Habari kuhusu Mauritania

Mauritania: Uchaguzi wenye udanganyifu?

  27 Julai 2009

Tarehe 18-07-2009, miezi 11 baada ya mapinduzi ya kijeshi yakiongozwa na Jenerali Mohamed Ould Abdel Aziz, Mauritania imemchagua Jenerali huyu kwa Urais, na kusababisha wapinzani wakuu wa Abdel Aziz kuukataa uchaguzi kwamba ni “kiini macho,” kwa mujibu wa Habari za BBC. Pitio la haraka haraka kwenye blogu za nchi za Saheli linaonyesha kwamba wapinzani wako katika ushirika mzuri.

Arabeyes: Rais wa Mauritania Aliyepinduliwa Katika mapinduzi ya Kijeshi

  17 Agosti 2008

MAKAMANDA wa jeshi wamemuondoa madarakani Rais Sidi Ould Cheikh Abdallahi, rais wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi huru katika miongo miwili, katika mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa Jumatano iliyopita baada ya mtafaruku wa kisiasa uliotokana na rais huyo kuwatimua kazi majenerali wanne wa ngazi za juu wa jeshi. Makamanda wa jeshi walitangaza...