The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

India Kumbukumbu za nchi

Kiungo cha RSS kwa India

2009-11-15

Economics ,
Governance

“Takriban asilimia 15 ya watu ambao ni viongozi wa siasa na watumishi wa serikali, kwa kupitia vitendo vya kifisadi, wamejilimbikizia asilimia 85 ya utajiri wote wa India, na kuwaachia asilimia 15 tu ya utajiri huo asilimia 85 ya wananchi,” anasema Ram Bansal katika blogu ya India in Peril.

2009-10-12

Wanablogu Wa Asia Kusini Na Tuzo Ya Nobeli Ya Amani Aliyopewa Obama

Rais wa Marekani Barack Obama amepokea tuzo mashuhuri ya Amani ya Nobeli leo. Wanablogu na wanaoblogu habari fupi fupi huko Asia kusini wanaelezea maoni yao kuhusu habari hiyo.

2009-05-20

Uchaguzi wa India 09: India Imepiga Kura, Imeamua kuimarisha Utulivu

Matokeo ya Uchaguzi yanamiminika kutoka kila upande wa nchi na ni dhahiri kwamba India imepiga kura kwa kishindo ili kuchagua serikali imara ya mseto ya UPA, chini ya uongozi wa chama cha Congress. Dr Manmohan Singh atakuwa Waziri Mkuu kwa mara ya pili mfululizo. Hata kabla matokeo hayajatimia, kwa kuangalia tu mwelekeo, kundi la vyama vya mseto la NDA linaloongozwa na chama cha BJP limetangaza rasmi kushindwa kwake katika uchaguzi.

2009-04-21

Nguvu ya Watu Maarufu Katika uchaguzi wa India

Waigizaji na watengenezaji filamu maarufu nchini India wana ushawishi mkubwa. Kushiriki kwa watoa burudani kutoka Bolywood (watengeneza wa filamu za Kihindi) wenye makao yao huko mjini Mumbai na wale wa filamu za Kitamil na Kitelugu kumepanda ghafla wakati huu wa kampeni za uchaguzi ujao wa India. Soma jinsi ambavyo wachezaji filamu maarufu wa India wanavyotoa ushawishi wakati wa kampeni.

2009-04-14

Wanawake na Uchaguzi Nchini India

Demokrasi kubwa zaidi duniani, India, itafanya uchaguzi mkuu utakaoanza katika wiki chache zijazo kutoka sasa. Wanawake wa India, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinyimwa nafasi yao ya haki majumbani, kazini na katika hatamu za uongozi wana dau kubwa katika uchaguzi ujao. Japokuwa wanawake wengi wanaanza kuwa na ufahamu wa haki zao za kupiga kura na wanashiriki katika siasa kwenye ngazi za chini, ripoti hii inaeleza kwamba inavyoelekea mwaka huu ni wanawake wachache zaidi watakaochaguliwa katika bunge la nchi.

2009-02-27

India: Filamu ya Slumdog Millionaire Yanyakua Tuzo za Oscar

Filamu ya Danny Boyle, Slumdog Millionaire, iliyotokana na kitabu chenye maudhui ya India imefanya vyema katika sherehe za 81 za tuzo ya Academy. Wahusika wake kutoka Uingereza na India walitia kapuni zawadi 8 ikiwemo ile ya Picha Bora. Kwa hakika ilikuwa ni siku ya India, kwa kuwa filamu nyingine fupi ...