GlobalVoices katika

Mali

Kumbukumbu za nchi · 6 jumbe


Habari mpya Kuhusu Mali

12 Februari 2013

Udhaifu wa Watawala wa Afrika unajionesha Mali?

Ousmane Gueye katika tovuti ya Mondoblog anaandika [fr] kuhusu kuchelewa kupeleka vikosi vya kijeshi kasikazini mwa Mali:

Kama tungekuwa tunasaiili matokeo ya watu wenye amani na huru kuingilia kati hali ya mambo nchini Mali, basi ni wazi kuwa kwa kuchelewa kupeleka vikosi vya ulinzi, nchi za Afrika zimewakosea wananchi wa Mali kwa mara nyingi…kelele zote za wakuu wa nchi lakini bado hawajaweza kutimiza lengo lolote waliloliweka wao kama hatua ya kupunguza nguvu ya Waslamu wenye msimamo mkali nchini Mali.

22 Januari 2013

“Wanasemaje Bamako?” Mazungumzo na Awa anayeishi Mali

Mazungumzo ya kila siku kwa njia ya skype(kwa Kifaransa)  kati ya Awa Traoré aliyeko Bamako na Anne Morin akiwa Ufaransa (kupitia anuani ya @annagueye)

Anne Morin na Awa Traoré wanabadilishana mawazo kuhusiana na maisha ya kila siku mjini Bamako, ujira usiokidhi mahitaji, gharama za maisha na hali ya kisiasa isiyotabirika wakati huu ambapo vita vinanukia nchini humo.

17 Juni 2012

Video jumbe
Mabadiliko ya Mfumo wa Ustawi wa Jamii ya Kiafrika

Soma makala hii.

Utekelezaji wa mifumo ya hifadhi ya jamii ya taifa bado uko katika hatua za mabadiliko katika nchi nyingi za Afrika. Mafanikio ya mifumo iliyopo yanajadiliwa na wataalamu wa hifadhi za jamii katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.

30 Aprili 2012

Photos jumbe
Mali: Kimya cha Wanablogu wa Nchini Humo

Soma makala hii.

Wakati mtandao wa intaneti umetawaliwa na blogu, ujumbe wa twita na video kutoka nchi mbalimbali, watumiaji wa intaneti wenyeji wa Mali wangali kimya. Mji mkuu, Bamako, umeathirika kwa kukatika kwa umeme kwa kile kinachodaiwa kuwa kuadimika kwa mafuta. Katika mazingira kama haya, kipaumbele si kutuma ujumbe, bali kutafuta kutafuta taarifa kuhusu viongozi wapya wa sehemu ya Kaskazini ya Nchi hiyo.

15 Aprili 2012

Video jumbe
Mali: Raia Washtushwa na Mapinduzi ya Kijeshi

Soma makala hii.

Askari walioasi wametangaza kwamba wanatwaa madaraka nchini Mali, baada ya kuwa wameteka nyara kituo cha televisheni ya taifa pamoja na ikulu. Wanadai kwamba serikali ilishindwa kuvipa vikosi vya jeshi la nchi hiyo msaada ili kuwakabili vilivyo wapiganaji wa kabila la Tuareg waliokuwa wakiteka miji ya kaskazini mwa nchi hiyo.

23 Machi 2010

Video jumbe
Mali: Vitambaa Vyasuka Nguzo za Uchumi na Utamaduni

Soma makala hii.

Kwa kupitia video, tunaona na kujifunza kuhusu umuhimu wa utamaduni na ongezeko la kiuchumi ambalo utengenezaji vitambaa huwapa baadhi ya watu na mashirika nchini Mali. Vikundi vya wanawake, wasanii na watalii wote wananufaika na utamaduni huu wa kutia rangi vitambaa na upakaji rangi kwa kutumia matope.

Sehemu za Dunia

Nchi

Lugha