The Global Voices Lingua project hopes to bring GV content to new linguistic audiences - Details

Also in:

South Asia Kumbukumbu za sehemu

Kiungo cha RSS kwa South Asia

2009-11-15

India

“Takriban asilimia 15 ya watu ambao ni viongozi wa siasa na watumishi wa serikali, kwa kupitia vitendo vya kifisadi, wamejilimbikizia asilimia 85 ya utajiri wote wa India, na kuwaachia asilimia 15 tu ya utajiri huo asilimia 85 ya wananchi,” anasema Ram Bansal katika blogu ya India in Peril.

2009-11-08

Nepal: Mapinduzi Ya Gesi Inayotokana na SamadiVideo post

Nchini Nepal karibu asilimia 87 ya kaya zinategemea kuni kama chanzo cha nishati. Hata hivyo, vituo vya kuzalisha gesi inayotokana na samadi vinajitokeza kwa idadi kubwa nchini Nepal na kuanzisha mapinduzi ya kijani.

2009-11-04

Pakistan

Mohammad Malick anatoa maoni juu ya shambulizi la kigaidi la hivi karibuni kwenye soko la watu wa tabaka chini na la kati huko Peshawar: “limeonyesha kuwa hii ni vita ambyo magaidi wanasimama upande mmoja wa mstari wa damu, na sisi wananchi upande mwingine.”

2009-10-25

Bhutan

Tshering Tobgay, kiongozi wa chama cha upinzani katika Bunge la Taifa la Bhutan, anatoa maoni kuwa: “mpito wetu kuelekea demokrasi, kwa hakika, umetukia bila mikwaruzo. Umetukia bila mikwaruzo kiasi kwamba wengi wetu walikuwa hata hawaufuatilii.”

2009-10-12

Wanablogu Wa Asia Kusini Na Tuzo Ya Nobeli Ya Amani Aliyopewa Obama

Rais wa Marekani Barack Obama amepokea tuzo mashuhuri ya Amani ya Nobeli leo. Wanablogu na wanaoblogu habari fupi fupi huko Asia kusini wanaelezea maoni yao kuhusu habari hiyo.

2009-08-31

Pakistani: Tatizo La Sukari Limeifanya Ramadhani Kuwa Chungu

Upungufu wa sukari pamoja na kupanda kwa bei nchini Pakistani mwaka huu kumewaathiri walaji na kumesitisha ongezeko la matumizi wakati wa mwezi wa ramadhani. Wanablogu wa kipakistani wanaichambua hali hiyo.

2009-05-20

Uchaguzi wa India 09: India Imepiga Kura, Imeamua kuimarisha Utulivu

Matokeo ya Uchaguzi yanamiminika kutoka kila upande wa nchi na ni dhahiri kwamba India imepiga kura kwa kishindo ili kuchagua serikali imara ya mseto ya UPA, chini ya uongozi wa chama cha Congress. Dr Manmohan Singh atakuwa Waziri Mkuu kwa mara ya pili mfululizo. Hata kabla matokeo hayajatimia, kwa kuangalia tu mwelekeo, kundi la vyama vya mseto la NDA linaloongozwa na chama cha BJP limetangaza rasmi kushindwa kwake katika uchaguzi.

2009-04-14

Wanawake na Uchaguzi Nchini India

Demokrasi kubwa zaidi duniani, India, itafanya uchaguzi mkuu utakaoanza katika wiki chache zijazo kutoka sasa. Wanawake wa India, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinyimwa nafasi yao ya haki majumbani, kazini na katika hatamu za uongozi wana dau kubwa katika uchaguzi ujao. Japokuwa wanawake wengi wanaanza kuwa na ufahamu wa haki zao za kupiga kura na wanashiriki katika siasa kwenye ngazi za chini, ripoti hii inaeleza kwamba inavyoelekea mwaka huu ni wanawake wachache zaidi watakaochaguliwa katika bunge la nchi.