· Machi, 2014

Habari kuhusu Iran kutoka Machi, 2014

“Iran haiwezi kuufungia Mtandao wa Facebook Milele”

  4 Machi 2014

Waziri wa Utamaduni na Ulinzi wa Uislamu wa Iran, Ali Jannati, alisema “Iran haiwezi kuufungia Mtandao wa Facebook milele.” Maofisa kadhaa wa Iran kama Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Kigeni, hutumia mitandao ya Twita na Facebook hata wakati tovuti hizo zimefungiwa nchini Iran.

Iran: Mwanafunzi Ahukumiwa Miaka 7 Jela

  4 Machi 2014

Blogu ya PersianBanoo iliripoti kuwa “mwanafunzi mwanaharakati wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Qazvin aliyefukuzwa, Maryam Shafipour amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela. Awali iliripotiwa na familia yake kuwa alikuwa amepigwa na maofisa wa kiume waliokuwa wanamhoji wakati wa kuhojiwa kukiendelea”.