Habari kuhusu Naijeria kutoka Februari, 2015
Je, Kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu Naijeria Kunatokana na Sababu za Kiusalama?
Jeshi la Nigeria litaendesha operesheni maalum ya wiki sita dhidi ya Boko Haram ili"kuepusha kuingiliwa na shughuli za uchaguzi." Baadhi ya watu wanatilia shaka kuwa, kuahiririshwa kwa uchaguzi ni mkakati wa kisiasa.
Vijana wa Naija Wacharuka Kufuatia Shambulizi la Boko Haram huko Bosso na Diffa
Kwa mara ya kwanza, Boko Haram kimetekeleza shambulio kwenye mpaka na Naija na vijana wa ki-Naija hakuweza kuvumilia. Boko Haram walishambulia Bosso na Diffa, miji miwili iliyo kusini mashariki mwa Naija kwenye mpaka wa nchi hiyo na Naijeria lakini walirudishwa nyuma na majeshi ya Chad na Naija. Boko Haram imepoteza...
Boko Haram Yaua Watu Wasiopungua 81 Huko Fotokol, Cameroon Kaskazini
Mnamo Februari 4, Boko Haram walifanya shambulio baya kwenye mji wa Fotokol Kaskazini mwa Cameroon, baada tu ya kuvuka mpaka wa Naijeria. Mamia wa raia wanahofiwa kupoteza maisha 81 wamethibitika kufa na Wizara ya Ulinzi. Shirika la Haki za Binadamu nchini humo linaamini kwamba karibu watu 370 wameuawa. Mashuhuda wa...