· Novemba, 2012

Habari kuhusu Asia ya Kusini kutoka Novemba, 2012

Watoto wa Mitaani Bangladesh Wakabiliwa na Unyanyasaji

  13 Novemba 2012

Jumla ya watoto wa mitaani nchini Bangladeshi wanakadiriwa kufikia 400,000. Karibu nusu ya idadi hiyo wanaishi katika Jiji la Dhaka. Asilimia kubwa ya watoto hao ni wasichana. Wasichana hao wa mitaani huishi katika mazingira yenye hatari nyingi hasa unyanyasaji na dhuluma nyingine.

Maelfu Watia Saini Pendekezo la Zawadi ya Nobel na Kusherehekea Siku ya Malala

  12 Novemba 2012

Mwanaharakati wa elimu mwenye umri wa miaka 15 -- Malala Yousufzai -- aliyepigwa risasi mnamo tarehe 9 Oktoba 2012 na wanamgambo wa TTP, anaendelea kupata nafuu japo polepole. Mnamo tarehe 10 Novemba, watu kote ulimwenguni walimpongeza Malala kama kielelezo kwa ajili ya wasichana wapatao milioni 32 ambao hawapati fursa ya kwenda shulen.