Habari kuhusu Iran

“Iran haiwezi kuufungia Mtandao wa Facebook Milele”

  4 Machi 2014

Waziri wa Utamaduni na Ulinzi wa Uislamu wa Iran, Ali Jannati, alisema “Iran haiwezi kuufungia Mtandao wa Facebook milele.” Maofisa kadhaa wa Iran kama Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Kigeni, hutumia mitandao ya Twita na Facebook hata wakati tovuti hizo zimefungiwa nchini Iran.

Iran: Mwanafunzi Ahukumiwa Miaka 7 Jela

  4 Machi 2014

Blogu ya PersianBanoo iliripoti kuwa “mwanafunzi mwanaharakati wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Qazvin aliyefukuzwa, Maryam Shafipour amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela. Awali iliripotiwa na familia yake kuwa alikuwa amepigwa na maofisa wa kiume waliokuwa wanamhoji wakati wa kuhojiwa kukiendelea”.

Uajemi: Washairi Wawili Watiwa Nguvuni

  2 Januari 2014

Washairi Mehdi Mousavi na Fatemeh Ekhtesari wametokomea nchini Uajemi. Kwa mujibu wa taarifa za habari, washairi hao wamewekwa kizuizini tangu mwanzoni wa mwezi Desemba. Zaidi ya watu mia mbili wametia saini hati ya malalamiko mtandaoni na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kuhusiana na hali za wanaharakati wa...

Iran: Mwanablogu Aliyefungwa Jela Ahitaji Huduma ya Matibabu ya Haraka

  27 Novemba 2013

Mwanablogu aliyefungwa jela,Hossein Ronaghi Maleki anahitaji huduma ya matibabu ya haraka. Alihukumiwa kifungo cha jela cha miaka 15. Laleh alitwiti Mwanaharakati aliyefungwa jela Hossein Ronaghi yuko katika hali mbaya ya afya, kuvimba figo -(moja haifanyi kazi), kibofu cha mkojo na ugonjwa wa kibofu #Iran #Iranelection — Lalehلاله (@Lalehsr) Novemba 25,...