· Januari, 2010

Habari kuhusu Marekani ya Kaskazini kutoka Januari, 2010

Marekani: Dkt. Martin Luther King, Jr. Akumbukwa

Martin Luther King Jr. alizaliwa tarehe 15 Januari, 1929 na akawa mmoja wa wasemaji na watetezi wakuu wa Harakati za Haki za Kiraia huko Marekani. Nchini Marekani, anaenziwa kwa sikukuu ya taifa, inayoadhimishwa kila mwaka siku ya Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari. Leo, wanablogu wengi nchini Marekani wanaadhimisha kumbukumbu yake kwa kuandika makala za kumuenzi, huku wakiungalisha urithi wake wa masuala ya haki za jamii na masuala ya leo, wakionyesha wazi kuwa miaka 42 baada ya kuuwawa kwa King, maneno yake bado yana maana.

Haiti: Ramani za Kwenye Mtandao Zaonyesha Uharibifu Pamoja na Jitihada za Kusambaza Misaada

  19 Januari 2010

Marc Herman anaziangalia kwa karibubaadhi ya ramani ambazo watoaji misaada wanazitumia ili kuwasilisha hali inayobadilika kila wakati katika maeneo ya tetemeko la ardhi nchini Haiti. Karibu ya juma moja baada ya janga kutokea - na matetemeko yaliyofuatia ambayo yalifanana na matetemeko mengine makuu – ramani na taswira za setilaiti zinajidhihirisha kuwa ni taarifa pekee ambazo zinaweza kutegemewa.

Marekani: Raia wa Haiti Wapatiwa Hadhi ya Hifadhi ya Muda

  17 Januari 2010

Hadhi ya Hifadhi ya Muda (inayojulikana kama TPS) ni hadhi maalumu inayotolewa na Marekani kwa raia wa kigeni wanaotoka katika nchi fulanifulani ambamo kunakuwa kumetokea aina fulani ya janga au pigo la karibuni, kama vile vita au tetemeko la ardhi. Jana, Utawala wa Rais Obama ulitoa hadhi hiyo kwa raia wa nchi ya Haiti itakayotumika kwa kipindi cha miezi kumi na nane ijayo. Jillian C. York anapitia jinsi suala hili lilivyopokelewa katika blogu mbalimbali.

Haiti: Maoni ya Mwanzo Kuhusu Tetemeko la Ardhi Lenye Ukubwa wa 7.0

  13 Januari 2010

Posti ya kwanza ya blogu iliyoandikwa kwa lugha ya Kifaransa kuhusu tetemeko la ardhi huko Haiti imetokea nje ya nchi hiyo, ikitangaza habari mbaya za kuanguka kwa Kasri ya Rais, hospitali na majengo mengine na pia tishio la tsunami. Kwa mujibu wa MetropoleHaiti, Marekani tayari imekwishapendekeza misaada ya kibinadamu.