The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

South Africa Kumbukumbu za nchi

Kiungo cha RSS kwa South Africa

2009-11-11

Humor ,
Language

Wimbo wa Taifa wa Afrika Kusini kwa wanaoongea Kiingereza: Ni njia kuu iliyoje ya kufafanua kwa kuonyesha Wimbo wa taifa wa Afrika Kusini kwa wale kati yetu ambao kwanza hatuufahamu mpaka sasa, pili tunaoufahamu lakini pengine hatujui jinsi ya kutamka maneno yake na tatu ambao hatuongei lugha iliyo kwenye wimbo huo.

2009-07-27

Afrika: Ujio wa Mkonga wa Seacom Wazua Mjadala

Ujio wa mkonga unaopita chini ya bahari utakao ongeza uwezo na kupunguza gharama za intaneti barani Afrika umewasha majadiliano na mvuto katika ulimwengu wa blogu wa Afrika. Seacom, ambayo inaunganisha Afrika Kusini, Tanzania, Kenya, Uganda na Msumbiji na Ulaya pamoja na Asia, ilianza kutumika moja kwa moja Alhamisi, kwa kuziunganisha nchi za Afrika ya mashariki na Afrika ya kusini kwenye mtandao wa dunia wenye wigo mpana.

2009-07-22

Afrika: Obama Atumia Nyenzo Mpya za Habari Kuzungumza na Waafrika

“Umeshawahi kutaka kumuuliza kijana wetu wa Nyangoma maswali yoyote? Kwa maneno mengine, je ungependa Rais wa Marekani, Barack Obama ajibu maswali yako?,” ndivyo inavyoanza makala kwenye blogu ya Hot Secrets inayohusu matumizi ya Obama ya zana mpya za habari ili kukutana na kuongea na Waafrika wa kawaida.

2009-07-19

Afrika Kusini: Kuvuvuzela au Kutovuvuzela?

Mjadala kuhusu kifaa maarufu kinachoitwa vuvuzela kinachopigwa na mashabiki wa mpira wa miguu Afrika Kusini umetawala katika blogu mbalimbali duniani tangu kuanza kwa Kombe la Mabara la mwaka huu nchini Afrika Kusini, lililohitimika wiki iliyopita. Waandishi wa habari, watazamaji wa televisheni, makocha na baadhi ya wachezaji wa kigeni walitoa wito wa kusitisha matumizi ya kifaa hiki katika Kombe la Dunia la 2010 nchini Afrika Kusini. Mabishano haya yana sauti kubwa kama chombo chenyewe.

2009-04-22

Afrika ya Kusini: ANC Yafanya Mjadala wa Uchaguzi Kwa Kutumia huduma ya Twita

Vyama vya siasa nchini Afrika ya kusini vimo katika hatua za mwisho za kampeni ya uchaguzi ujao. Chama tawala cha ANC (African National Congress) kilifanya mjadala kwa kutumia huduma ya twita.

2009-01-26

Blogu za Afrika Zapendekezwa Kupokea Tuzo ya Bloggies 2009

Blogu zilizopendekezwa kwa ajili ya Tuzo ya Tisa ya Zawadi za Weblog: Mapendekezo ya blogu katika mashindano ya Bloggies ya 2009 yalifunguliwa tarehe 1 Januari na kufungwa tarehe 19 Januari. Kwa mujibu wa waandalizi, mashindano hayo ya Bloggies ni mashindano ambayo yamedumu kwa muda mrefu zaidi mtandaoni, na mapendekezo pamoja na uchaguaji wa washindani katika fainali, ni juu ya msomaji wa blogu. Mshindi hupata senti 2,009 za Marekani! Je, ni mabloga gani wa Kiafrika waliopendekezwa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha blogu bora zaidi?

2008-11-04

Afrika ya Kusini: Matumizi ya Simu za Viganjani Kupambana na UKIMWI

Afrika ya Kusini imegundua silaha mpya katika vita dhidi ya VVU/UKIMWI - simu za viganjani. Kwenye mchakato mpya, jumbe za maandishi zitakuwa zikitumwa kila siku kuwahamasisha Wa-Afrika ya Kusini kwenda kupimwa na kutibiwa ugonjwa huo. Mradi huo, unaoitwa Mradi wa Masiluleke au Project M, ulitangazwa rasmi wiki iliyopita wakati wa kongamano ...

2008-10-26

Afrika ya Kusini: VVU na UKIMWI na mabadiliko ya sera

Mwishoni mwa mwezi Septemba, Barbara Hogan, aliteuliwa na Rais wa mpito Kgalema Motlanthe kuwa waziri mpya wa afya wa Afrika ya Kusini, akichukua nafasi ya mtangulizi wake mwenye utata mwingi, Manto Tshabalala-Msimang. Wanaharakati wa masuala ya UKIMWI na raia wengi wa Afrika ya Kusini wana matumaini makubwa kwamba hatua hii ...