· Novemba, 2013

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Novemba, 2013

Mkusanyiko wa Makala za Kuvuliwa Madaraka kwa Mbunge Maarufu Nchini Tanzania

  27 Novemba 2013

Ben Taylor aweka mkusanyiko wa makala zinazohusiana na kuvuliwa madaraka kwa Zitto Kabwe,mbunge maarufu na kijana wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema. Zitto: […] alivuliwa nyadhifa zote rasmi na viongozi wakuu wa chama mapema siku ya ijumaa asubuhi. Zitto Kabwe hatakuwa tena Naibu katibu Mkuu wa chama wala...

VIDEO: Serikali Yaharibu Misikiti Nchini Angola

  27 Novemba 2013

Uharibifu wa misikiti isiyopungua 11 katika miezi miwili iliyopita nchini Angola imechochea athari ya hasira kwenye mtandao. Kwa mujibu wa Voz da América [pt], Mamlaka ya Angola ilisema kuwa sababu ya uharibifu ni ujenzi kinyume cha sheria na ripoti&nyingine kuongeza kwamba mchakato wa kuhalalisha Uislamu na dini nyingine katika nchi haijawahi...

MATOKEO: Tuzo za Kwanza za Uandishi wa Kiraia Kuwahi Kutolewa Uganda

  25 Novemba 2013

Tuzo za kwanza za uandishi wa kiraia nchini Uganda (SMAs) zilitolewa kwa mara ya kwanza Novemba 15, 2013 kwenye kituo cha Teknolojia kiitwacho The Hub, kwenye mtaa wa maduka ya Oasis jijini Kampala, Uganda. Malengo ya tuzo hizo, ambayo iliandaliwa na BluFlamingo, yalikuwa: Tuzo hizi za Uandishi wa habari za...

Mkutano wa Global Kampala, Uganda

Sauti Chipukizi  25 Novemba 2013

Mkutano wa Global Voices umepangwa kufanyika Novemba 23 jijini Kampala, Uganda, kuwaleta pamoja wanachama wa jamii hii kushirikisha mawazo.

Huzuni na Hasira Mjini Kidal, Mali

  13 Novemba 2013

Mwanablogu Wirriyamu anaomboleza kuuawa kwa waandishi wa habari wawili wa ufaransa [fr] mjini Kidal, Mali. Lakini kando na huzuni yake kubwa, Wirriyamu pia anajisikia hasira kwa kuona kaskazini mwa Mali inaendelea kutaabika tena kwa mashambulizi ya kigaidi. Anaandika kuhusu hasira ya kimya chake kuhusu hali ya mambo: Tant qu’il ne...

Wa-Malawi Wajiandae kwa Kashfa Zaidi za Ufisadi

  13 Novemba 2013

Steve Sharra anaelezea kwa nini Wamalawi wanakabiliwa na kashfa ya zaidi za ufisadi baada habari kuwa wazi kwamba baadhi ya wa-Malawi wenye nguvu walitumia vibaya Mfumo wa Pamoja wa Ndani wa Udhibiti wa Fedha kupora mabilioni ya fedha za umma: Kutokuwepo kwa usawa wa kijamii kunajenga ufa mkubwa miongoni mwa...

“Nchi” Nzuri ya Afrika

  11 Novemba 2013

Katika toleo la wikii hii la Brainstorm, jarida la mtandaoni la Kikenya, Brenda Wambui hulaani masimulizi ya sasa kuhusu Afrika: “Afrika ni nchi”, “Afrika inapaa”, ‘”Mitindo ya Kiafrika.” Huchunguza jinsi Wakenya wanavyoweza kukomboa simulizi lao na kujiainisha kwa kuweka masharti yao wenyewe: Kama wenyeji wa Kenya ama nchi nyingine ile,...

Mradi Mkubwa wa Reli Kati ya Mji wa Niamey na Cotonou Kuanza

  4 Novemba 2013

Mradi wa reli wa urefu wa kilometa 1,500 kati ya Niamey, mji mkuu wa Niger na Cotonou, mji mkuu wa Benin umepitishwa na mamlaka ya nchi hizo mbili na ujenzi utaanza Machi 2014 [fr].  Francois Ndiaye katika Niamey anaelezea kuhusu makubaliano ya fedha [fr] inayojumuisha wadau mbalimbali na itasimamiwa na kundi la uwekezaji...