Habari kuhusu Ghana

Picha Nyeusi: Waafrika Nchini Italia

  27 Septemba 2013

Picha Nyeusi ni kazi za wapiga picha watatu – Marco Ambrosi, Matteo Danesin na Aldo Sodoma – Kituo cha Stadi za Uhamiaji mjini Verona, Majiji ya Verona na Padua, Chuo Kikuu cha Padua Idara ya Sosholojia ikiwaonyesha Waafrika nchini Italia.

China Yadaiwa Kuchimba Dhahabu Kinyume cha Sheria Nchini Ghana

  9 Juni 2013

Shirika la Habari la Xinhua limeripoti kwamba raia 124 wa Kichina waliodaiwa kushiriki katika uchimbaji wa madini haramu ya dhahabu walikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Ghana. Serikali ya China imetakiwa kulinda na kuwatetea raia wake. Kwa upande mwingine, maoni yaliyotokana na tukio hilo yaliukosoa unyanyasaji unaofanywa dhidi ya watu wa Afrika katika biashara ya...

Kitabu-pepe Kipya cha GV: Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko

  30 Disemba 2012

"Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko",  kinakupa mtazamano wa kipekee kuhusu watu na habari za eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia posti zetu zilizo bora zilizoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kwa mwaka 2012. Hii ni zawadi sahihi kabisa ya kuukaribisha mwaka mpya.

Chama cha Upinzani NPP Chapinga Matokeo ya Urais Ghana Mahakamani

  30 Disemba 2012

Chama Kikuu cha Upinzani nchini Ghana, NPP, kimegoma kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa Rais. Mnamo tarehe 9 Desemba 2012, Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Rais Mahama kuwa mshindi kwa asilimia 50.70 ya kura, akimshinda mshindani wake wa maribu Nana Akufo-Addo wa NPP. Chama cha NPP hapo awali kilifungua mashitaka katika Mahakama Kuu tarehe 28 Desemba, 2012.

Ghana: Vikwazo Vinavyowakabili Wanawake Kimaendeleo

  16 Oktoba 2012

Betty Mould Iddrisu, Jaji na Waziri wa Sheria wa Ghana, anaandika [fr] kwenye blogu ya pambazuka.org: Kufikia ngazi za juu kabisa za utawala si rahisi, na hata unapopanda mpaka juu kabisa, bado unajikuta unakabiliwa na hisia za watu zenye uadui na watu wanakuwa na mashaka na uwezo wako, kwa sababu...

Afrika: Tuzo la Mbuyu wa Dhahabu

  18 Septemba 2012

Wasilisha kisa chako upate fursa kushinda Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu: “Tuzo ya Mbuyu wa Dhahabu ilianzishwa mwaka 2008 kuwahamasisha waandishi wa ki-Afarika waliojikita katika vitabu vya watoto na vijana.”