The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

Kenya Kumbukumbu za nchi

Kiungo cha RSS kwa Kenya

2009-11-10

Governance ,
Law

Ubia wa Kuleta Mabadiliko umetoa tamko linalowataka mwai kibaki na raila odinga kushirikiana na mahakama ya kimataifa ya Jinai na kuhakikisha muswada wa Tume Maalum unapitishwa nchini kenya na kurasimishwa kama sheria ndani ya wiki mbili.

2009-11-05

Media

Marvin anaandika kuhusu Afripot, tovuti ya habari inayotilia makini habari za Afrika: “Hivi sasa anatambulisha chungu cha kuyeyushia Afrika – Afripot. Tayari nimo ndani ninayeyuka na ninatumaini kukuona pale na wewe pia kwani mazungumzo kuhusu Afrika na Waafrika yanachukua kasi na kupamba moto. Ni nani ajuaye, inaweza kutengeneza joto la kutosha na kulazimisha mabadiliko tuayoyahitaji sana.”

2009-11-04

Development ,
Technology

Mradi wenye lengo la kutengeneza ramani mpya ya wazi ya kitongoji cha Kibera mjini Nairobi, Kenya: “Na jana tulimaliza siku nzima pale MS Action Aid kenya, ambako wanafunzi wa ki-Denmark pamoja na wengine waliotokea kwenye mashirika mbalimbali kama vile Ushahidi, UNICEF, Umande Trust na World Bike, walipoonyeshwa mbinu za kutengeneza ramani.”

2009-10-11

Australia: Wanawake wa Kenya wakataliwa haki ya ukimbizi

Wanawake wawili wanakabiliwa na uwezekano wa kutimuliwa kutoka Australia baada ya maombi yao ya kuomba hifadhi kukataliwa, pamoja na hatari wanayoweza kuipata ya kulazimishwa tohara ya kike ikiwa watarudishwa nyumbani.

2009-07-29

Kenya: Ukame Uliokithiri Wachochea Mgogoro kati ya Binadamu na Wanyama Pori

Kenya inakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja kwa mujibu wa Idara ya Hali ya Hewa. Ukame huu umeathiri nchi nzima, lakini athari zake zimeonekana zaidi katika jamii ya Kimasai ambayo chanzo zhake cha kwanza cha maisha ni mifugo. Wakikabiliwa na hatari ya kupoteza mifugo yao ...

2009-07-22

Afrika: Obama Atumia Nyenzo Mpya za Habari Kuzungumza na Waafrika

“Umeshawahi kutaka kumuuliza kijana wetu wa Nyangoma maswali yoyote? Kwa maneno mengine, je ungependa Rais wa Marekani, Barack Obama ajibu maswali yako?,” ndivyo inavyoanza makala kwenye blogu ya Hot Secrets inayohusu matumizi ya Obama ya zana mpya za habari ili kukutana na kuongea na Waafrika wa kawaida.

2009-07-20

Afrika: Wanablogu wamwombolezea Michael Jackson

Barani Afrika, wanablogu wanatoa heshima zao za mwisho kwa Michael Jackson baada ya kifo chake hivi karibuni kwa kutuma picha, video za muziki, mashairi pamoja na tafakari. “Pumzika Kwa Amani” anaandika Mwanablogu wa Kenya WildeYearnings. “Sasa unalo anga zima kucheza kwa madaha kwa staili ya kutembea mwezini…”