· Juni, 2013

Habari kuhusu Asia ya Kusini kutoka Juni, 2013

Uzuri wa Mlima Everesti Nyakati za Usiku

  27 Juni 2013

Sinema fupi za Elia Saikaly zimenasa uzuri mkuu wa Mlima Everesti nyakati za usiku kwa kila sekunde. Anasimulia kwenye blogu yake uzoefu wake wa kupanda hadi kilele cha Mlima Everest kwa mara ya pili.

Vijiwe Vya Usomaji Gazeti Mjini Mumbai Vyazorota

  8 Juni 2013

Vachanalays (vituo vya kusoma magazeti) ni jambo la kawaida katika vitongoji vingi mjini Bombay ambapo wenyeji husoma magazeti na kujadili habari zilizotokea siku husika. Sans Serif anaripoti jinsi vituo hivyo vinavyozidi kupitwa na wakati pole pole. Blogu hiyo pia inaonyesha picha nzuri inayojieleza ya mwanablogu wa picha M.S. Gopal juu ya maudhui hayo...