Habari kuhusu Guinea-Bissau

Mwandishi wa Guinea Atoweka Kiajabu nchini Angola

  31 Disemba 2012

Yuko wapi Milocas Pereira? Swali hili linarudiwa rudiwa kupitia blogu mbalimbali kwa majuma kadhaa sasa, lakini majibu yamekuwa vigumu kupatikana. Katika mitandao ya kijamii harakati zililipuka kuzishinikiza mamlaka za nchi ya Guinea kuchunguza mazingira ya kupotea kwa mwandishi huyo na mhadhiri wa Chuo Kikuu miezi sita liyopita katika jiji la Luanda, alikokuwa akiishi tangu mwaka 2004.

Kitabu-pepe Kipya cha GV: Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko

  30 Disemba 2012

"Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko",  kinakupa mtazamano wa kipekee kuhusu watu na habari za eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia posti zetu zilizo bora zilizoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kwa mwaka 2012. Hii ni zawadi sahihi kabisa ya kuukaribisha mwaka mpya.