· Oktoba, 2008

Habari kuhusu Afrika Kusini kutoka Oktoba, 2008

Afrika ya Kusini: VVU na UKIMWI na mabadiliko ya sera

  26 Oktoba 2008

Mwishoni mwa mwezi Septemba, Barbara Hogan, aliteuliwa na Rais wa mpito Kgalema Motlanthe kuwa waziri mpya wa afya wa Afrika ya Kusini, akichukua nafasi ya mtangulizi wake mwenye utata mwingi, Manto Tshabalala-Msimang. Wanaharakati wa masuala ya UKIMWI na raia wengi wa Afrika ya Kusini wana matumaini makubwa kwamba hatua hii...

Macho ya Kimataifa kwenye Uchaguzi wa Marekani

  15 Oktoba 2008

Kadiri uchaguzi wa Marekani unavyokaribia, ndivyo kadiri macho ya kimataifa yanavyozidi kuelekezwa katika sera za nje za taifa hilo na wagombea wake wakuu. Kazimiradi kama vile ile ya Collective Journalism inayofanywa na Current TV (Uandishi wa Habari wa Umma wa Current TV) na Global Voices' Voices Without Votes (Mradi wa Global Voices - Sauti Zisizo na Kura) zimechukua jukumu la kukusanya taarifa na kuzipa mtazamo wa kimataifa katika masuala ya ndani ya sehemu fulani tu ulimwenguni.

Afrika Ya Kusini: Mjomba, Urais Uko Wapi?

  1 Oktoba 2008

Ulimwengu wa blogu nchini Afrika ya Kusini umelipuka kutokana habari za hivi karibuni kuhusu mawaziri 11 na manaibu 3 kujiuzulu wakiwemo mawaziri vinara, Trevor Manuel na Naibu Rais, Phumzile Mlambo-Ngcuka. Yafuatayo ni yale wanayosema mabloga …