji kadhaa wenye vipaji, ambao kazi zao ni kama vile masimulizi ya Ashanti yaliyosukwa kutoka miji ya Moroko na...
Hukumu ya Haki? Ina uzito wa Kutosha? Oscar Pistorius Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Mitano Jela
Mkimbiaji wa Afrika Kusini aliyepatwa na hatia kwa kumwuua pasipo kukusudia rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp imelinganishwa na hukumu ya jangili aliyefungwa miaka 77 jela kwa kumwuua faru mwezi Julai
Majadiliano na Picha za Mkutano wa Highway Africa 2014
Mkutano wa Highway Africa 2014 ulifanyika kuanzia tarehe 7-8 Septemba, 2014 kwenye Chuo Kikuu cha Rhodes, Grahamstown, Afrika Kusini. Maudhui ya mkutano huo yalikuwa Mitandao ya Kijamii -kutoka pembezoni kwenda kwenda kwenye vyombo vikuu vy habari. Angalia picha na mzungumzo kuhusiana na mkutano huo hapa.